Rais wa Burundi, Evariste Ndayishimiye alithibitisha dhamira ya Burundi katika kuleta amani nchini DRC

bagamoyo

JF-Expert Member
Joined
Jan 14, 2010
Posts
24,941
Reaction score
28,869
27 February 2025
Ikulu ya Gitega
Burundi

RAIS WA BURUNDI , EVARISTE NDAYISHIMIYE, ABADILI MSIMAMO WA BURUNDI KATIKA KULETA AMANI NCHINI DRC,

Rais Evariste Ndayishimiye akutana na mabalozi wa kigeni wanaowakilisha nchi zao nchini Burundi kwa mara ya pili mwaka huu 2025, na kuleta mapendekezo mapya ya amani.


View: https://m.youtube.com/watch?v=YeVk0-2kSRc
Mheshimiwa Rais Evariste NDAYISHIMIYE, kwa mara nyingine - "ninaongea nanyi tena, maana kukaa kimya juu ya hali mpya inayoendelea DR Congo haiwezekani" .

Mheshimiwa rais Evariste Ndayishimiye anasisitiza Burundi inathibitisha dhamira ya yake katika kuleta amani nchini DRC, akikataa ushiriki wowote wa moja kwa moja wa kijeshi na kupendelea mbinu ya kidiplomasia meza ya maridhiano. Kama ile iliyoanzishwa na rais mstaafu Uhuru Kenyatta kuhusu kuwa mwezeshaji wa kuleta wadau wa mzozo wa Congo katika meza ya maridhiano.

Mabalozi wanamkazia macho mheshimiwa rais kama vile kutaka kujua kiini cha mkutano huu wa pili katika muda mfupi baada ya ule wa mwisho wa mwezi January 2025 juzi juzi tu. Je kuna kitu kikubwa kinatokota ndiyo sababu ya kuitwa Ikulu Gitega ?

Mheshimiwa rais anaelezea wasiwasi wake kuhusu migogoro inayozidi kuleta hali mbaya na anapendekeza mpango wa amani wenye vipengele vitano:

unaozingatia ushirikishwaji wa kimataifa, uondoaji wa vikosi vya kigeni, ujumuishaji wa M23 katika mazungumzo, usitishaji mapigano mara moja na uimarishaji wa mifumo ya kikanda.

Pia mheshimiwa rais Evariste Ndayishimiye , alitoa hakikisho kuhusu uthabiti wa Burundi na kusisitiza uwazi wake wa mazungumzo na Rwanda, huku akithibitisha kuwa nchi yake itajilinda inapobidi.

Rais Evariste Ndayishimiye agusia matishio ya kundi la waasi la FDC kwa nchi ya Burundi, na lile la waasi wa FDLR kwa DR Congo, asema tishio hilo lisiwe kisingizio cha kukoleza vita baina ya mataifa, badala yake njia zingine zinaweza kutumika kumaliza vita hivyo bila kuumiza raia zaidi.

Hotuba yake ya 27 February 2025 kwa mabalozi wa nchi za kigeni ni ya pili ndani ya mwaka huu wa 2025, inaonesha kuna jambo nyeti nchi ya Burundi inataka dunia kufahamu zaidi.

TOKA MAKTABA :

31 January 2025
Bujumbura, Burundi

Burundi: "Rwanda inaandaa jambo dhidi yetu (...), hatutaruhusu litokee", anaonya Ndayishimiye.​


View: https://m.youtube.com/watch?v=mYoRD5C1v8YWakati wa kubadilishana salamu na mabalozi na mabalozi wa heshima walio wawakilishi maalum wa nchi za kigeni walioidhinishwa nchini Burundi, Ijumaa, Januari 31, Rais Évariste Ndayishimiye alielezea wasiwasi wake kuhusu hali ya usalama katika Afrika Mashariki, akishutumu kampeni za Rwanda katika eneo hili lisilo na utulivu.


Rais wa Burundi aliilaumu Kigali, akisema kuwa nchi hiyo jirani inawapa silaha na kuwapa mafunzo wakimbizi wa Burundi katika mazingira ya mzozo wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC).

"Ikiwa Rwanda itaendelea kupata ushindi katika eneo hilo basi na tutegemee pia hilo kupenyezwa katika nchi ya Burundi ," rais Ndayishimiye alisema, akiongeza kuwa nchi yake haitajiruhusu kuingizwa katika vita vya jumla.

Akirejelea mvutano unaoongezeka nchini DRC, rais wa Burundi aliona kuwa eneo lote liko chini ya tishio: "Tuna tishio katika kanda hii. Sio Burundi pekee. Hata Tanzania, Uganda, Kenya, ukanda mzima una wasiwasi. "Alisisitiza kuwa ukosefu wa usalama mashariki mwa DRC ulikuwa na athari mbali zaidi ya nchi mipaka ya nchi hiyo.

