Rais Trump amesaini amri ya kuiondoa Marekani kwenye uanachama wa Shirika la Afya Duniani (WHO)

Rais Trump amesaini amri ya kuiondoa Marekani kwenye uanachama wa Shirika la Afya Duniani (WHO)

Rais Donald J. Trump ametia saini agizo la kuiondoa Marekani kutoka Shirika la Afya Duniani(WHO) 20 Januari 2025, muda mfupi baada ya kuapishwa kwake

Uamuzi huu umezua mjadala na wasiwasi mkubwa miongoni mwa wataalam wa Afya duniani.

Rais Donald Trump alitaja sababu kadhaa za Marekani kujiondoa kwenye Shirika la Afya Duniani (WHO). Moja ya sababu hizo ni tofauti katika michango ya Kifedha, akibainisha kuwa China pamoja na Idadi kubwa ya watu(population over a billion) inalipa karibia US$40 wakati Marekani yenye idadi ndogo inalipa zaidi ya US$400.

Source:USAToday.
=======
My take
Tuamke.

View: https://twitter.com/AutismCapital/status/1881514281189130556
 
Hapa ndio utajua china sio taifa tajili kabisaa...........utajili wa china uko kwa uwingi wa watu tu na sio pesa...............labda na kutuuzia yale makoro koro yao fake........na kuchukua mitonyo yetu original...........ndio maana mi niliwapenda waliokuwa wanawatandika makontena ya michanga na kuwaambia hizo ni korosho
 
Hapa ndio utajua china sio taifa tajili kabisaa...........utajili wa china uko kwa uwingi wa watu tu na sio pesa...............labda na kutuuzia yale makoro koro yao fake........na kuchukua mitonyo yetu original...........ndio maana mi niliwapenda waliokuwa wanawatandika makontena ya michanga na kuwaambia hizo ni korosho
China ni tajiri lakini pesa zake ni kwaajiri ya wachina na sio za kutoa misaada Kwa wavivu na ombaomba
 
Hiyo willingness ya kutoa 400$ na siyo 40$ kama China ndiyo imeipa USA access ya natural resources sehemu mbalimbali duniani na kuonekana ndiye kiranja wa dunia, diplomatic strength. Access ya kuweka military bases all over the world n.k. uhusiano wake na nchi wanachama umekua wa mutual benefit na siyo kwamba USA alikua akitoa hicho kiasi anapata hasara moja kwa moja.

Ingawa kwa kuitaja hivyo inaonekana nyingi lakini misaada anayotoa USA duniani kwenye bajeti yake hua haizidi hata 2% ya mapato yake (last time nasoma juu ya hiyo ishu unless ibadilike)
 
Kujitoa kwa Marekani kutoka Shirika la Afya Duniani (WHO) kunaweza kuwa na athari kubwa kwa Afrika, ikizingatiwa jinsi bara hili linavyotegemea msaada wa kimataifa katika sekta ya afya. Athari kuu ni pamoja na:


1. Upungufu wa Rasilimali za Fedha


Marekani imekuwa mmoja wa wafadhili wakubwa wa WHO, ikichangia takriban 15% ya bajeti ya shirika hilo. Kujitoa kwake kungepunguza rasilimali zinazopatikana kwa miradi ya afya barani Afrika, kama vile:


  • Mapambano dhidi ya magonjwa kama malaria, kifua kikuu, na VVU/UKIMWI.
  • Chanjo na udhibiti wa magonjwa ya mlipuko kama polio na surua.

2. Kupungua kwa Msaada wa Dharura


WHO ina jukumu muhimu katika kushughulikia dharura za kiafya, kama vile milipuko ya magonjwa na majanga ya asili. Kujitoa kwa Marekani kungeathiri uwezo wa WHO kusaidia nchi za Afrika wakati wa dharura za kiafya, kama ilivyoonekana wakati wa milipuko ya Ebola.


3. Kudhoofika kwa Miradi ya Kinga na Uzuiaji wa Magonjwa


Afrika inategemea sana mipango ya kinga inayoungwa mkono na WHO, kama vile Mpango wa Chanjo Duniani (Gavi). Bila msaada wa Marekani, miradi hii inaweza kukumbwa na changamoto za kifedha, na hivyo kuhatarisha afya ya mamilioni ya watu.


4. Athari kwa Ushirikiano wa Kimataifa


Kujitoa kwa Marekani kunapunguza mshikamano wa kimataifa katika kushughulikia changamoto za kiafya. Afrika inaweza kupata changamoto zaidi kushirikiana na WHO kutokana na upungufu wa rasilimali na ushawishi wa kisiasa.


