Robert Heriel Mtibeli
JF-Expert Member
- Mar 24, 2018
- 28,297
- 68,017
RAIS TUMTAKAYE 2020
Na, Robert Heriel
Mwaka huu Mungu akipenda utakuwa mwaka wa uchaguzi kama ilivyosheria kwa nchi yetu.
Huu ni mwaka muhimu sana kwa kila mmoja wetu. Ni Mwaka muhimu kwa sisi vijana, wanawake, wazee, na watoto wetu. Ni mwaka muhimu kwa Wafanyakazi wa kada zote, Watumishi wa serikali na sekta binafsi mwaka huu ni mwaka muhimu sana. Ni mwaka muhimu kwa Wasanii wa sanaa zote, wakulima, na Wafugaji.
Ni mwaka muhimu kwa vijana wote wasio na muelekeo wa maisha, vijana wasomi wote wasio na ajira, huu ndio mwaka muhimu kabisa kwenu. Wafanyabiashara na wajasiriamali huu ni Mwaka muhimu.
Sijawasahau Watu wa Vyombo vya habari, waandishi, watangazaji wote. Mwaka huu ni mwaka muhimu sana. Je unaifanya kazi yako kwa furaha? au unafanya ukiwa huna uhuru? Sitaki majibu yako hapa, ninachotaka kutoka kwako ni kukumbuka kuwa mwaka huu ni muhimu.
Sijawasahau wanasiasa wenye vyama vyao, iwe ni CCM. CHADEMA, ACT - WAZALENDO, TLP miongoni mwa vyma vingine. Huu ndio mwaka muhimu kwenu. Je unafurahia mienendo ya chama chako, je kinakupa uhuru au kinakufanya kuwa Mtumwa wa kusema ndio hata kama ulitaka kusema hapana, je chama chako kinakufanya useme hapana hata kama ulipaswa kuseman ndio? Je kiongozi wa chama chako amekugeuza msukule kukupeleka peleka kama mwanasesere kama mtoto mdogo.
Sijawasahau wanasheria, mwaka huu ni muhimu sana. Najua ninyi ndio mnanielewa vizuri zaidi. Je fani yenu ya sheria haijaingiliwa kabisa, je sheria za nchi zinafuatwa na viongozi waliomadarakani au hawana adabu wanafanya wayatakayo bila kufuata sheria za nchi. Mwaka huu ni muhimu zaidi kwenu.
Wananchi kwa ujumla, mwaka huu ni muhimu sana. Hii ni nchi huru. Je unavyoona upo huru na nchi yako? Au kuna jambo linakufanya uishi kama upo utumwani? Je unauhuru wa kutoa maoni, kueleza mawazo yako hata kama huvunji sheria?
Mwaka huu ni muhimu sana kwetu. Ni mwaka wa uchaguzi. Watanzania wote tuungane kuchagua Rais mwenye sifa za kutuongoza. Tusichague Rais ilimradi tumechagua.
Na huyu ndiye Rais ambaye Watanzania Tunamtaka:
Baada ya kusema hayo, niwaombe Watanzania kuwa tushiriki katika kuchagua viongozi wenye sifa za hapo juu. Ninafahamu kuwa Katiba yetu inaruhusu mtu yeyote kugombea kiti cha urais kama anasifa. Hivyo wapo ambao watagombea Urais pasipo kuwa na sifa nilizozitaja hapo juu.
Mwaka huu usikubali kudharaulika.
Robert Heriel
Taikon Wa Fasihi
0693322300
0711345431

- Tunamtaka Rais ambaye hatatuambia kuwa amekuza uchumi wa nchi wakati uchumi wa mtu mmoja mmoja ni duni. Rais wa hivyo ni mwongo, mlaghai na asiye na sifa za kuwa Rais la taifa letu. Maendeleo hayasemwi mdomoni bali yanaonekana kwa kila mmoja wetu. Tunataka Rais ambaye atatufanya tuone uchumi wetu umekuwa na sio kutupa maneno ya kitoto na kutufanya sisi kama wapumbavu. Kiongozi akikuambia uchumi umekuwa wewe jiulize kuwa; wewe amekuongezea uchumi kutoka wapi mpaka wapi. Yaani kama uchumi wako kwa mwezi ulikuwa ni 200,000/= je umeongezeka mpaka wapi. Kama haujaongezeka zaidi ya kupungua kutokana na gharama za maisha. Piga chini. Wala usisubiri maneno maneno ya kitapeli.
- Rais atakayekuwa na lengo la Kufuta umasikini na siyo kufuta chama chochote cha siasa. Rais tumtakaye mwaka huu ni yule atakayekuwa na Agenda za kufuta umasikini. Sio mwenye lengo la kufuta vyama vingine ili chake kiendelee kuwapo. Huyo Rais hatufai na wala hana sifa kuwapo. Hajui vyama ni sehemu ya ajira kama yeye alivyopata ajira kwenye chama chake. Kufuta chama kingine ni kufuta ajira kwa watu waliomo kwenye chama hicho. Unafuta ajira alafu huajir, hatutaki Rais wa hivi. Tunataka Rais atakaye kuwa na mikakati ya kufuta umasikini ili sisi Watanzania tuneemeke.
