Rais, tunakuomba uvunje Baraza la Mawaziri limekuangusha na limetuangusha Watanzania

Rais, tunakuomba uvunje Baraza la Mawaziri limekuangusha na limetuangusha Watanzania

Msanii

Platinum Member
Joined
Jul 4, 2007
Posts
26,483
Reaction score
40,130
Mheshimiwa Rais, ripoti ya jana uliyoipokea imebeba maudhi mengi sana dhidi ya serikali unayoiongoza na Taifa.

Kama wasaidizi wako hawajakudokeza basi pokea taarifa kuwa upo ukaribu usio wa kawaida kati ya maafisa masuuli na wakuu wa sera yaani wizara ama mawaziri wako. Ukifuatilia kwa makini utagundua kuwa kila mteuliwa kwenye vitengo, idara ama Halmashauri zetu ana godfather au godmother wake huko juu.

Kulindana imekuwa ni chachu ya kila mteuliwa kubakia nafasi yake.

Rais. Iwapo wewe uliapa kiapo cha Uaminifu kwa JMT na hapo tukapata rais mpya. Kulikuwa na ugumu gani kwa PM kuapa upya kiapo cha uaminifu kwako? Hapo Katiba imevunjwa na kurekebisha ni kuvunja Baraza la Mawaziri na kuunda upya.

Uliowarudisha wengi wao walitimuliwa na Mwendazake kwa sababu za kukosa maadili na ubadhirifu. Umewafuta machozi kwa kuwarejeza serikalini na sasa wamehamishia machozi kwao.

Tengua na teua ni zoezi la kudumu kwa sababu wapo Watanzania waaminifu na chapakazi wengi labda hutaki tu

Ni ushauri na siyo shinikizo
 
Back
Top Bottom