Hakuna rafiki wa kudumu wala adui wa kudumu.
Ruto alipoamua kuungana na Uhuru na kumsaidia kumwangusha Raila aliamini kabisa njia ya ikulu ingekua nyepesi kwake. Maskini hakujua angewaza kutumika na kutupwa nje vilevile
Nimpongeze kwa kuamua kukomaa, mwanaume amekataa kushindwa kirahisi, baada ya kutumika. Ila akumbuke tuu kwa ukabila uliokuwepo Kenya bado safari yake ni ngumu bila kuwa na support ya Raila.
Achilia mbali Daniel Arap Moi aliyekua rais japo hakuwa mkikuyu, linapokuja suala la Urais Kenya wakikuyu wapo tayari kufanya lolote Rais awe mkikuyu
Tusishangae kuja kumwona yeye na Raila wakiungana tena kabla ya uchaguzi ujao. Wakiungana Wa luo na Kalenjin wanaweza kushinda na kuvunja mfumo wa ukikuyu kenya na pia wakijipanga vizuri wanaweza kuondoa kabisa roho ya ukabila
Ila wakikuyu nao wanajua kuzaliana!!!!!!
View attachment 1905837
Mungu ibariki Tanzania.
Mwalimu Julius Kambarage Nyerere utaendelea kuwa Rais bora kuwahi kutokea duniani uliyweza kuunganisha taifa kwa kuondoa ubaguzi wa makabila, rangi hata dini