MK254
JF-Expert Member
- May 11, 2013
- 32,408
- 50,809
Swali gumu hilo, mimi pia nimekuwa nikiwaza juu ya suala hilo hilo; je, Isaak Hassan na tume lake wakitimuliwa hapo ndipo itakuwa suluhu kwa vyama vya kisiasa kutokuwa na uaminifu na tume ya uchaguzi? I really doubt that will happen.
Hata kama the next electoral body itasimamia uchaguzi ambao upinzani (CORD) itaibuka washindi, pengine baadhi ya wafuasi wa chama kilichoko mamlakani kwa sasa (JUBILEE) watadai udanganyifu, tume ya uchaguzi ni vibaraka vya upinzani na kuzua rabsha baadaye.
In 2013, mimi nilidhani kutumika kuwa electronic voter registry ingetatua hayo matatizo yote, lakini tena tulishuhudia yale maadai yaliyochipuka ati they could have hacked into the system, that it isnt temper proof after all.
What I think has further provided the CORD the fodder for their current objections against the IEBC is that so-called "chicken Gate Scandal". Otherwise, they had very little basis, for there was limited evidence about that hacking claim.
IMO, I think the solution to this problem of mistrust of the electoral authorities in such young democracies and rather volatile countries as Kenya is by having UN backed international bodies that are independent and impartial to supervise our elections, until such a time that we mature up. But ofcoss too many would oppose such an idea as preposterous, they would argue that would be contravening our national sovereignty.
Tusipochunga, whatever happened in 2007/08 would be chicken feeds in comparison to what would happen in 2017!
Hapo sasa, nchi hizi za Kiafrika hazina nini wala nini, ufisadi ndio kabisa. Natazama sasa hivi kwenye habari, mojawapo wa majaji wakuu bwana Tunoi ametuhumiwa kupokea kitita cha hela nyingi sana ili amwezeshe gavana wa Nairobi aibuke mshindi. Sasa hapo unakuta mfumo wote umeghubikwa kwenye ufisadi.
Wengi huwa wakiteuliwa kwenye nyadhifa zozote zile, huwa ni fursa ya kupiga hela, iwe kule EACC, IEBC, mahakamani. Hamna anayekubali kuitumikia jamhuri ipasavyo.
Kauli yangu ya upinzani kuhamasisha watu wao wajiandikishe kwa wingi, nilimaanisha waifanye hivyo kimya bila hizi vurugu wanazozifanya sasa hivi. Hizi vurugu zao zinawapa taharuki wafuasi wa upande wa serikali, na hapo wanafanya maamuzi ya kujiandikisha kwa fujo.
Mojawapo wa dhana ambazo hufanya watu wa kwetu mlima Kenya kutompigia kura Raila, huwa ni uwoga waliowekewa kwamba jamaa akiibuka mshindi, atazunguka nchi yote akiwakandamiza. Hiyo huwa inaenezwa kwenye vijiji vyote, na sasa walikua wametulia na kuanza kutokua na nia au haja ya ushindani huo, juzi wakati wa uandikishaji, wengi hawakujitokeza kusajiliwa, maana wengi wamechoshwa na umaskini na sera zisizowanufaisha.
Lakini baada ya matukio ya majuzi, picha kwenye runinga za matatu zilizochomwa na vurugu, aisei watu wanaitana kuwa tayari kusajiliwa kishenzi. Yaani vijijini hamna lingine wanaloongea, ni kwamba kila mtu awe tayari kulinda dhidi ya ushindi wa Raila. Wagonjwa, walemavu, wazee, kila mtu amekua na taharuki ya kujiandikisha. Ujumbe ni kumzuia Raila, na sio kwamba wana haja ya Uhuru, lakini kupiga kura kwa fujo wamzuie ilmradi tu.
Ndio maana nasema, ingekua bora sana kwa washauri wa upinzani kuwa makini na jinsi wanavyowashauri hao viongozi wao.