Tulipuuza vipi sasa? Umesikia huku kwamba hospital zimezidiwa na wagonjwa? Au umesikia kuna vifo vya covid huku?
Tulifuata taratibu na ndio maana maisha yanaendelea bila shida huku. Tupo na tahadhari zetu kawaida. Sasa sijui huko kwenu ndio hamfuati hizo taratibu maana nchi imesimama na hospitals zimejaa wagonjwa.
Huu ugonjwa kweli upo na unaua ila ninachojiuliza ni kwa nini umefanywa ni kitu kigumu sana kiasi watu wametoa ufahamu wao kiasi hiki?
Hii corona mpaka sasa dunia nzima haijaua watu wafikao laki nane kama jirani zetu hapo Rwanda walivyouana mwaka 1994 kwa siku 90_100 watu laki nane.
Corona hii inamiezi takribani saba ila haijafikia Rwanda idadi ya vifo vilivyotokana na machafuko yale na je hapa kuna kitu kinafichwa?
Hata marehemu Nkurunziza alisema hayo na corona ilipompa salamu matokeo tumeyaona.Huyu alisema covid haimtishi chochote na ni kama mafua kiduchu tu. Ngoja tuone
Anapewa sifa za ushujaa wa kupambana na corona. Shujaa asiyetambulika na WHO.Ngoja tuone sasa kama ataendelea kuchukulia poa
Corona sio malaria! Ugonjwa ambao unabana mapafu na kusababisha kushindwa kupumua sio wa kuchukulia poa kabisacorona ni ugonjwa kama malaria tatizo wajinga ndo wanaupa kiki mpaka umekua maarufu kuliko magonjwa hatari kama malaria na nk...
Rais mpya wa Burundi amebadili msimamo kuhusu Covid 19 baada ya kushuhudia ikimla kichwa NkuruzinzaAnapewa sifa za ushujaa wa kupambana na corona. Shujaa asiyetambulika na WHO.
Nyie mlijichokea, hamna cha taratibu, sema pona yenu ni kwamba hiki kirusi hakiui wtu wengi Afrika, maana hata sisi ambao hatukujichokea na tunaaendelea kupima bila kuficha data hatujafa sana, mpaka sasa tuna vifo 160 miezi yote hiyo.
Hahaha mbona hueleweki budaa! kwa hiyo kupambana na kirusi kisayansi ni kupima pima? kama unaona sisi hatujafanya kitu bhas na nyie fungueni mashule na nyumba za ibada..achieni watu waishi maisha kama zamani.
Ndio, mbinu za kisayansi, pima pima pima kila mmoja, ili ukibaini unacho uchukue tahadhari za kujipiga lockdown na kuwalinda wengine, ikumbukwe kunao wanasambaza bila wao kujua wanacho, na ingekua nafuu kama tungejua kwamba ukiumwa corona una uhakika wa kuishi na kwamba kitatoka chenyewe, ila huo uhakika haupo, kunao wanakufa na hatujapata pattern au formula gani kinatumia kuwaua, unakuta mtu mwenye umri mdogo tu, tena ana mapesa na anapata huduma bora za kiafya lakini kinapita naye tunamzika, ila unakupta mzee maskini ghetto anaumwa corona na kudunda mtaani baada ya wiki mbili.
Kuna watu dhaifu kiafya kwa mfano wanaoumwa presha, kisukari na mengineyo, hawa wanapaswa kulindwa, ukigundua unacho, jiepushe kuwaambukiza, jitie ndani na malimau. Lakini mkijichokea nyote na kuacha kupima, mnakua kama wanaume ambao hulazimisha ngono bila condom kwa machangudoa na kujiaminisha kwamba UKIMWI haupo.
Hiyo kupima pima na lockdown mpaka sasa imewasaidia vipi kumalizana na corona?
Umeshasikia huku Bongo kwamba hospital zimejaa wagonjwa?
Hauwezi ukamaliza shida za corona, iwe kwa sisi tunaopima au kwa nyie mliojichokea, corona itamalizwa pale beberu atagundua chanjo, ila kwa sasa ni kutumia ushauri wa kisayansi wa kuchukua tahadhari, kupima ili kuwalinda walio dhaifu kiafya.
[emoji23] [emoji23] [emoji23] Naona unaotaMimi nachukua hatua,sanitizer,navaa mask,sijichanganyi kwenye misongamano. Magu soon atakuwa covid 19 positive. Inawezekana uchaguzi 2020 ukasogezwa mwezi. Maana yajayo yanasikitisha.....
Unajichanganya, kupima na kuchukua tahadhari ni vitu viwili tofauti.
Kupima ni kupoteza muda na resopurces tu, unapima ili nini? ukishajua mtu mgonjwa then what? Best option ni kuchukua tahadhari thats all.
Sawa kama itakusaidia kuelewa ninachokisema, kupima ni tofauti na tahadhari ila ndio ya msingi zaidi ya zote maana ni vigumu kuchukua tahadhari 100%, kwa namna moja au nyingine utateleza sehemu, lakini ukiwa unapima mara kwa mara na kujihakikishia uko salama hauambukizi watu, basi maisha yataenda.