Baada ya kulivunja maendeleo yalipatikana kwa kufufua uchumi uliokufa enzi za mtangulizi wake. Badhaa dukani zilijaa kama vile unga, sukari, mchele, ngano, mafuta ya taa na ya kupikia, sabuni za kuogea na kufulia. Maduka makubwa nayo hayakuwa nyuma watu wakaanza kuingiza TV, Redio na vitu mbali mbali vinavyotumia umeme. Pia magari ya kila aina hakaanza kuingia kwa wingi yakiwemo mabasi ya abiria, barabara zikapanuliwa kutokana na mahitaji ya kipindi kile, moja ya barabara na alama aliyoacha Mwinyi ni hii ya morogoro road ambapo lile daraja la manzese lilijengwa wakati wa utawala wake, shule za serikali ziliongezeka, na za binafsi pia zikajengwa kwa wingi, nguo za mitumba na dukani zikaanza kuingia kwa wingi hata ww leo unavaa kiatu kizuri, jinsi zuri na unaenda kunyoa salon kwa mashine hizo ni juhudi za Mwinyi ktk kuwaletea maendeleo raia wake. hapo sijataja hospital nyingi za serikali na private zilizojengwa kwa wingi chini ya utawala wake including madawa nk. Hakika Mwinyi ameifanyia mengi ya kiutu nchi hii, na alikuwa na uwezo wa kuthubutu bila kujali nani anasema nini