Katika hotuba yake, Ndayishimiye alitoa wito kwa jumuiya ya kimataifa kuchukua hatua ili kuepusha ongezeko hilo. Alishutumu "Ukimya" mbele ya matukio ya sasa, akionya kwamba hali inaweza kuwa mbaya ikiwa hakuna uingiliaji kati uliofanywa.

Kauli hizi zinakuja katika hali ya mvutano unaoendelea kati ya Burundi na Rwanda. Mnamo Januari 2024, Bujumbura iliamua kufunga mipaka yake ya ardhi na Kigali, ikishutumu serikali ya Paul Kagame kwa kuunga mkono kundi la waasi la RED-Tabara, linalofanya kazi mashariki mwa DRC. Rwanda daima imekanusha shutuma hizi.

Burundi, inayoshiriki pamoja na DRC katika mapambano dhidi ya makundi yenye silaha yanayofanya kazi mashariki mwa nchi hiyo, inapinga aina yoyote ya uungaji mkono wa harakati za waasi.

Uhusiano wa kidiplomasia kati ya nchi hizo mbili za Burundi na Rwanda bado umejaa kutoaminiana, licha ya majaribio ya ukaribu yaliyoonekana katika miaka ya hivi karibuni.

Rais wa Burundi alisisitiza kuwa mzozo wa usalama wa DRC haukuathiri nchi jirani pekee, bali pia mataifa ya mbali zaidi, kama vile Afrika Kusini, ambayo wanajeshi wake wanashiriki ndani ya SADC nchini DRC.

"Waafrika Kusini wanateseka mashariki mwa Kongo. Bado angalia Afrika Kusini ilipo! " aliwaambia wanadiplomasia. Alionya kuwa bila majibu yaliyoratibiwa, kila nchi itaishia kukabiliwa na matokeo ya mzozo pekee yake .

Huku mvutano ukiendelea kuwa mkubwa katika eneo la Maziwa Makuu, Burundi inathibitisha tena kuwa macho kutokana na vitisho inavyoona kwenye mipaka yake
 
Kama ile iliyoanzishwa na rais mstaafu Uhuru Kenyatta kuhusu kuwa mwezeshaji wa kuleta wadau wa mzozo wa Congo katika meza ya maridhiano.

TOKA MAKTABA :

Toka maktaba :

Mazungumzo ya Nairobi I na Nairobi II kuhusu Congo chini ya rais mstaafu Uhuru Kenyatta kuhusu utatuzi wa mzozo wa Congo ( Mahojiano kwa KiSwahili)


View: https://m.youtube.com/watch?v=BI5HRv7WVrA
Uhuru Kenyatta, rais wa zamani wa Kenya, aliyeteuliwa kuwa mwezeshaji wa mchakato wa Nairobi na Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC), anatathmini safari yake ya saa 48 mjini Kinshasa tangu Jumapili, Novemba 13, 2022. Pia inashughulikia suala la usalama mashariki mwa DRC.

Mstaafu Uhuru Kenyatta alikutana na mheshimiwa Rais Felix Tshisekedi wa DR Congo na kiongozi mkuu wa MONUSCO (SRSG-Head of MONUSCO), Bi. Bintou Keita .... kuhusu vita inayoendelea na kuona kwa njia gani wanaweza kusaidiana na wananchi wa kabila mbalimbali na jamii mbalimbali mbalimbali

Mwezeshaji wa mchakato wa Nairobi rais mstaafu Uhuru Kenyatta anasema wakutoka nje wenye maslahi binafsi wanawagawa siyo kwa mapendo bali wanaangalia madini kwa manufaa yao na kuwa bunduki na risasi haziwezi kuleta amani juu ya mzozo wa Mashariki ya Congo

Nimepewa jukumu hili na Jumuiya ya Afrika ya Mashariki EAC kuwa bunduki na risasi haziwezi kuleta ushindi wowote, mimi nimetoka Ethiopia kule wamakubali Tigray na Amhara kuwa bunduki na risasi hazileti amani na ujumbe wangu kwa Congo ni huo huo asisitiza rais mstaafu Uhuru Kenyatta

Jukumu letu kama viongozi ahadi kubwa unayoweza kutoa kwa raia ni usalama wao kwa kuhakikisha hakuna umwagaji wa damu ili watu waendelee na maisha yao ya kujiletea maendeleo

Shida zilizopo zitatuliwe kisiasa na tusiwe na fikra kuwa jamii moja inaweza kushinda pekee bali wakongomani wa aina zote wakae pamoja kwa mazungumzo

Mazungumzo ya mèzani ni muhimu iwe M23 au serikali wote kwa kuweka bunduki chini, njia ya nguvu haitafauli na wala haitaleta ushindi ...
 
