Rais tunaomba usikilize vilio vya watanzania, mfumuko wa bei ni mkubwa mno

Ni Tanzania pekee duniani mfanyabiashara anaweza kupanga bei aitakayo bila kujali chochote
Serikali kupitia waziri wa viwanda na biashara angalieni mfumuko wa bei nchini hasa bidhaa za msingi ni mkubwa mno.

Ukiuliza kila kitu unaambiwa ni sababu ya vita ya Ukraine na Urusi.

Sio kweli wafanyabiashara wengi sasa wanajificha kwenye vita hiyo kuumiza wananchi kwa kupanga bei kubwa na kunufaika juu ya hiyo vita.

Swali dogo tu hivi hapa Tanzania kila kitu tunachotumia kinatoka Urusi na Ukraine?

Bei ya Mafuta ya kula kwa lita ni 7000/= na baadhi ya mikoa ni 10,000/= na mafuta mengi yanazalishwa nchini.

Kwanini bei iko hivi. Wiki kama mbili binafsi nilifanikiwa kuona mfanyabiashara mmoja wa duka jumla unashusha shehena ya mafuta na kuficha nyumbani kwake ndani ya fensi na kupanga madumu kama 300 kuzunguka uwanja wa nyumba yake. Lakini mtaani ukiuliza unaambiwa bidhaa hii ni adimu sana sababu ya vita na ndio maana bei ni kubwa kitu ambacho si kweli.

Kwanini Serikali inafumbia macho wafanyabiashara wenye tamaa kuumiza raia wao?

Bei ya vifaa vya stationery nayo haikamatiki. Fikiria kufikia mwezi Machi mwanzoni ream ya karatasi ilikuwa ilikuwa Tsh 8000/= kwa pc1 na katoni yenye ream iliuzwa kwa Tsh 40000/= Ila kwa sasa ream 1 tu ni Tsh 15000/= mpaka 18000 baadhi ya maeneo huku katoni ikiuzwa kwa Tsh 65000/= .

Mbona Zanzibar vitu bei ni rahisi sana kwanini huku bara tunanyanyasika na huku Rais wetu umekaa kimya? Huna huruma na watu wa bara? Mbona Rais Mwinyi katangaza kushusha kodi kwa bidhaa za msingi kwa kipindi hiki cha mfungo ili bidhaa zishuke kwanini huku bara inashindikana?

Mheshimiwa Rais kauli yako uliyoisema kuwa bidhaa nyingi zitapanda kwa sababu ya vita na zitazidi kupanda sana imechukuliwa kama fimbo na wafanyabiashara kuumiza raia.

Serikali ya awamu ya tano bei ya Sukari ilipanda sana na ikawa sukari ni adimu sana lkn kwa umakini wao walihundua ni janjajanja ya wafanyabiashara walikuwa wameficha sukari ili wapandishe bei kwa kwa kuwa ni adimu.

Lkn tuliona Serikali imejitokeza na kutangaza bei kikomo kwa mikoa yote na huku ikifanya msako kukamata sukari iliyofichwa. Kwanin sasa inashindikana?

Kiukweli Rais bila kuwa mkali nchi hii hautafanikiwa kwa chochote. Watanzania wengi walishaharibika wakipata fursa wanawaza matumbo yao na kujinemeesha wao kwa wao.

Nchi hii kwa sasa ndo tuseme ni ya watu wachache? Hapo nchi jirani ya DRC bei za bidhaa za msingi zilipanda majuzijuzi tu, lakini tumeona Bunge wamemta waziri anayehusika na biashara ajiuzulu ndani ya masaa48.

Tanzania hapa kila kitu ni kusifia hata ujinga. Bunge letu mmekosa mamlaka kisheria kuchukua hatua mbalimbali kurekebisha mambo nchini?
Wabunge na mawaziri wameambiwa waruambie ukweli, ( wawe mabalozi wazuri wa mfumuko wa bei )
 
Hebu tuongee ukweli huu mfumuko wa bei uko tanzania pekee?,huu mfumuko kauleta samia?na kwamba huo mfumuko samia unataka afanye nini?
Huna akili wewe mshenzi, pumbavu na mjinga,ni nchi gani ambayo Rais wake ametoka hadharani kusema kuwa vitu vitapanda bei tu sababu ya Vita vya Russia na Ukraine? Ni mmoja tu ambae ni SASHA,wenzake wanajitahidi kufanya jitihada kupunguza mfumuko wa bei lenyewe lipo tu halina hata nini kifanyike kukabiliana na mfumuko wa bei!
 
Tunajua hii ni changamoto ya dunia nzima, lakini je ndio ukae kimya? Tumesikia rais wa Ghana na serikali yake hatua walizochukua tumesikia Kenya jana hata kama hatua hizi ni za uongo kwanini serikali yetu ipo kimya kabisa? Ina maana hakuna hatu inayoweza kuchukua kupunguza mzigo kwa wananchi?.
CCM ikijiloga kuweka tume huru ya uchaguzi 2025 hata 10% ya kura hawapati.

My take:
Kwanini serikali isipunguze matumizi yake?
Kwanini rais asianze kupunguza walau mshahara wake na viongozi wengine wafuate kama ilivyokuwa kwa chanjo ya Uviko-19?
Serikali ipo kwa sababu zao binafsi au sababu ya wananchi?
 
Tunajua hii ni changamoto ya dunia nzima, lakini je ndio ukae kimya?
Bwashee ina maana hujasikia Mh Rais Samia amelitangazia taifa na kuwataarifu wananchi kuwa bei za vitu na gharama za maisha zitapanda?
 
Serikali ya CCM iko very pathetic na inept na ndiyo maana waoga wa katiba mpya. Wanachojali wao ni kulindiana maslahi tu!
 
