Rais Vladmir Putin asaini kuichukua rasmi mikoa minne ya Ukraine kuwa sehemu ya Urusi

Rais Vladmir Putin asaini kuichukua rasmi mikoa minne ya Ukraine kuwa sehemu ya Urusi

Huyu Putin naye sijui Akili zake zimehama au vipi?

Unatangazaje kuyajumuisha majimbo ambayo hauyadhibiti kijeshi kwa 100%. Mpaka Sasa Urusi imeshindwa kuyateka kijeshi kwa 100% majimbo ya Donbas( Luhansk na Dotnesk). Huko Dotnesk Urusi inamiliki 58% ya Jimbo lote na 80% ya Jimbo la Luhansk. Miji Mkuu wa Zaporhzhzia na Dotnesk (Kramatosk) bado inadhibitiwa na Majeshi ya Ukraine. Mji mkuu wa Jimbo la Luhansk wa Lysychansk na Severodotnesk ndio inadhibitiwa na Urusi TU. Kwanini Putin ameshindwa kusubili Majeshi Yake yateke eneo lote la majimbo hayo Manne?

Maoni yangu

Baada ya ile CounterOffensive ya Majeshi ya Ukraine kuyafurusha Majeshi ya Urusi kwenye Jimbo la Kharkiv,Basi Putin ameona Bora ajitangazie Ushindi Kabla Mambo hayajawa magumu kwa upande wake. Sasa Urusi inataka kutishia Nyuklia Endapo Ukraine itaendelea na CounterOffensive kwenye hayo majimbo. Kama huu mkwala wa Putin utawaingia Marekani na kuogopa kuipa Silaha Ukraine Basi huu utakuwa Ushindi kwa Putin. Ngoja tusubiri tuone.
endelea kuota
 
kuna uwezekano urusi wakimaliza na hili ndo mpango unaofuata
Mrusi kukubali kuchukua mfungwa mmoja wa ukraine tena mpinzani mkubwa wa Zelensky halafu kuwarudishia ukraine wafungwa 200 jamaa wanajua wanachofanya, Putin anaweza akapiga mpaka Kiev na akamuweka huyo jamaa kama rais wa pale
 
Mrusi anatafuta tu sababu ya vita kamili na ukraine, kwa sasa lolote litakalotokea atasema analinda nchi yake, mwanzoni alikua anakwepa kupiga sehemu zenye raia na huko ndo wanajeshi wa ukraine walipokua wanajificha angeua raia yangekua mengine , ila kwa sasa ukraine akiua raia wa hayo majimbo mrusi atachukulia kaua raia wake na yeye ana uhalali wa kukupiga kokote hata sehem za raia wako pia......huo ndo mwisho wa operesheni maalum hii inayofata sasa ni vita kamili
Tena vita mbaya mno,mana oparesheni imeisha
 
Back
Top Bottom