Ojuolegbha
JF-Expert Member
- Sep 6, 2020
- 1,773
- 1,174
RAIS WA FINLAND AZINDUA MRADI WA KUONGEZA THAMANI BIDHAA ZA MISITU
Rais wa Jamhuri ya Finland Mheshimiwa Alexander Stubb amezindua mradi unaolenga kufadhili shughuli za ubunifu wa kuongeza thamani bidhaa za misitu utakaotekelezwa nchini kupitia Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP).
Mradi huo unaowalenga zaidi vijana, utalisaidia kundi hilo kukuza ubunifu na kujiongezea kipato kupitia rasilimali za misitu na kuchangia katika juhudi za kulinda mazingira.
Akizungumza wakati wa uzinduzi wa mradi huo, jijini Dar es Salaam Mheshimiwa Alexander Stubb alisema mradi huo utasaidia kuongeza kipato cha wakulima wa misitu na wajasiriamali, kutokana na upatikanaji wa teknolojia na mbinu za kisasa za usindikaji wa mazao ya misitu kupita ufadhili huo. Aliongeza kuwa ufadhili huo utasaidia kupunguza athari za uharibifu wa mazingira kwa kutumia njia endelevu za kilimo cha misitu.
Katika uzinduzi huo Rais Stubb aliambatana na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Balozi Mahmoud Thabit Kombo (Mb.), Waziri wa Maliasili na Utalii Mhe. Balozi Dkt. Pindi Chana, wanadiplomasia na viongozi wengine waandamizi wa Serikali kutoka Tanzania na Finland.
Mradi huo ni sehemu ya jitihada za Rais Stubb na Serikali ya Finland za kukuza ushirikiano wa kiuchumi na kijamii na Tanzania, vilevile kuunga mkono agenda ya Serikali ya Tanzania na Kimataifa ya utunzaji wa mazingira na maendeleo endelevu.