- Tunataka Rais atakayeheshimu Watanzania. Mwaka huu tunahitaji Rais ambaye atatuheshimu sisi Watanzania. Ataheshimu mawazo ya kila mmoja wetu hata kama yanatofautiana na yeye. Atakayeheshimu utu wetu na nguvu zetu, na akili zetu. Siyo Rais ambaye hatambui Utu, nguvu na akili zetu kwa vitendo zaidi ya maneno matupu. Kutuheshimu ni pamoja na kujali maslahi yetu kama Wafanyakazi na watumishi wa taifa hili, mishahara yetu, posho na marupurupu. Hatutaki Rais anayesema anatuheshimu wakati kinyume chake ni kuwa anatudharau kwa sababu akishakuwa Rais anajua hatuna cha kumfanya. Kwa sababu Watanzania wenzetu atakaowateua wataungana naye kutudharau Watanzania. Mtu ambaye anadharau Watanzania, ni yule asiyejali maslahi ya Watanzania kivitendo sio blah blah. Rais ambaye haheshimu Wanzania ni yule ambaye hataki kusikia watu wanaotofautiana naye wakimshauri au wakimsema. Rais anayedharau Watanzania ni yule ambaye hajali Mustakabali wa vijana iwe wasomi au wasiosoma. Rais asiyehangaika kuhakikisha vijana wa taifa lake wanapata ajira iwe kwa kuajiriwa au kujiajiri. Huyo hatumtaki.
- Tunataka Rais ambaye atajua thamani ya Mtanzania. Hatutaki Rais ambaye hajali na wala hajui thamani ya Mtanzania. Hata kama Mtanzania ni masikini, hajasoma, au anasifa yoyote ile. Tunataka Rais anayejua thamani yetu. Rais ambaye hajui thamani ya Mtanzania mmoja mmoja huyo hatufai, huyo tumpuuze. Rais ambaye akisikia mtanzania kapotea au kauawa ataagiza vyombo vya ulinzi na usalama kufuatilia na kutoa majibu kwa Umma na hatua kali za kisheria zinachukuliwa. Rais ambaye hajui thamani ya Watanzania atatugeuza tusiwe na umoja wa kitaifa. Rais anayejali watanzania atafanya hata vyombo vya dola kujua thamani ya Watanzania. Atafanya wafanyakazi na watumishi kuhudumia Watanzania kwa kujali. Lakini Rais asiyejua thamani yetu huyo ni adui yetu. Atatutukana kwa vile anajua hatutamfanya chochote. Yapo matusi ya mdomoni na yakivitendo.
- Tunataka Rais ambaye hatalaumu wengine bali atafanya kwa sehemu yake. Rais anayelaumu wengine kikawaida hapendi kulaumiwa. Yeye hutaka aonekane ni bora wakati sio bora. Kikawaida hata mtu anayependa kulaumu wengine hupenda kujisafisha ili hata yeye akikosea ionekane yeye anaafadhali. Tunataka Rais anayeleta maendeleo na sio kila kitu kulaumu watu wengine. Huyo hatufai kwani hatutafika popote. Rais anayelaumu wengine hajui majukumu yake, jukumu la Rais sio kulaumu wengine bali kuondoa lawama, kumaanisha Rais ndiye hupaswa kulaumiwa hivyo ni jukumu lake kuondoa lawama. Sasa ikiwa Rais atakuwa analaumu wengine, je nani wakuondoa hizo lawama?
- Tunataka Rais atakayeheshimu sheria na Katiba. Hii inafahamika kabisa, Hatuwezi mchagua mtu asiyeheshimu Sheria na Katiba ya nchi. Kiongozi wa namna hiyo hatufai hata kidogo.
- Tunataka Rais atakayetupa maendeleo yatupayo uhuru wetu, na wala siyo Rais anayetupa maendeleo yanayonyang'anya uhuru wetu. Uhuru wa kisiasa, uhuru wa kiuchumi, uhuru wa kijamii. Kwa mfano: Rais anaweza akaleta maendeleo katika majimbo fulani ya chama chake alafu muda huo huo akasema majimbo yasiyochama chake hatapeleka maendeleo. Huko ni kunyima watu uhuru wa kisiasa wa kuwa katika chama akipendacho, watu watalazimika kufuata chama chake kwa kulazimika na wala sio kupenda.
- Tunataka Rais atakayehakikisha anaondoa Rushwa na Ufisadi. Tunahitaji Rais ambaye atahakikisha mafisadi wote na wahujumu uchumi wanashughulikiwa kama sheria za nchi zinavyoagiza. Sio mtu imebainika ni Fisadi na mhujumu uchumi lakini anaonekana mtaani.
- Tunataka Rais atakayekuwa na uhusiano mzuri na mataifa mengine. Tunajua zipo nchi nyingine hapa duniani. Tunataka Rais ambaye ataongeza mahusiano mema na mataifa mengine pasipo kuathiri maslahi ya taifa letu. Rais ambaye hajui umuhimu wa mahusiano mazuri na mataifa mengine huyo hatufai.
- Tunataka Rais anayejua kuwa kuinua uchumi ni jukumu la Watanzania wote na wala sio jukumu lake peke yake. Rais anayejua hivyo hupokea ushauri kwa wadau mbalimbali, huwa na mahusiano mazuri na Wafanyabiashara. Anashirikiana na viongozi wenzake kwa upendo. Na ikiwa itatoa makosa basi yatarekebishwa kwa njia njema pasipo matusi au kashfa.