Rais wa Angola awasili nchini kwa ziara ya kitaifa ya siku tatu

Rais wa Angola awasili nchini kwa ziara ya kitaifa ya siku tatu

Habari za Zanzibar

JF-Expert Member
Joined
Dec 18, 2024
Posts
651
Reaction score
433
IMG-20261028-WA0138.jpg

Rais wa Jamhuri ya Angola, Mhe. João Manuel Gonçalves Lourenço, amewasili nchini kwa ziara ya kitaifa ya siku tatu inayolenga kuimarisha uhusiano na ushirikiano kati ya Tanzania na Angola.

Rais Lourenço amewasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Dar es Salaam, ambako amepokelewa na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Balozi Dkt. Mahmoud Thabit Kombo (Mb.).

Oktoba 29, 2026, Rais Lourenço atapokelewa rasmi na mwenyeji wake, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, katika Ikulu ya Dar es Salaam. Baada ya mapokezi hayo, viongozi hao watafanya mazungumzo rasmi ya pande mbili kuhusu masuala yenye maslahi kwa nchi zao, kabla ya kukutana na waandishi wa habari kueleza makubaliano na matokeo ya mazungumzo yao.

IMG-20261028-WA0118.jpg

Aidha, Oktoba 30, 2026, Rais Lourenço ataelekea Dodoma, makao makuu ya nchi, ambako atashiriki pamoja na mwenyeji wake katika hafla ya uzinduzi wa Mji wa Serikali Mtumba.

Ziara hiyo inatarajiwa kutoa fursa ya kuimarisha zaidi uhusiano wa kidiplomasia na kupanua ushirikiano kati ya Tanzania na Angola katika maeneo yenye manufaa kwa mataifa hayo mawili.

IMG-20261028-WA0105.jpg
IMG-20261028-WA0104.jpg
IMG-20261028-WA0140.jpg
IMG-20261028-WA0107.jpg
 

Attachments

  • IMG-20261028-WA0137.jpg
    IMG-20261028-WA0137.jpg
    544.2 KB · Views: 5
RAIS wa Jamhuri ya Angola, João Manuel Gonçalves Lourenço, amewasili nchini Tanzania kwa ziara ya kitaifa ya siku tatu inayotarajiwa kuimarisha uhusiano wa kidiplomasia na kufungua fursa mpya za ushirikiano wa kiuchumi, kijamii na maendeleo kati ya mataifa hayo mawili.

Rais Lourenço amewasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Dar es Salaam, ambapo amepokelewa na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Dkt. Mahmoud Thabit Kombo.

Ziara hiyo inatarajiwa kuimarisha mawasiliano ya ngazi ya juu kati ya viongozi wa nchi hizo na kutoa fursa ya kutathmini maeneo ya ushirikiano yaliyopo, pamoja na kubaini fursa mpya zinazoweza kuchochea maendeleo na kuwanufaisha wananchi wa Tanzania na Angola.

Oktoba 29, 2026, Rais Lourenço atapokelewa rasmi na mwenyeji wake, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, katika hafla itakayofanyika Ikulu ya Dar es Salaam.

Baada ya mapokezi rasmi, viongozi hao watafanya mazungumzo ya pande mbili
yatakayolenga masuala yenye maslahi ya pamoja, yakiwemo kuimarisha uhusiano wa kidiplomasia na kupanua wigo wa ushirikiano katika maeneo ya kimkakati.

Mazungumzo hayo yanatarajiwa kufuatiwa na mkutano na waandishi wa habari, ambapo viongozi hao watatoa taarifa kuhusu matokeo ya majadiliano yao na makubaliano yatakayofikiwa.

Katika hatua nyingine, Oktoba 30, 2026, Rais Lourenço ataelekea Dodoma, makao makuu ya nchi, ambako atashiriki pamoja na Rais Samia katika hafla ya uzinduzi wa Mji wa Serikali Mtumba.

Ushiriki wa kiongozi huyo katika hafla hiyo unaipa ziara hiyo nafasi ya kuhusisha diplomasia na juhudi za Tanzania za kuimarisha utawala na maendeleo ya miundombinu ya serikali.
​
Soma pia Rais wa Angola, João Lourenço, Kufanya Ziara ya Kiserikali ya Siku 3 Tanzania

HVxShr6W8AAxU1n.jpg
HVxSizIXQAAY0SW.jpg
HVxShEIXcAABwWX.jpg
 

Attachments

  • HVxSiPNWMAE0X6B.jpg
    HVxSiPNWMAE0X6B.jpg
    105.2 KB · Views: 4
Mbona hajaenda kumpokea raisi mwenzake kaenda waziri?
 
Back
Top Bottom