Rais Uhuru Kenyatta ataka Makamishina wa IEBC watimuliwe haraka


Hapo sasa, nchi hizi za Kiafrika hazina nini wala nini, ufisadi ndio kabisa. Natazama sasa hivi kwenye habari, mojawapo wa majaji wakuu bwana Tunoi ametuhumiwa kupokea kitita cha hela nyingi sana ili amwezeshe gavana wa Nairobi aibuke mshindi. Sasa hapo unakuta mfumo wote umeghubikwa kwenye ufisadi.

Wengi huwa wakiteuliwa kwenye nyadhifa zozote zile, huwa ni fursa ya kupiga hela, iwe kule EACC, IEBC, mahakamani. Hamna anayekubali kuitumikia jamhuri ipasavyo.

Kauli yangu ya upinzani kuhamasisha watu wao wajiandikishe kwa wingi, nilimaanisha waifanye hivyo kimya bila hizi vurugu wanazozifanya sasa hivi. Hizi vurugu zao zinawapa taharuki wafuasi wa upande wa serikali, na hapo wanafanya maamuzi ya kujiandikisha kwa fujo.

Mojawapo wa dhana ambazo hufanya watu wa kwetu mlima Kenya kutompigia kura Raila, huwa ni uwoga waliowekewa kwamba jamaa akiibuka mshindi, atazunguka nchi yote akiwakandamiza. Hiyo huwa inaenezwa kwenye vijiji vyote, na sasa walikua wametulia na kuanza kutokua na nia au haja ya ushindani huo, juzi wakati wa uandikishaji, wengi hawakujitokeza kusajiliwa, maana wengi wamechoshwa na umaskini na sera zisizowanufaisha.
Lakini baada ya matukio ya majuzi, picha kwenye runinga za matatu zilizochomwa na vurugu, aisei watu wanaitana kuwa tayari kusajiliwa kishenzi. Yaani vijijini hamna lingine wanaloongea, ni kwamba kila mtu awe tayari kulinda dhidi ya ushindi wa Raila. Wagonjwa, walemavu, wazee, kila mtu amekua na taharuki ya kujiandikisha. Ujumbe ni kumzuia Raila, na sio kwamba wana haja ya Uhuru, lakini kupiga kura kwa fujo wamzuie ilmradi tu.

Ndio maana nasema, ingekua bora sana kwa washauri wa upinzani kuwa makini na jinsi wanavyowashauri hao viongozi wao.
 

Umechemsha kijana. Rudi kwenye hoja za Lumumba.
 
Hivi mkuu zile matatu zilichomwa then zikapelekwa ofisi ya Raila ilikuwaje..?!?
 
Hivi mkuu zile matatu zilichomwa then zikapelekwa ofisi ya Raila ilikuwaje..?!?

Picha kama hizo za matatu kuchomwa ndio zinazua taharuki, bora wapinzani wangeandamana bila kuvuruga. Na ndio tatizo kubwa huwa kwetu, pale wanapokua na tatizo na serikali, badala ya kupambana dhidi ya polisi kama tulivyokua tunafanya miaka ya tisini, watu wanageukana na kupigana wenyewe.

Viongozi kule juu hawajali, hata mpigane hadi wa mwisho, ilmradi vurugu zenu zinaishia humo humo kwenye mitaa ya mabanda basi. Unaichoma nyumba ya mwenzio au daladala/matatu, huyo hapo ni mhangaikaji kama wewe na siye anayehusika kwenye uongozi. Nchi hii tukumbatie amani na kujua ni yetu sote na tuna watoto wanaokua ambao tutawaachia siku za usoni.

Maandamano dhidi ya serikali ni jambo la maana sana, linaifanya dola inakua makini katika utekelezaji wake, lakini tusiwe watu wakugeukana wenyewe.
 
Nakushangaa unapoteza nguvu zako kubishana na Mbuzi.
 
Sasa hao wajumbe wanateuliwa vipi kwa namna katiba inavyoelekeza?
Je wanateuliwa na bunge gavana ama rais? ama inakuwa je hapo? Naomba kuelimishwa.
 
