Rais Uhuru Kenyatta ni mlevi au?




Leta hapa maswala tujadiliane sio watu na maisha yao binafsi, haikusaidii, Uhuru Kenyatta ni mmoja wa marais weledi sana hapa Afrika na dunia ya tatu, the guy is very smart upstairs, he aims b4 he shoots, UK is not a loose canon! And above all, I admire the way he treats people, young and old, rich
and poor, sitamsahau alivyotukimbilia
kuwasaidia wahanga wa tetemeko Kagera, hizo ndio issues za kujadiliana sio mambo ya gizani! Wacha ufukunyungu bro!
 
Kenyatta havuti bangi. Huwa anaichoma tu iungue kama ubani anapenda harufu yake.

Na wala hakuanza yeye. Hata baba yake Jomo Kenyatta alikuwa anafanya hivyo.
Mkuu kumbuka moshi si ule ule tuu? kwani kunatofauti gani na kutumia sigara?
 
Mkuu hilo bomba la mafuta la SS kutoka Mombasa Kenya ni la mafuta ya samli au mawese?

South Sudan is in negotiation with Uganda and Tanzania to use Hoima-Tanga pipeline after DRC Congo
 
Halafu inasemekana hakumaliza shule ni university drop out!
 


Ongezea na hizo

Kenya donates Sh91m to Malawi flood victims

Kenya To Donate US$1 Million For Ebola Fight in Liberia, Sierra Leone & Guinea; Reviews Suspension of Kenya Airways Flights



KENYA: Children Donate Foodstuff to South Sudan – AMECEA Communications
 
Hehehe bora tumewapa rais wetu ili nyie mkejeli maana ukianza mada kama hii kwa rais wa Tanzania lazima ujiandae na milioni saba.

Rais Uhuru kama anapitia JF lazima atavunjika mbavu kwa kicheko akisoma comments za huu uzi.
Jamaican majani popopopo whatagwan peace love and unity.
 
Kenyatta havuti bangi. Huwa anaichoma tu iungue kama ubani anapenda harufu yake.

Na wala hakuanza yeye. Hata baba yake Jomo Kenyatta alikuwa anafanya hivyo.
Teh....mkuu Kiranga yakweli haya?
 
Bonge la sela jombaa ,hata kama unakula majani fanya kuongeza dozi mazee
Una utu sana na sio mtu wa kumaindisha mambo madogo
 
Teh....mkuu Kiranga yakweli haya?
For real.

Ila Uhuru kaonesha roho nzuri sana hapa kwenye habari hii ya chini.
Angekuwa Magufuli mtu angenyea debe.

Rais Kenyatta alipomkumbatia diwani wa Kiogoro Samuel Aboko Onkwani nje ya Ikulu ya Nairobi Agosti 4, 2016 na kumsamehe kwa kumwita 'mvuta bangi' mnamo 2013. Picha/ PSCU

Na WYCLIFFE MUIA

Imepakiwa - Thursday, August 4 2016 at 13:21
Kwa Mukhtasari

Rais Uhuru Kenyatta amemsamehe diwani kutoka Kisii ambaye alimtusi kwa kumwambia 'aache kuvuta bangi’.




RAIS Uhuru Kenyatta amemsamehe diwani kutoka Kisii ambaye alimtusi kwa kumwambia 'aache kuvuta bangi’.
Mnamo Agosti 28, 2013 akiwahutubia wakazi wa Kerera, diwani wa Kiogoro Samuel Aboko Onkwani alinukuliwa akisema, “Wale wako karibu na Rais Uhuru Kenyatta wanapaswa kumshauri aache kuvuta bangi.”


Matamshi ya Bw Onkwani yalimfanya ashtakiwe kwa kudhalilisha mamlaka ya afisa wa umma kinyume na Kipengele cha 132 cha Penal Code.


Alhamisi katika mkutano na madiwani wa Kisii na Nyamira, Rais Kenyatta alitangaza msamaha kwa diwani huyo na kumwambia asahau yaliyopita. “Sahau yaliyopita na turidhiane,” Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Kidigitali katika Ikulu Denis Itumbi alimnukuu Rais Kenyatta.


Bw Onkwani ambaye alikuwa miongoni mwa madiwani wa Kisii na Nyamira waliomtembelea Rais Kenyatta katika Ikulu ya Nairobi alionekana akisalimiana na kupeana pambaja na Rais Kenyatta kama ishara ya msamaha.


Kesi dhidi ya diwani huyo ilikuwa bado inaendelea kortini japo kupitia mawakili Gideon Nyambati na Isaiah Mosota, diwani huyo alikuwa amekanusha mashtaka hayo.


Madiwani 58 kutoka Kaunti ya Kisii na wenzao 29 kutoka Kaunti ya Nyamira walikutana na Rais Kenyatta na Naibu Rais William Ruto kupanga ziara ya rais maeneo hayo na kujadiliana kuhusu miradi ya maendeleo atakayozindua.


Akiwahutubia Rais Kenyatta alisisitiza azma yake ya kutaka kufanya kazi na viongozi kutoka maeneo yote nchini bila kuzingatia mirengo yao ya kisiasa kwa manufaa ya Wakenya wote.


“Nina hakika Wakenya wengi wanataka amani, maendeleo na umoja. Hii ndio maana sisi kama viongozi tunapaswa kuwa na mwelekeo wa pamoja wa kuunganisha nchi,” alisema Rais Kenyatta.


Katika kile kinachoonekana kama kupigia debe chama kinachoendelea kuundwa cha Jubilee, Rais na Niabu wake waliwarai madiwani hao kutembea katika barabara moja nao kisiasa katika juhudi za kuwa na vyama vichache vya kisiasa nchini.


Rais Kenyatta alisema lengo kuu la kuunda chama kipya cha Jubilee ni kuunganisha Wakenya wote. “Siasa za kuwagawanya Wakenya na kuchochea chuki hazitasaidia kuleta maendeleo nchini,” alisema Rais Kenyatta.


Naibu Rais alielezea matumaini yake kuwa viongozi pamoja na wakazi wa Nyamira na Kisii watafanya uamuzi bora wa kuunga mkono Jubilee ifikiapo 2017.
 
Uhuru mnyawaji siyo mlevi. Most sober president Afrika.
 
aliwahi kuwa swaiba mzuri wa Tony Gachoka na sasa ni swaiba wa Sonko kwa misingi ya tell me your friends and i will tell your characters unaweza conclude tu
 
Sawasawa mkuu. Niliisoma hii habari miezi imepita sasa. Kwa maoni yangu president Uhuru ni kiongozi poa.....haumizwi na mambo madogo kama hayo kumsema anatumia marijuana. Sipati picha hapa kwetu umseme "bana kubwa" anatumia Mary Jane.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…