5. Kuongezeka kwa Utegemezi kwa Mataifa Mengine


Nchi za Afrika zinaweza kulazimika kutegemea zaidi msaada kutoka kwa nchi kama China, Umoja wa Ulaya, au taasisi za kibinafsi, ambazo zinaweza kuwa na vipaumbele tofauti.


Kwa ujumla, kujitoa kwa Marekani kutoka WHO kunaweza kudhoofisha juhudi za kuboresha afya barani Afrika, hasa kwa wale walioko kwenye mazingira magumu zaidi.

Source: chat GPT. "AI".
 
Kujitoa kwa Marekani kutoka Shirika la Afya Duniani (WHO) kunaweza pia kuwa na athari kubwa kwa upatikanaji wa dawa za kupunguza makali ya VVU (ARVs) barani Afrika, kwani Marekani imekuwa mdau muhimu katika ufadhili wa mipango ya VVU/UKIMWI. Athari kuu zinazowezekana ni:


1. Kupungua kwa Upatikanaji wa ARVs


Marekani kupitia programu kama PEPFAR (President’s Emergency Plan for AIDS Relief) imekuwa chanzo kikuu cha rasilimali kwa ununuzi wa ARVs na miradi ya matibabu ya VVU/UKIMWI. Ikiwa msaada huu utapunguzwa kutokana na kujitoa WHO, mamilioni ya watu wanaotegemea dawa hizi barani Afrika wanaweza kuathirika.


2. Kuzorota kwa Huduma za Matibabu


WHO inasaidia nchi za Afrika kupitia uratibu wa miradi ya afya, mafunzo ya watoa huduma, na usambazaji wa dawa. Kupungua kwa msaada wa Marekani kunaweza kuathiri utoaji wa huduma muhimu, kama vile:


  • Vipimo vya mara kwa mara kwa wagonjwa wa VVU.
  • Ufuatiliaji wa maendeleo ya matibabu.
  • Huduma za kinga na elimu ya afya.

3. Ongezeko la Maambukizi Mapya ya VVU


Kupungua kwa upatikanaji wa ARVs kunamaanisha wagonjwa wengi wanaweza kushindwa kudhibiti kiwango cha virusi mwilini. Hii inaweza kusababisha maambukizi mapya kwa kasi zaidi, hasa kwa watoto wachanga na wenza wa wagonjwa.


4. Athari kwa Watoto na Wajawazito


WHO, kwa msaada wa Marekani, imekuwa ikiratibu upatikanaji wa ARVs kwa wajawazito ili kuzuia maambukizi ya VVU kutoka kwa mama kwenda kwa mtoto. Kujitoa kwa Marekani kunaweza kudhoofisha juhudi hizi, na kusababisha ongezeko la watoto wanaozaliwa na maambukizi ya VVU.


5. Gharama za Dawa Kupanda


Kupungua kwa rasilimali za kimataifa kupitia WHO kunaweza kulazimisha nchi za Afrika kutafuta suluhisho mbadala, ambazo mara nyingi ni ghali zaidi. Hili linaweza kufanya dawa za ARVs kuwa ghali na hivyo zisifikiwe na walio wengi.


Kwa ujumla, kujitoa kwa Marekani kunaweza kurudisha nyuma maendeleo makubwa yaliyopatikana katika mapambano dhidi ya VVU/UKIMWI barani Afrika, na kuathiri maisha ya mamilioni ya wagonjwa wanaotegemea ARVs kwa matibabu.

Source: chat GPT. "AI".
 
Umeongea ukweli kabisa, kwa ufupi tunaweza sema ni wabinafsi

Marekani itatummia Kila njia kuhakikisha pesa zilizokuwa zinatolewa kama mmisaada zinawezesha watu wao ndani kwanza
Sasa marekani utajiri wake Kwa kiasi kikubwa unatokana na kuumiza nchi nyingine na kufadhiri machafuko mfano DRC, Libya, Iraq na alijaribu Venezuela ikafeli anachotoa ni kidogo sema ili kuiziba mdogo Dunia
 
Rais Donald J. Trump ametia saini agizo la kuiondoa Marekani kutoka Shirika la Afya Duniani(WHO) 20 Januari 2025, muda mfupi baada ya kuapishwa kwake

Uamuzi huu umezua mjadala na wasiwasi mkubwa miongoni mwa wataalam wa Afya duniani.

Rais Donald Trump alitaja sababu kadhaa za Marekani kujiondoa kwenye Shirika la Afya Duniani (WHO). Moja ya sababu hizo ni tofauti katika michango ya Kifedha, akibainisha kuwa China pamoja na Idadi kubwa ya watu(population over a billion) inalipa karibia US$40 wakati Marekani yenye idadi ndogo inalipa zaidi ya US$400.

Source:USAToday.
=======
My take
Tuamke.
Turudi kwenye tiba asilia tulizosema za kishenzi
 
Back
Top Bottom