Hii ni ishara tosha hatuwezi kutatua migogoro yetu wenyewe. Hivi mtu mkorofi kama Kagame anaogopwa au anadekezwa? Kwanini wasiamue kufunga mipaka yake yote tuone hao waasi wanapata wapi Silaha.

Au badala ya hizi nchi kulinda amani, ziingie vitani kwanza, kukitulia ndio walinde amani huku njia za kidiplomasia zikifuata.
 
Hii ni ishara tosha hatuwezi kutatua migogoro yetu wenyewe

Tayari mheshimiwa rais jenerali Rais Evariste Ndayishimiye ameingia woga mkubwa, amebadilisha matishio aliyokuwa anatoa kwa Rwanda baada ya kuona wako Bukavu kilometa chache kutoka Bujumbura.

Rais Evariste Ndayishimiye ambaye ni mlaji wa taarifa za kiintelejensia atakuwa amepewa data zilizochakatwa na Idara yake ya Usalama na ile ya utambuzi jeshini (military intelligence) kuwa kuna tishio kubwa utawala wake kutingishwa.

Ikumbukwe majeshi ya Burundi yamekuwa yakishirikiana na jeshi la FARDC kutaka kuivamia Rwanda lakini wakakurupushwa na M23 ambayo imeyarudisha majeshi ya FARDC na Burundi hadi Bukavu.


TOKA MAKTABA :
22 February 2025

MGOGORO WA DR Congo : Yaliyokutwa katika ghala la silaha za askari wa Tshisekedi na mipango yake ya kuvamia Rwanda


View: https://m.youtube.com/watch?v=STZBGC_UncEMhariri mtendaji James Munyaneza wa The New Times Rwanda atoa ushuhuda wa kina alipopata fursa kuwepo Goma na leo akiwa studio pamoja na mwandishi James Kahuranga kwa njia ya simu akiwa Rusizi kutupa habari za kina...

Inaonesha FARDC walikuwa wamejipanga kuivamia Rwanda kutokana na mpangilio wa zana zilivyopangwa (formation) kuelekea nchi ya Rwanda. Mhariri mtendaji James Munyaneza anasimulia kwa undani hali hiyo alivyokuwa amejipanga Tshisekedi ..

Mhariri mtendaji James Munyaneza alichokiona Goma ni uthibitisho unaoweza kuchukuliwa kuwa kulikuwa na mkakati mpana wa jeshi la Congo FARDC, Burundi kuivamia Rwanda kama tukio la bahati la M23 wasingejitokeza na kutibua mipango hiyo kwa ...

Mhariri mtendaji James Munyaneza aliweza kufika eneo la Airport ya Goma ambapo kilikuwa kitovu cha mapambano makali baina ya FARDC na M23 yaliyotokea wiki mbili zilizopita ....

Mhariri mtendaji James Munyaneza aliweza kufika kambi iliyokuwa na hadhi ya Joint Command Centre iliyokuwa inaratibu mipango ambapo kulikuwa na milingoti minne ya bendera kuwakilisha jeshi la Congo FARDC, jeshi la Burundi, jeshi la SADC SAMIDRC, jeshi la BURUNDI na FDLR - mgambo wa intarahamwe

Na kuwa ...Joint Command Centre hiyo ni kambi ongozi ya Operesheni za kijeshi kuna nyaraka na ramani zilizotokana ukusanyaji wa intelejesia ya kijeshi zinazobainisha maeneo mkakati nyeti ambayo FARDC na FDLR wangeyashambulia Rwanda... zilizoachwa baada ya kambi hizo kukimbiwa kufuatia kipigo kutoka kwa M23

Kilima Nyoka vilikuwepo vikosi special forces wa FARDC wakiwa wamejichimbia wanataza mpaka wa Rwanda na Kanyamahoro kulikuwepo kambi ya FDLR iliyo kilometa 3 tu kutoka mpaka na Rwanda..

Kambi zenye majina ya Satan 2 (shetani) Armageddon (Ziwa la Moto) majina hayo yakiashiria unyama unyama na silaha kali za maangamizi zilizo tayarishwa kuishambulia Rwanda ...

Kambi za mamluki waliosema ni 'wataalamu' kwa kumaanisha wangekuwa wanatoa ujuzi wa kutumia silaha hizo za maangamizi za 'shetani' na 'Ziwa la Moto' kuitia adabu Rwanda ..

Kwa hiyo majeshi haya FARDC, kikosi cha ulinzi wa Rais, FLDR, mamluki wote hawa wangejiunga pamoja kuivamia Rwanda kwa kustukiza ... kama M23 wasingeanzisha mashambulizi February 2023..