Tunajua hii ni changamoto ya dunia nzima, lakini je ndio ukae kimya? Tumesikia rais wa Ghana na serikali yake hatua walizochukua tumesikia Kenya jana hata kama hatua hizi ni za uongo kwanini serikali yetu ipo kimya kabisa? Ina maana hakuna hatu inayoweza kuchukua kupunguza mzigo kwa wananchi?.
CCM ikijiloga kuweka tume huru ya uchaguzi 2025 hata 10% ya kura hawapati.

My take:
Kwanini serikali isipunguze matumizi yake?
Kwanini rais asianze kupunguza walau mshahara wake na viongozi wengine wafuate kama ilivyokuwa kwa chanjo ya Uviko-19?
Serikali ipo kwa sababu zao binafsi au sababu ya wananchi?
IMEJIONDOA YENYEWE KWENYE NCHI ZENYE UCHUMI WA KATI BILA KUNGOJA KUONDOLEWA AU KUFUKUZWA. HII HATUA NI MUHIMU MAANA ITASAIDIA KUELEZA MFUMUKO WA BEI.
 
ili waendelee kukopa mikopo ya masharti nafuu [emoji28]
 
Tunajua hii ni changamoto ya dunia nzima, lakini je ndio ukae kimya? Tumesikia rais wa Ghana na serikali yake hatua walizochukua tumesikia Kenya jana hata kama hatua hizi ni za uongo kwanini serikali yetu ipo kimya kabisa? Ina maana hakuna hatu inayoweza kuchukua kupunguza mzigo kwa wananchi?.
CCM ikijiloga kuweka tume huru ya uchaguzi 2025 hata 10% ya kura hawapati.

My take:
Kwanini serikali isipunguze matumizi yake?
Kwanini rais asianze kupunguza walau mshahara wake na viongozi wengine wafuate kama ilivyokuwa kwa chanjo ya Uviko-19?
Serikali ipo kwa sababu zao binafsi au sababu ya wananchi?
Raisi hajui kuwa anaposisitiza gharama za maisha kupanda itamlazimu pia kupandisha mishahara ili kuendana na ongezeko la gharama za maisha [emoji28][emoji28][emoji28]
 
Serikali na EWURA ni waongo mchana kweupe!

Eti tunayo akiba ya mafuta siku 27, ila mafuta yakipanda Bei Duniani, kesho yake yanapanda Bei...Sasa kwa Nini tusiuziwe hiyo akiba Kwa Bei ya Zamani, ili baada ya Siku 27 ndio Bei mpya ianze?

Hii ni Serikali yenye walafi.... Serikali be yenye kujilipa posho, na kutumia maV8 ovyo ovyo.... Matumizi makubwa

Kwa Nini tusinunue huko Russia, mafuta ya discount?

Hakuna mbunge wa CCM mwenye akili ya kusema hili bungeni?
 
Tunajua hii ni changamoto ya dunia nzima, lakini je ndio ukae kimya? Tumesikia rais wa Ghana na serikali yake hatua walizochukua tumesikia Kenya jana hata kama hatua hizi ni za uongo kwanini serikali yetu ipo kimya kabisa? Ina maana hakuna hatu inayoweza kuchukua kupunguza mzigo kwa wananchi?.
CCM ikijiloga kuweka tume huru ya uchaguzi 2025 hata 10% ya kura hawapati.

My take:
Kwanini serikali isipunguze matumizi yake?
Kwanini rais asianze kupunguza walau mshahara wake na viongozi wengine wafuate kama ilivyokuwa kwa chanjo ya Uviko-19?
Serikali ipo kwa sababu zao binafsi au sababu ya wananchi?
Hawajali, wanachojali wao ni kueneza mapolisi mtaani kukamata watu wanaotongoza madada poa.
 
Hebu tuongee ukweli huu mfumuko wa bei uko tanzania pekee?,huu mfumuko kauleta samia?na kwamba huo mfumuko samia unataka afanye nini?
Tatizo sio mfumuko wa bei tatizo ni hatua gani zinachukuliwa angalau kuupunguza... au kuwa na mkakati wa muda mfupi mfano kuondoa kwa dharula baadhi ya kodi, au kutoa ruzuku kwenye bidhaa muhimu au kuaamua kutumia akiba ili kunusuru hali, au kufanya mazungumzo na wazalishaji wakuu ili kupata bidhaa fulani kwa nafuu mfano india imenunua mafuta pipa 150k toka Russia kwa US$25 Kwa pipa ili hali bei maeneo mengine ni usd 108 mpaka 118 kwa pipa... lakini sio kukaa kimya as if nothing happen. Hapo ndio penye tatizo.
 
Bwashee ina maana hujasikia Mh Rais Samia amelitangazia taifa na kuwataarifu wananchi kuwa bei za vitu na gharama za maisha zitapanda?
Kila mtu anajua hata asingetangaza... wananchi tunataka kujua serikali imechukua hatua gani na sio tangazo tu.
 
Serikali na EWURA ni waongo mchana kweupe!

Eti tunayo akiba ya mafuta siku 27, ila mafuta yakipanda Bei Duniani, kesho yake yanapanda Bei...Sasa kwa Nini tusiuziwe hiyo akiba Kwa Bei ya Zamani, ili baada ya Siku 27 ndio Bei mpya ianze?

Hii ni Serikali yenye walafi.... Serikali be yenye kujilipa posho, na kutumia maV8 ovyo ovyo.... Matumizi makubwa

Kwa Nini tusinunue huko Russia, mafuta ya discount?

Hakuna mbunge wa CCM mwenye akili ya kusema hili bungeni?
🤣🤣🤣
 
Back
Top Bottom