Rais wa Brazil yuko sahihi, kwanini Waziri Jr Shemtembo hakucheza?

Wakati mwingine kucheza nje ni mipango na connection TU. Tuna wachezaji wazuri hapa lakini hawana connection. Kibu alitaka akajaribu lakini viongozi wa Simba hawakuwa waelewa.
 
Wakati mwingine kucheza nje ni mipango na connection TU. Tuna wachezaji wazuri hapa lakini hawana connection. Kibu alitaka akajaribu lakini viongozi wa Simba hawakuwa waelewa.

Ni kweli
Wachezaji wazuri tunao, na ili waimarike na kuwa wazuri zaidi kiasi cha kuisaidia Starz ni lazima waende nje ya nchi
 
Ni kweli
Wachezaji wazuri tunao, na ili waimarike na kuwa wazuri zaidi kiasi cha kuisaidia Starz ni lazima waende nje ya nchi
Nakataa hilo kaka. Dawa pekee ni:

1. kuwatambua watoto wenye vipaji na maumbo ya mpira mapema, hata kule vijijini.
2. kuwa na vitalu vya kukuzia vipaji kwenye soka
3. Timu zetu za madaraja yote kuwa na mabenchi qualified wa mpira wa miguu
4. Wachezaji kutoka nje kuja kucheza ligi yetu lazima wawe wanaoitwa/cheza timu zao za taifa za vijana na wakubwa
5. Tuboreshe waamuzi wa mpira
6. Viwanja viwe safi kwa kucheza mpira
7.Wachezaji kutibiwa na kula vizuri.
8. Kupewa maslahi mazuri kwa kazi yao

Ziko nchi ambazo wachezaji wake wengi wanacheza ligi za ndani nchini kwao lakini ziko vizuri
 
Unajilinganisha na Brazil wakati timu yako ni ya kawaida, Comoro wako juu sababu ya wachezaji wa kigeni wakati zamani tulikuwa tukijipigia.
Karibuni mataifa yote yanayotamba Afrika ukiondoka nchi chache Kama south Afrika wanatamba sababu ya wachezaji wa kigeni lakini nyinyi mnatulea siasa za vijiweni.
 
Hatuwezi kuweka rehani usalama wetu kwa kuwa na uraia wa nchi mbili watu ili waje kucheza mpira kwetu! Mpira ni kitu kizuri lakini usalama ni kitu kizuri zaidi.
 
Hili ndo tatizo la Timu yetu ya taifa..........Thread louding
 

Nimekutajia mataifa ya África yanayofanya vizuri kwenye michuano ya kimataifa na wanavyobebwa na uwepo wa wachezaji wao kutoka Ulaya na Asia

Sasa nitajie nchi yoyote ya África inayotamba kwenye Afcon na FIFA games inayotumia local players wake wanaocheza ligi ya nyumbani tu
 
Wanabebwa mpaka wapi, kombe la dunia au hadi wapi? Be serious!! Hawa wanabebwa na academies nzuri (c/o ASEC) na selection ya vipaji wenye maumbo makubwa na good coaching. Nothing more. Hawa akina Aziz Ki, Diara, Yao, Mayelle, Nzengeli, Ahuawa, Kipre Jr hawachezi ulaya ili walipitia kwenye vitalu sahihi.
 
Hatuwezi kuweka rehani usalama wetu kwa kuwa na uraia wa nchi mbili watu ili waje kucheza mpira kwetu! Mpira ni kitu kizuri lakini usalama ni kitu kizuri zaidi.
Hivi Tanzania Wana academy ngapi? Wana makocha wangapi wanafundisha nje ya nchi? Taifa letu Kila kitu kinaendeshwa kijanjajanja na haya ndio.matokeo yake.
Uingereza wanachukua makocha wa taifa toka nje sio wajinga Bali wanatoa changamoto kwa makocha wao
 

Mkuu mbona swali langu ni rahisi sana

Nitajie nchi moja África katika michuano either ya Afcon au FIFA games inayotawala kisoka huku ikitumia local players (wanaocheza ligi ya ndani ktk nchi husika) wake na sio wale wanaotokea Vilabu vya Ulaya & Asia

Mind you kwa mujibu wa CAF national team ranking 2024, mataifa 5 bora África ni haya:
1. Morroco
2. Senegal
3. Nigeria
4. Egypt
5. Cote d ivoire
 
Kaka hutaki kunijibu kwanini? Hao wachezaji wa mataifa hayo unaosema hata kama wasingekuwa wanacheza nje ya Africa bado wangetufunga Tanzania vilevile. Hata bila kucheza nje ya nchi bado wangeshika 5 Bora CAF.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…