Huu ugonjwa kweli upo na unaua ila ninachojiuliza ni kwa nini umefanywa ni kitu kigumu sana kiasi watu wametoa ufahamu wao kiasi hiki?
Hii corona mpaka sasa dunia nzima haijaua watu wafikao laki nane kama jirani zetu hapo Rwanda walivyouana mwaka 1994 kwa siku 90_100 watu laki nane.
Corona hii inamiezi takribani saba ila haijafikia Rwanda idadi ya vifo vilivyotokana na machafuko yale na je hapa kuna kitu kinafichwa?
Mnajitoa ufahamu kwa kulinganisha corona na malaria, cancer, mauaji ya kimbari ya Rwanda na mambo mengine mengi, inapaswa ifahamike kwamba
- Hiki kirusi kimeibua taharuki maana ni kipya na hakuna utaalam wowote mpaka sasa ambao umefaulu kukikabili
- Kinawalaza hata matajiri na mapesa yao, hakuna mwenye jeuri dhidi ya corona kwa sasa
- Kinasambaa kwa kasi, imebainika juzi kwamba kinaambukiza hata kwa hewa
- Hakina formula ya nani kinaua na kusaza yupi, kuna taarifa za vijana kufa na wazee kupona, hivyo kikikukuta, hauna uhakika kama wewe ni mmojawapo wa wale watakaopona au kujifia.
Hiyo pointi ya mwisho ndio balaa zaidi ya zote, kwamba kila mmoja angekua na uhakika wa kupona akiumwa corona, wala usingeona taharuki au wasiwasi, maana ukinasa kwenye 18 zake, unatulia ndani ukiwa na uhakika wa kupona kisha baada ya wiki mbili unarudi kwenye mishe zako.
Niliwahi kuumwa Dengue kipindi nikiwa Dar, yaani madaktari waliniambia Dengue haina dawa, nikae ndani na kunywa maji mengi tu siku ziende yenyewe itaniaga.
Hamna kipindi niliwahi kupitia kigumu kama hicho, wiki mbili za Dengue, nilikua nahisi hovyoo kupita maelezo, kila dakika nilikua naona kama ndio mwisho, kifo kinanikondolea macho na hakuna dawa wala nini, mapesa hayanisaidii yaani mwili wenyewe upambane tu. Yaani sitaki hizo habaari kabisa tena nikisikia neno Dengue nywele hunisimama.