Rais wa Ghana,
John Mahama ametangaza marufuku ya safari za Ndege za daraja la kwanza kwa Maafisa wa Serikali wakiwemo Mawaziri ikiwa ni sehemu ya juhudi za kupunguza matumizi ya Serikali.
View attachment 3232547
Aidha
Rais Mahama amesisitiza kuwa safari za dharura pekee ndizo zitakubaliwa na lazima zidhinishwe na Ofisi ya mkuu wa Wafanyakazi.
View attachment 3232548
Aliongeza kwa kusema kuwa Maafisa wanapaswa kuepuka matumizi ya anasa na kutumia rasilimali za umma kwa busara akisisitiza kuwa fedha za Serikali zinapaswa kuelekezwa katika kuboresha maisha ya Wananchi wa Ghana badala ya kupotezwa kwenye anasa.