JanguKamaJangu
JF-Expert Member
- Feb 7, 2022
- 2,780
- 6,607
Mazungumzo hayo yamefanyika pembezoni mwa Mkutano wa Tano wa Tume ya Pamoja ya Kudumu ya Ushirikiano (JPC) kati ya Tanzania na Algeria unaofanyika kuanzia tarehe 30 Julai 2023 hadi 1 Agosti 2023.
Mazungumzo ya viongozi hao yalijikita katika kuendelea kuimarisha ushirikiano wa kirafiki na kidiplomasia ili kuweza kutekeleza diplomasia ya uchumi kwa maslahi mapana ya nchi zao.
Aidha, katika kuendelea kuimarisha ushirikiano Mhe. Waziri Dkt. Tax pamoja na majukumu mengine, atafungua rasmi Ofisi za Ubalozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania tarehe 2 Agosti 2023 Jijini Algiers.
Ufunguzi rasmi wa ofisi za ubalozi huo ni hatua muhimu hasa wakati huu ambapo viongozi hao wamekubaliana kuinua uchumi kupitia sekta za biashara, uwekezaji, nishati, madini, elimu, sayansi na teknolojia, afya na utalii.