Shilingi ina pande mbili, kuna baadhi ya maamuzi ya Magufuli nakubaliana nayo haswa lile la kuwajali maskini na kuamua kutokufunga ili wauza madafu na mabuyu wasibaki ndani Tandale wanahangaika, hilo nampa hongera sana, huyo mzee kakulia kwenye umaskini anafahamu hali ya maisha ya chini, ila sema naye kapitiliza na kuanza kuonekana kama kituko.
Alipoanza kuponda mabarakoa huku akiwashangaa wanaozivaa, mara corona ipo kwa ajili ya kuwahujumu Watanzania, akaachia viwanja vya michezo watu wanakusanyika na kubanana na kupumuliana, yaani akahamasisha watu wasichukue tahadhari kila mtu akarejea maisha yake ya kawaida, hapo ndio alianguka mtihani.
Alipaswa akomalie umuhimu wa tahadhari, yeye mwenyewe akiwa mstari wa mbele, kila akipewa mic awe anaongea na kuhamaisha watu kuwa makini, na pia kuwaacha wataalam na wanasayansi waendelee kufanya yao kama vile kupima na mtu akiaga dunia kwa corona isemwe kweli ni corona sio huo ujuha wa changamoto za kupumua.
Kenyatta kawa mjanja sana kwenye hili, yeye amejua kweli hatutazingatia tahadhari ila kila akiongea huonyesha namna anavyokubali uwepo wa corona na kupambana nayo, na ameachia wataalam wapambane, hivyo hata tukipukutika hakuna anayemsema rais. Leo Tanzania kila anayeaga dunia hata kwa Malaria wananchi wanasema corona na lawama zote zinamshukia rais Magufuli.
Hii imechangia idadi kubwa ya Watz haswa wa kwenye mitandao kuonekana kufurahia hizi tetesi za mzee wao kulazwa, wengi wanaamini kama kweli kalazwa, akipona atalegeza misimamo na kuanza kuhamasisha tahadhari.