Dalton Elijah
JF-Expert Member
- Jul 19, 2022
- 968
- 1,978
Rais wa Afrika Kusini Cyril Ramaphosa leo Jumatatu amelaani tishio la Rais wa Marekani Donald Trump la kuongeza ushuru kwa mataifa ya BRICS, akisema juhudi za Trump za "kuuadhibu" umoja huo zinawasikitisha.
Trump amekuwa akilishutumu kundi hilo la mataifa 11 -- ambalo pia linajumuisha Brazil, Urusi, India na China -- kwa kile anachokitaja kama sera ya kuipinga Marekani na kuapa kuwatoza ushuru wa ziada wa asilimia 10 baada ya mataifa hayo kukosoa vikali hatua hiyo kwenye mkutano wa kilele huko Rio De Janeiro, Brazil.
"BRICS haitaki kushindana na mamlaka nyingine yoyote," Ramaphosa aliambia shirika la utangazaji la umma la Afrika Kusini, SABC na kuongeza "inasikitisha" kwamba baadhi "wanauona kwa mtazamo hasi na wanataka kuwaadhibu wale wote waliomo kwenye kundi hili".
Trump aidha ametangaza leo Jumatatu kwamba wataanza kupeleka barua za kuongeza ushuru kwa takriban nchi 15 ambazo zimeshindwa kufikia makubaliano ya kibiashara na Marekani.