pingli-nywee
JF-Expert Member
- Sep 16, 2015
- 11,923
- 13,350
Huu ndio muendelezo wa mapigo ya kuipuuza kuibeza na kuiita Corona kaugonjwa kadogo. Sasa hasara itatuandama sisi sote, wakenya kwa watanzania, baada ya rais Kenyatta kufunga boda kati ya Kenya na Tanzania na pia Kenya-Somalia. Amri ambayo itadumu kwa siku thelathini zijazo.
Sio jambo njema wala la kufurahiwa ila haina budi kufikia maamuzi kama haya ili kujilinda dhidi ya maambukizi zaidi ya Corona. Ikitiliwa maanani kwamba Kenya imetimiza hatua nyingi, kwenye malengo yake ya vita dhidi ya maambukizi ya Corona. Hatua zote hizo na shughuli zote hizo zitakua za bure iwapo tutalegeza kamba. Hadi leo hii kwenye boda Kenya imewazuia madereva 78 kuingia nchini, baada ya wao kupatikana wana virusi vya Corona.