Roving Journalist
JF Roving Journalist
- Apr 18, 2017
- 3,984
- 13,760
Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Rais wa Umoja wa Mabunge Duniani (IPU), Dkt. Tulia Ackson, leo tarehe 7 Oktoba, 2024 amekutana na kufanya mazungumzo na Mkuu wa Chuo Kikuu cha Kilimo na Sayansi hai nchini Hungary, Ndg. Gyuricza Csaba katika Makazi ya Kifalme ya Godollo nchini humo ambapo aliongozana na Naibu Spika wa Bunge la Hungary, István JAKAB.
Pamoja na mambo mengine, Viongozi hao wamejadili kuhusu Mashirikiano baina ya Chuo hicho ambacho pia ni kikubwa kwa ukanda wote wa Ulaya ya Kati na Vyuo vya kilimo vilivyopo Tanzania ikiwemo kubadilishana wanafunzi na walimu wa pande zote mbili kwa maana ya Tanzania na Hungary ili kupeana uzoefu wa mafunzo kwa vitendo.
Soma Pia: Dkt. Tulia ataka ushirikiano na mawazo bunifu kuliendeleza Bara la Afrika na watu wake
Hali kadhalika, Viongozi hao wamejadili namna ya kuzalisha mbegu bora zitakazoweza kuhimili athari za mabadiliko ya tabianchi na kufikia hatua ya kuvuna mazao bora yatakayoihakikishia dunia kuwepo kwa jitihada madhubuti za kutunza usalama wa chakula duniani.