Makontena yaliyosheheni silaha za mizinga ya masafa marefu ya kila aina , RPG , sniper rifles, kamikaze drones, camera ikionesha ingekuwa vita ya kisasa ...

Masimulizi hayo ya Mhariri mtendaji James Munyaneza yanakwenda na video mwendo ndani ya mahojiano haya ya ushuhuda wa kina..

Wataalamu kijeshi, utambuzi (intelejensia) ya kijeshi na intelejensia ya kiraia wanasema mkusanyiko huo wote wa mikakati, silaha, utaalamu, matayarisho mazito ya upande wa serikali ya Tshisekedi jirani na mpaka wa Rwanda. i
The missiom was to topple the Rwandan government and that mission has aborted
Inaonesha hayakuwa kujitayarisha kuishughulikia majeshi ya waasi wa M23 bali lengo lilikuwa kukamilisha tamko la Tshisekedi kuwa wataipiga Rwanda na kubadilisha uongozi wa kiserikali uliopo nchini Rwanda..
 
Yani atishwe na nani sasa Rwanda? Mbona huyo Kagame mnamuogopa sana? yeye hafi yani ni Immortal?

Burundi kaongea vizuri sana, Huyo Rwanda ndiye mwenye tatizo kwenye eneo hilo, anataka kuongeza ukubwa wa nchi yake.

Binafsi mimi ningekuwa hizi nchi zinazolinda amani, ninge watandika M23 kwanza kisha ndio tulinde amani.
 

Mambo yanazidi kuchangamka Kinshasa na Bujumbura watawala wame panick, sasa wanataka mazungumzo
 
Tanzania na Kenya zinaweza kufunga mipaka dhidi ya Uganda na Rwanda na ndani ya muda mfupi tu kagame na genge lake la m23 wangeufyata.
 
Tanzania na Kenya zinaweza kufunga mipaka dhidi ya Uganda na Rwanda na ndani ya muda mfupi tu kagame na genge lake la m23 wangeufyata.
Unafkiri kagame alikuwa mjinga kuwekeza kwenye usafiri wa anga?
 
Unafkiri kagame alikuwa mjinga kuwekeza kwenye usafiri wa anga?
Kagame ni mtu mdogo sana ni vile ego is getting to his head labda Museveni inaweza kuwa shida! Kama Kenya wasingekuwa upande wa Kagame na M23 lingewezekana! Na believe me angeondoa wanajeshi wa M23! Hana jeuri! Akiendeleza ujinga na bandari Mombasa na Dar zinafungwa!
 
Wewe unaishi zama za mawe
 
Tanzania na Kenya zinaweza kufunga mipaka dhidi ya Uganda na Rwanda na ndani ya muda mfupi tu kagame na genge lake la m23 wangeufyata.
Yaani kwa sababu ya endless ethnicity war yenu ndio Kenya na Tanzania zifunge mipaka?
 
Burundi kaongea vizuri sana, ngoma bado mbichi
 
Sasa unataka kusema akizuiwa anga atafanya nn? Rwandair inatumia anga ya DRC kwa Sasa? Kama DRC imeweza kuwazuia ishindwe Tanzania na Kenya?
Ndio maana nakwambia unaishi zama za kale

Tanzania haina ushawahi wowote kwa sasa east africa

Mseven na kenya ndio wanaamua nini kifanyike

Nao hao ni rafk wa kweli wa rwanda

Sisi rafki etu wa kweli ni burundi kwa sasa😁
 
Mkuu haya mambo huwa yanachagizwa na watu kama wewe either kwa kujua au kutokujua. Huyu mburundi unaemtetea si ndio alikuwa mstari wa mbele kufunga border na kutangaza kuwa ataivamia Rwanda na hizi taarifa zipo BBC na hata African journal waliandika? Ni bora hata ungesema kuwa kwa kufanya hivyo atakuwa amemsaliti Tishekedi sababu yeye ndio chanzo cha yeye kukataa usaidizi toka EAC na AU.
 
Ndio maana nakwambia unaishi zama za kale

Tanzania haina ushawahi wowote kwa sasa east africa

Mseven na kenya ndio wanaamua nini kifanyike

Nao hao ni rafk wa kweli wa rwanda

Sisi rafki etu wa kweli ni burundi kwa sasa😁
jidanganye mbele ya Kenya hamna rafiki wa kweli! Halafu wewe inakaa unatumia id fake ni Mtutsi! Angalia kuhadi Kagame anavyolalama baada ya UK kumlima sanctions! UK wakitangaza woote wanaom-support Kagame nao wanapigwa sanctions, unafikiri Kenya itabaki?
 
Afrika tujifunze kumaliza migogoro yetu kwa mazungumzo.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…