Damaso
JF-Expert Member
- Jul 18, 2018
- 3,978
- 6,739
Rais wa Ghana, John Mahama ametangaza marufuku ya safari za Ndege za daraja la kwanza kwa Maafisa wa Serikali wakiwemo Mawaziri ikiwa ni sehemu ya juhudi za kupunguza matumizi ya Serikali.
Aidha Rais Mahama amesisitiza kuwa safari za dharura pekee ndizo zitakubaliwa na lazima zidhinishwe na Ofisi ya mkuu wa Wafanyakazi.
Aliongeza kwa kusema kuwa Maafisa wanapaswa kuepuka matumizi ya anasa na kutumia rasilimali za umma kwa busara akisisitiza kuwa fedha za Serikali zinapaswa kuelekezwa katika kuboresha maisha ya Wananchi wa Ghana badala ya kupotezwa kwenye anasa.