Rais Trump amesaini amri ya kuiondoa Marekani kwenye uanachama wa Shirika la Afya Duniani (WHO)

Rais Trump amesaini amri ya kuiondoa Marekani kwenye uanachama wa Shirika la Afya Duniani (WHO)

Nkaburu

JF-Expert Member
Joined
Mar 23, 2023
Posts
1,638
Reaction score
1,961
Rais Donald J. Trump ametia saini agizo la kuiondoa Marekani kutoka Shirika la Afya Duniani(WHO) 20 Januari 2025, muda mfupi baada ya kuapishwa kwake

Uamuzi huu umezua mjadala na wasiwasi mkubwa miongoni mwa wataalam wa Afya duniani.

Rais Donald Trump alitaja sababu kadhaa za Marekani kujiondoa kwenye Shirika la Afya Duniani (WHO). Moja ya sababu hizo ni tofauti katika michango ya Kifedha, akibainisha kuwa China pamoja na Idadi kubwa ya watu(population over a billion) inalipa karibia US$40 millioni wakati Marekani yenye idadi ndogo inalipa zaidi ya US$400 millioni.

Source:USAToday.
=======
My take
Tuamke.
 
Nachukizwa na hii tabia ya kutembeza bakuli.. Kuwa ombaomba.. Misaada ni utumwa🤬
JPM ???????

Angalau kwa hili alikuwa sawa?

Kuanza kujaribu kutubadilisha fikra zetu kwamba hakuna mjomba wala shangazi wa kutusaidia kuleta maendeleo bali inabidi tukomae sisi wenyewe na makinikia zetu?
 
Sasa Tundu lissu akichukua nchi atakutana na wakati mgumu sana.
Naona pia ARV zitaanza kuuzwa sasa maana WHO wamepungukiwa mchango wa marekani.
Au mchango wa marekani wa hizo dola hauna athari?
Tutakufa kama kuku sasa
 
Rais Donald J. Trump ametia saini agizo la kuiondoa Marekani kutoka Shirika la Afya Duniani(WHO) 20 Januari 2025, muda mfupi baada ya kuapishwa kwake

Uamuzi huu umezua mjadala na wasiwasi mkubwa miongoni mwa wataalam wa Afya duniani.

Rais Donald Trump alitaja sababu kadhaa za Marekani kujiondoa kwenye Shirika la Afya Duniani (WHO). Moja ya sababu hizo ni tofauti katika michango ya Kifedha, akibainisha kuwa China pamoja na Idadi kubwa ya watu(population over a billion) inalipa karibia US$40 wakati Marekani yenye idadi ndogo inalipa zaidi ya US$400.

Source:USAToday.
=======
My take
Tuamke.
"Tuamke"! Unataka na sisi tujitoe kutokana na kuchangia kiasi kikubwa kuliko China! Twafwaa mayo! Sisi ugonjwa upo tusaidiwe tunasema haupo! Mara haupo ila ni mtu mmoja tu anaumwa! NHIF inatushinda kuiendesha kwa sababu za udokozi usiokuwa na maana, sasa tutakwisha kwani hatutakuwa na watu wa kudhibiti magonjwa yasisambae.
 
Back
Top Bottom