Ikaria
Member
- Jul 17, 2019
- 93
- 238
Rais Uhuru Kenyatta leo tarehe 9 Machi, 2021 amefanya kikao na Rais wa Baraza la Ulaya Charles Michel katika Ikulu ya Nairobi.
Viongozi hao wamejadili masuala pana yanayohusu uhusiano wa Kenya na Umoja wa Ulaya yakiwemo:
• Kukuza uhusiano wa sekta binafsi ya Kenya na Umoja wa Ulaya ili kubuni nafasi za ajira.
• Kujenga ushirikiano wa Kenya na EU kwenye masuala yanayohusu kanda ya Afrika Mashariki na Afrika kwa ujumla.
• Kushirikiana katika kufufua uchumi wa Kenya na EU hasa katika kipindi hiki cha Covid19.
Rais Charles Michel alikuwa ameandamana na Simon Mordue, Balozi wa EU nchini Kenya.
Aidha pia katika kikao hicho walikuwepo Raychelle Omamo, ambaye ni Waziri wa mambo ya nje wa Kenya pamoja na Adan Mohamed, Waziri wa utangamano wa Afrika Mashariki.