Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Duuh,watu ni wagomvi ile mbayaa
Huyu Rais wa Kenya sina imani nae kwa kweli.
Macho yake mekundu na baadhi ya speech kadhaa namuona kama mtu flani ivi mlevi.
Kuna kipindi alikuwa anasalimiana na Raila Odinga nikahisi huyu jamaa alikuwa amekunywa kidogo maana alikuwa anaongea kwa kuvuta mno na kuyumba.
Ni kweli wakuu au ni mtizamo mbaya?
Mkuu kumbuka moshi si ule ule tuu? kwani kunatofauti gani na kutumia sigara?Kenyatta havuti bangi. Huwa anaichoma tu iungue kama ubani anapenda harufu yake.
Na wala hakuanza yeye. Hata baba yake Jomo Kenyatta alikuwa anafanya hivyo.
Mkuu hilo bomba la mafuta la SS kutoka Mombasa Kenya ni la mafuta ya samli au mawese?Ndiye rais wa kwanza Afrika kutia saini ya mswada wa kupunguza riba huku akiwa anamiliki bank kutoka 24% mpaka 12%-14 %
Ndiye rais wa kwanza Africa ambaye sijawai kumsikia akiwakejeri wapinzani wake
Ndiye rais wa kwanza Africa ambaye sijawai kumsikia akiwakejeri majirani zake...
Ujenzi wa reli ya kihistoria kutoka Mombasa kwenda Western Kenya ....
Ujenzi wa bomba la mafuta kutoka Mombasa litaenda mpaka south sudani...
Rais wa kwanza Africa aliyekubali kutengeneza tume huru akiwa madarakani bila kupepesa macho....
Rais pekee anayejichanganya na watu wa kila wawe masikini wawe matajiri
Kikubwa zaidi office ya rais nchini Kenya imetangazwa ndio ofisi pekee isiyokuwa na kiwango cha Rushwa iko chini ya 5% hasa Rushwa ya Ajira .
Ndiye pia rais pekee wa Africa ambaye safari za nje alizozifanya ndani ya mwaka huu pekee zitaongeza pato la taifa kwa 27% kwa mwaka mmoja yaani maana yake hakusafiri kwenda kushangaa au kubembea Bali ni kwa faida ya nchi yake !!
Na mengine mengi tu kiukweli nampenda sana kwa Sera zake akiwa ni msomi wa uchumi naona anaitendea haki hii taharuma yetu
Ndiye rais wa kwanza Afrika kutia saini ya mswada wa kupunguza riba huku akiwa anamiliki bank kutoka 24% mpaka 12%-14 %
Ndiye rais wa kwanza Africa ambaye sijawai kumsikia akiwakejeri wapinzani wake
Ndiye rais wa kwanza Africa ambaye sijawai kumsikia akiwakejeri majirani zake...
Ujenzi wa reli ya kihistoria kutoka Mombasa kwenda Western Kenya ....
Ujenzi wa bomba la mafuta kutoka Mombasa litaenda mpaka south sudani...
Rais wa kwanza Africa aliyekubali kutengeneza tume huru akiwa madarakani bila kupepesa macho....
Rais pekee anayejichanganya na watu wa kila wawe masikini wawe matajiri
Kikubwa zaidi office ya rais nchini Kenya imetangazwa ndio ofisi pekee isiyokuwa na kiwango cha Rushwa iko chini ya 5% hasa Rushwa ya Ajira .
Ndiye pia rais pekee wa Africa ambaye safari za nje alizozifanya ndani ya mwaka huu pekee zitaongeza pato la taifa kwa 27% kwa mwaka mmoja yaani maana yake hakusafiri kwenda kushangaa au kubembea Bali ni kwa faida ya nchi yake !!
Na mengine mengi tu kiukweli nampenda sana kwa Sera zake akiwa ni msomi wa uchumi naona anaitendea haki hii taharuma yetu
Teh....mkuu Kiranga yakweli haya?Kenyatta havuti bangi. Huwa anaichoma tu iungue kama ubani anapenda harufu yake.
Na wala hakuanza yeye. Hata baba yake Jomo Kenyatta alikuwa anafanya hivyo.
For real.Teh....mkuu Kiranga yakweli haya?
