Rais wa IPU, Dkt. Tulia Ackson alivyofungua Mkutano Mkuu wa 149 wa Umoja wa Mabunge Duniani (IPU), Geneva, Uswisi

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Joined
Apr 18, 2017
Posts
3,984
Reaction score
13,760
WhatsApp Image 2024-10-14 at 16.28.40_1843cd71.jpg

Rais wa Umoja wa Mabunge Duniani (IPU) na Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Tulia Ackson, tarehe 14 Oktoba, 2024 amefungua rasmi Mkutano Mkuu wa 149 wa Umoja wa Mabunge Duniani (IPU) uliofanyika katika Kituo cha Kimataifa cha Mikutano (CICG) mjini Geneva, Uswisi.

Mkutano huu unalenga kujadili mada kuu inayohusu “Matumizi ya Sayansi, Teknolojia na Ubunifu kwa ajili ya mustakabali wa Amani na Uendelevu.” Mkutano huu umehudhuriwa na takribani washiriki 1,500 wakiwemo Maspika, Naibu Maspika, Wakuu wa Misafara pamoja na Wabunge. Mkutano unatarajiwa kuhitimishwa tarehe 17 Oktoba, 2024 kwa kutoa maazimio muhimu yatakayolenga kutatua changamoto za kimataifa zinazoikabili dunia kwa sasa.

WhatsApp Image 2024-10-14 at 16.28.39_600658ae.jpg

WhatsApp Image 2024-10-14 at 16.28.39_55c6aff6.jpg
 
Hivi Kila mikutano lazima aende yeye hawezi hata kumkaimisha msaidizi wake? 😂😂
 
Ali-panic sana walipo mhoji kwa nini alikwenda Russia kabla ya Ukraine??

Nadhani alijisahau, alidhani bado anaongea kwenye Bunge la akina Jesca Msavatabangu na Deo Sanga
View attachment 3126211
Huyo mwamba alie msogezea maji ya kunywa hajui hata protokali ndogo ya kushika glass? 😁😁😁😁
 
Mkutano wa Umoja wa Mabunge Duniani unafanyika Geneva, Uswisi. Mkutano ulianza Oktoba 13 na utatamatika Oktoba 17,2024. Huu ni mkutano wa 149.

Mjadala mkuu katika mkutano huo ni kuhusu "Matumizi ya Sayansi,Teknolojia na Ubunifu Kwa ajili ya mustakabali wa Amani na Uendelevu" (Harnessing Science, Technology and Innovation for a More Peaceful and Sustainable future)

Hivyo Rais wa IPU, ambaye ni Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ni nguzo muhimu katika mkutano unaoangazia mustakabali wa akili mnemba(artificial intelligence) katika demokrasia,haki za binadamu pamoja na utawala wa kisheria na hatimaye kuweka mwongozo wa dunia (outcome document).

CamScanner 10-15-2024 12.14.jpg

Mkutano wa IPU unajili baada ya Mkutano wa Umoja wa Mataifa,UN kufanyika mwezi uliopita, Septemba,2024. Mkutano wa UN ulipitisha Mpango wa Mageuzi yaani Mkataba kwa ajili ya Mustakabali wa baadaye wa Dunia(the Pact for the Future).

Mustakabali kuhusu masuala ya tabia nchi,hali ya vita duniani, akili mnemba,ukosefu wa usawa na umasikini.
CamScanner 10-15-2024 13.02.jpg

Hivi ndivyo masuala ya dunia na ulimwengu yanavyojadiliwa Kwa mitazamo mbalimbali na hisia tofauti tofauti. Lengo ni kuifanya dunia kuwa pahala salama pa kuishi pasina kujali rangi ya mtu, itikadi, imani na waishio binadamu. Viva Spika Tulia Ackson.

CamScanner 09-30-2024 04.57_1.jpg
 
Attachments

Tunamsubiri mahakamani kwa nini amfukuze Luhiga Mpina kwa kusema kweli kuwa waziri wa Kilimo Bashe ametoa vibali vya sukari kishikaji wapige hela.

Charity start at home siyo huyo aliyekataa bunge kuzungumzia utekaji na mauaji? Kama nyumbani hawezi kutunza nyumba yake ataweza za jirani? Mnafiki huyo mwakani apewe mbeleko ubunge Mbeya
 
Ali-panic sana walipo mhoji kwa nini alikwenda Russia kabla ya Ukraine??

Nadhani alijisahau, alidhani bado anaongea kwenye Bunge la akina Jesca Msavatabangu na Deo Sanga
View attachment 3126211
Nimrfuatilia issue nzima hapa niseme tu Akson T amejibu vizuri na hakuonesha panic yoyote kwa hili inaonekana kulikuwa na ajenda nyuma ya pazia na usipo tuliza kichwa unashangaa watu wana vote a vote of no konfidensi kwako.

View: https://youtu.be/VQzcl1p-fkE?si=A4Gr_krWjAPS-Csc

Hongera mAdam president of IPU
 
Mkutano wa Umoja wa Mabunge Duniani unafanyika Geneva, Uswisi. Mkutano ulianza Oktoba 13 na utatamatika Oktoba 17,2024. Huu ni mkutano wa 149.

Mjadala mkuu katika mkutano huo ni kuhusu "Matumizi ya Sayansi,Teknolojia na Ubunifu Kwa ajili ya mustakabali wa Amani na Uendelevu" (Harnessing Science, Technology and Innovation for a More Peaceful and Sustainable future)

Hivyo Rais wa IPU, ambaye ni Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ni nguzo muhimu katika mkutano unaoangazia mustakabali wa akili mnemba(artificial intelligence) katika demokrasia,haki za binadamu pamoja na utawala wa kisheria na hatimaye kuweka mwongozo wa dunia (outcome document).

View attachment 3126441

Mkutano wa IPU unajili baada ya Mkutano wa Umoja wa Mataifa,UN kufanyika mwezi uliopita, Septemba,2024. Mkutano wa UN ulipitisha Mpango wa Mageuzi yaani Mkataba kwa ajili ya Mustakabali wa baadaye wa Dunia(the Pact for the Future).

Mustakabali kuhusu masuala ya tabia nchi,hali ya vita duniani, akili mnemba,ukosefu wa usawa na umasikini.
View attachment 3126453

Hivi ndivyo masuala ya dunia na ulimwengu yanavyojadiliwa Kwa mitazamo mbalimbali na hisia tofauti tofauti. Lengo ni kuifanya dunia kuwa pahala salama pa kuishi pasina kujali rangi ya mtu, itikadi, imani na waishio binadamu. Viva Spika Tulia Ackson.

View attachment 3126461
Tulia bonge Moja la Spika. I love You Tulia
 
Nimrfuatilia issue nzima hapa niseme tu Akson T amejibu vizuri na hakuonesha panic yoyote kwa hili inaonekana kulikuwa na ajenda nyuma ya pazia na usipo tuliza kichwa unashangaa watu wana vote a vote of no konfidensi kwako.

View: https://youtu.be/VQzcl1p-fkE?si=A4Gr_krWjAPS-Csc

Hongera mAdam president of IPU

Unampongeza ujinga na wewe ni chawa wake tu. Ndiyo maana hamfiki mbali. Tilia hana skills kwenye masuala ya conflict resolution and diplomacy. Akikubali positive criticism itamjenga lakini siyo sofa za kibwege
 
Back
Top Bottom