Rais wa Guinea-Bissau, Umaro Sissoco Embaló, amewasili nchini Senegal siku ya Alhamisi baada ya kudaiwa kushikiliwa na jeshi wakati wa mapinduzi ya kijeshi yaliyotokea nchini mwake, serikali ya Senegal imethibitisha.
Katika taarifa, Wizara ya Mambo ya Nje ya Senegal ilisema: “Ndege maalum iliandaliwa na Serikali kwenda Bissau kwa ajili ya kusaidia operesheni hii ya kumrejesha. Hii imemuwezesha Rais Umaro Sissoco Embaló kufika Senegal akiwa salama.”
Mapema Alhamisi Novemba 27, 2025, jeshi la Guinea-Bissau lilimteua jenerali mmoja kuwa kiongozi mpya wa nchi hiyo, siku moja baada ya kuchukua madaraka kwa nguvu na kusimamisha kutangazwa kwa matokeo ya uchaguzi.
Soma pia Jeshi la Guinea-Bissau lachukua madaraka baada ya Uchaguzi wenye utata
Mgombea wa upinzani, Fernando Dias da Costa, aliambia shirika la habari la AFP kuwa anaamini alishinda uchaguzi wa Jumapili na kudai kuwa Embaló — ambaye pia alijitangaza mshindi — “alipanga” mapinduzi ili kumzuia kuchukua madaraka.
Mapinduzi hayo yalitokea siku moja kabla ya kutangazwa kwa matokeo ya awali ya uchaguzi wa rais na wabunge.
Jenerali Horta N’Tam, Mkuu wa Majeshi, aliteuliwa kuwa kiongozi wa nchi kwa kipindi cha mwaka mmoja. Alikula kiapo katika makao makuu ya jeshi akisema: “Nimekula kiapo kuongoza Kamandi Kuu.”
========
Guinea-Bissau’s President Umaro Sissoco Embalo has arrived in Senegal after being detained during a military coup in his country, the Senegalese government said on Thursday.
“An aircraft was chartered by the Government to travel to Bissau in order to assist in this repatriation operation. This allowed for the safe and sound arrival in Senegal of President Umaro Sissoco Embalo,” the Senegal Foreign Ministry said in a statement.
The military in Guinea-Bissau earlier on Thursday appointed a general as the country’s new leader, a day after seizing power and halting the announcement of election results.
Opposition candidate Fernando Dias da Costa told AFP he believed he had won Sunday’s election and alleged that Embalo — who also claimed victory — had "organised" the coup to prevent him from taking office.
The coup came one day before the provisional results of the presidential and parliamentary elections were due to be released.
General Horta N’Tam, chief of staff of the army, was designated as the country’s leader for a one-year period.
He took the oath of office at military headquarters, declaring: "I have just been sworn in to lead the High Command."
Source: TRT AFRIKA