Rais wa Indonesia kuwasili Tanzania, leo Agosti 21 katika ziara ya siku mbili

Rais wa Indonesia kuwasili Tanzania, leo Agosti 21 katika ziara ya siku mbili

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Joined
Apr 18, 2017
Posts
3,984
Reaction score
13,760
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Dkt. Segomana Tax ameelezea ujio wa kiongozi huyo, Rais wa Indonesia, Joko Widodo katika ziara yake ya siku mbili Nchini Tanzania.

Waziri Dkt. Tax amesema ziara hiyo ni matokeo ya kazi kubwa anayoifanya Dkt. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya kuimarisha uhusiano kati ya Tanzania na mataifa mengine.

Ziara ya Rais Widodo itakuwa ni ya pili kwa kiongozi wa taifa hilo kutembelea nchini, ya kwanza ilifanywa na Soeharto, Rais wa Pili wa Indonesia, 05 Disemba 1991, miaka 32 iliyopita.
IMG-20230821-WA0382-1536x1023.jpg

Amesema baada ya mapokezi, viongozi hao watakuwa na mazungumzo ya faragha, na baadaye mazungumzo rasmi. Baada ya mazungumzo rasmi, kutakuwa na hafla ya utiaji saini Hati za Makubaliano ya ushirikiano kwenye sekta mbalimbali kama afya, nishati, madini, uchumi wa buluu, ushirikiano wa kimataifa, uhamaji na biashara na kuzungumza na waandishi wa Habari.

Baadaye Rais Widodo atashiriki dhifa ya chakula cha mchana iliyoandaliwa na Rais kwa heshima yake.

Siku hiyohiyo pia, Rais Widodo atatembelea Ofisi ya Ubalozi wa Indonesia uliopo hapa nchini kabla ya kuhitimisha ziara yake na kuondoka nchini.

Waziri Tax amesema “Ziara hii ni matokeo ya kazi kubwa anayoifanya Dkt. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya kuimarisha uhusiano kati ya Tanzania na mataifa mengine.

“Ziara ya Widodo itakuwa ni ziara ya pili kwa kiongozi wa taifa hilo kutembelea nchini. Ziara ya kwanza ilifanywa Soeharto, Rais wa Pili wa Indonesia tarehe 05 Disemba 1991, miaka 32 iliyopita.”

USHIRIKIANO KATI YA TANZANIA NA INDONESIA
Chimbuko la uhusiano kati ya Tazania na Indonesia ni Mkutano wa Bandung uliofanyika mwaka 1955 ambapo nchi nyingi za Afrika na Asia zilikuwa katika utawalu wa kikoloni kwa kipindi hicho.

Kupitia Mkutano huo nchi hizo zilikubaliana kuimarisha ushirikiano ili kujikomboa kutoka katika utawala wa kikoloni, na ulikuwa ndiyo msingi wa kuanzishwa kwa Umoja wa Nchi zisizofungamana na Upande Wowote (Non- Aligned Movement –NAM).

Hivyo, Tanzania na Indonesia zina uhusiano wa muda mrefu na wa kihistoria. Uhusiano huo uliasisiwa na Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Kambarage Nyerere na Rais wa Kwanza wa Indonesia Mheshimiwa Soekarno.

Uhusiano wa kidiplomasia ulianza mwaka 1964, ambapo Indonesia ilifungua Ubalozi wake nchini mwaka 1964 na kuwa miongoni mwa nchi za mwanzo kabisa kufungua Ubalozi wake nchini miaka michache baada ya uhuru. Aidha, Tanzania ilifungua Ubalozi wake nchini Indonesia Agosti, 2022.

Pamoja na kushirikiana katika harakati za ukombozi, tangu kuanzishwa ushirikiano wa kidiplomasia pamekuwepo na mafanikio makubwa ikiwa ni pamoja na;

Uwekezaji: Hadi kufikia mwaka 2023, Indonesia imewekeza nchini miradi ipatayo mitano (5) katika sekta za Kilimo, uzalishaji wa viwandani, ujenzi, n.k.

Kilimo: Mwaka 1996 Indonesia ilianzisha Kituo cha Mafunzo ya Kilimo kwa Wakulima Vijijini (Farmers’ Agriculture and Rural Training Centre-FARTC), kilichopo Mikindo mkoani Morogoro. Kituo hicho kimekuwa kikitoa mafunzo mbalimbali kwa wakulima.

Aidha, kwa kuzingatia kuwa, Indonesia imepiga hatua kubwa katika kilimo cha zao za mchikichi kutokana na kuwa na mbegu bora ya zao hilo, pamoja na teknolojia ya kisasa, ziara ya Mheshimiwa Rais Widodo nchini itapanua wigo wa ushirikiano katika zao la mchikichi utakaowawezesha wakulima wetu za zao hilo kunufaika na mbegu bora ya mchikichi, na hivyo kuwajengea uwezo na kuongeza uzalishaji wa mafuta ya kula.

Ushirikiano wa Kimataifa
Tanzania na Indonesia zina uhusiano wa muda mrefu na wa kihistoria. Katika nyanja za Kimataifa, tangu wakati wa harakati za kujikomboa kutoka katika utawala wa kikoloni kama wanachama wa Umoja wa Nchi zisizofungamana na Upande Wowote (Non- Aligned Movement –NAM) ambapo nchi zote mbili ni mwanachama wa umoja huo hadi leo.
 
Back
Top Bottom