Ghazwat
JF-Expert Member
- Oct 4, 2015
- 23,718
- 66,267
Mnamo Agosti 28'2013 akiwahutubia wakazi wa Kerera, diwani wa Kiogoro Samuel Aboko Onkwani alinukuliwa akisema, "wale wako karibu na Rais Uhuru Kenyatta wanapaswa kumshauri aache kuvuta bangi."
Matamshi ya Bw Onkwani yalimfanya ashtakiwe kwa kudhalilisha mamlaka ya afisa wa umma kinyume na kipengele cha Penal Code.
Alhamisi katika mkutano na madiwani wa Kisii na Nyamira, Rais Kenyatta alitangaza msamaha kwa diwani huyo na kumwambia asahau yaliyopita. "Sahau yaliyopita na turidhiane"Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Kidigitali katika Ikulu Denis Itumbi alimnukuu Rais Kenyatta.
Bw Onkwani ambaye alikuwa miongoni mwa madiwani wa Kisii na Nyamira waliomtembelea Rais Kenyatta katika Ikulu ya Nairobi alionekana akisalimiana na kupeana pambaja na Rais Kenyatta kama ishara ya msamaha.
Kesi dhidi ya diwani huyo ilikuwa bado inaendelea kortini japo kupitia mawakili Gideon Nyambati na Isaiah Mosota, diwani huyo alikuwa amekanusha mashtaka hayo.
Madiwani 58 kutoka Kaunti ya Kisii na wenzao 29 kutoka kaunti ya Nyamira walikutana na Rais Kenyatta na Naibu Rais William Ruto kupanga ziara ya Rais maeneo hayo na kujadiliana kuhusu miradi ya maendeleo atakayozindua.