Sasa hao wajumbe wanateuliwa vipi kwa namna katiba inavyoelekeza?
Je wanateuliwa na bunge gavana ama rais? ama inakuwa je hapo? Naomba kuelimishwa.

Hapo itabidi busara itumike bila kuvunja katiba au sheria. Kila upande utateua wajumbe wake waliopo kwenye bunge zote mbili, hivyo ina maana wahusika watakua wabunge na maseneta (japo wadau wengine wanataka wahusishwe).

Kumbuka katiba haijakataza watu wasikutane huko nje na kujadili mambo yao, hivyo watakutana na kujadili na kukubaliana nini cha kubadilishwa kikatiba. Baada ya hapo ipelekwe bungeni kwa mujibu wa katiba. Makubaliano yoyote yatakayofanyika lazima yataishia kujadiliwa bungeni na kufanyiwa maamuzi ya kura ya wabunge.

Tatizo litakua pale watakua na nia ya kubadilisha chochote ambacho kinahitaji kura ya maamuzi (referendum). Hapo patanoga kwa sababu muda wa kufanya hiyo kura wakati pia uchaguzi ndio huu umetukondolea macho ilhali tutakua tunawapiga chini makamishna wa tume ya uchaguzi, patakua hapakaliki. Dah! nchi yangu hii, anyway yangu macho.
 
Hilo halina ubishi ni lazima vigogo wa IEBC wang'oke wote tuunde tume upya, pamoja na Kwamba Kenya kuna Ukabila ila mimi naamini mwaka jana Walishinda kibahati tu tena kwa Kumchukua DP, lakini sasa hivi wamegawanyika ngoja CORD tutawanyoosha Mwaka huu kwa kutinga Ikulu
#ODM2017
 
Hata kule kwetu dhana zilikuwa ni hizo hizo in 2013, kwamba ikiwa Uhuruto wangenyakua uongozi, basi watu wa Nyanza na western wangedhulumiwa sana kwasababu ya perception that Raila ndiye ali-instigate hao vijana wawili kupelekwa huko The Hague. So they would retaliate that by kuwanyima vijana wa huko kazi na wale wote wanaofanya kazi kwenye maofisi za serikali wangechujwa. Yaani hata kama wako na madegree wangenyimwa ajira na hizo nafasi kupewa watu wa R. Valley na Central, hata wale wako na class 8 certificate. Pia upande za huko Western zingeachwa nyuma kimaendeleo kama alivyofanya babake Uhuru, a repeat of the 1960-70s political rivalries that is.
Hapo sasa watu wa huko wakajiandikisha kwa fujo kupiga kura ili kuzuia hayo kutokea. Thank God Uhuru has turned out to be a rather level-headed person. All that hasent come to pass.

I do not think Raila anaweza kuwa na nia ya kuwadhulumu wakikuyu ama kabila lolote lile, lakini ni kweli ulivyosema ni hao watu wake ambao wanaeneza dhana mbaya kumhusu na pia campaign strategies mrengo wake wanazozitumia pia haziwasaidii, zinawaharibia sana.....yani it's "us against them".The campaigns should be focused on issues, about developing the country about promising to fix the problems that the govt currently in charge is failing to address.
I think it is high time Kenya re-engineered how its politics are being conducted cos hii aina ya siasa ambayo inagawanya watu kwa misingi ya makabila na maeneo (na tusipochunga, tuutaanza kuona hata vyama vinaundwa kwa misingi ya kidini, ie Muslims, Christians, Catholics, Protestants, Shias, Sunnis etc). Hii itaelekeza nchi hii pabaya sana miaka ya usoni.
Tuige zile siasa za America au Britain, kukuwa na hivi viama nyingi, kila elections year jubuni vyama ati za kuunganish makabila A, B and C dhidi ya D, E and F hazisaidii na ni za kiupuzi kabisa.
Halafu hilo suala la ufisadi. Kama majaji watapoteza uaminifu, eti wanaweza kununuliwa na wanasiasa ili kuamua makesi in their favor, then we are so done for!

Kenya, more than Somalia is increasingly becoming a dangerous country for this region. No wonder Uganda and the other countries in the region are having second thoughts about collaborating with Kenya in crucial development projects!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…