Sawasawa mkuu. Niliisoma hii habari miezi imepita sasa. Kwa maoni yangu president Uhuru ni kiongozi poa.....haumizwi na mambo madogo kama hayo kumsema anatumia marijuana. Sipati picha hapa kwetu umseme "bana kubwa" anatumia Mary Jane.For real.
Ila Uhuru kaonesha roho nzuri sana hapa kwenye habari hii ya chini.
Angekuwa Magufuli mtu angenyea debe.
Rais Kenyatta alipomkumbatia diwani wa Kiogoro Samuel Aboko Onkwani nje ya Ikulu ya Nairobi Agosti 4, 2016 na kumsamehe kwa kumwita 'mvuta bangi' mnamo 2013. Picha/ PSCU
Na WYCLIFFE MUIA
Imepakiwa - Thursday, August 4 2016 at 13:21
Kwa Mukhtasari
Rais Uhuru Kenyatta amemsamehe diwani kutoka Kisii ambaye alimtusi kwa kumwambia 'aache kuvuta bangi’.
![]()
RAIS Uhuru Kenyatta amemsamehe diwani kutoka Kisii ambaye alimtusi kwa kumwambia 'aache kuvuta bangi’.
Mnamo Agosti 28, 2013 akiwahutubia wakazi wa Kerera, diwani wa Kiogoro Samuel Aboko Onkwani alinukuliwa akisema, “Wale wako karibu na Rais Uhuru Kenyatta wanapaswa kumshauri aache kuvuta bangi.”
Matamshi ya Bw Onkwani yalimfanya ashtakiwe kwa kudhalilisha mamlaka ya afisa wa umma kinyume na Kipengele cha 132 cha Penal Code.
Alhamisi katika mkutano na madiwani wa Kisii na Nyamira, Rais Kenyatta alitangaza msamaha kwa diwani huyo na kumwambia asahau yaliyopita. “Sahau yaliyopita na turidhiane,” Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Kidigitali katika Ikulu Denis Itumbi alimnukuu Rais Kenyatta.
Bw Onkwani ambaye alikuwa miongoni mwa madiwani wa Kisii na Nyamira waliomtembelea Rais Kenyatta katika Ikulu ya Nairobi alionekana akisalimiana na kupeana pambaja na Rais Kenyatta kama ishara ya msamaha.
Kesi dhidi ya diwani huyo ilikuwa bado inaendelea kortini japo kupitia mawakili Gideon Nyambati na Isaiah Mosota, diwani huyo alikuwa amekanusha mashtaka hayo.
Madiwani 58 kutoka Kaunti ya Kisii na wenzao 29 kutoka Kaunti ya Nyamira walikutana na Rais Kenyatta na Naibu Rais William Ruto kupanga ziara ya rais maeneo hayo na kujadiliana kuhusu miradi ya maendeleo atakayozindua.
Akiwahutubia Rais Kenyatta alisisitiza azma yake ya kutaka kufanya kazi na viongozi kutoka maeneo yote nchini bila kuzingatia mirengo yao ya kisiasa kwa manufaa ya Wakenya wote.
“Nina hakika Wakenya wengi wanataka amani, maendeleo na umoja. Hii ndio maana sisi kama viongozi tunapaswa kuwa na mwelekeo wa pamoja wa kuunganisha nchi,” alisema Rais Kenyatta.
Katika kile kinachoonekana kama kupigia debe chama kinachoendelea kuundwa cha Jubilee, Rais na Niabu wake waliwarai madiwani hao kutembea katika barabara moja nao kisiasa katika juhudi za kuwa na vyama vichache vya kisiasa nchini.
Rais Kenyatta alisema lengo kuu la kuunda chama kipya cha Jubilee ni kuunganisha Wakenya wote. “Siasa za kuwagawanya Wakenya na kuchochea chuki hazitasaidia kuleta maendeleo nchini,” alisema Rais Kenyatta.
Naibu Rais alielezea matumaini yake kuwa viongozi pamoja na wakazi wa Nyamira na Kisii watafanya uamuzi bora wa kuunga mkono Jubilee ifikiapo 2017.
Ha ha ha haiwezekani.. Hii kina Erick Omond ndionwametengenezaNi kweli huyu ndo Rais bora Duniani, ndio maana juzi katuwekea alicho-sign Zuma kwenye daftari la wageni Ikulu.
View attachment 418558View attachment 418560