Webabu
JF-Expert Member
- Apr 29, 2010
- 8,870
- 14,258
Raisi Isaac Hezrog wa Israel amethibitisha kuwa nchi hiyo haijawahi kupata kipigo na madhara tangu vita vya Yom Kipur isipokuwa mwaka huu wakati wa waziri mkuu Benjamin Netanyahu.
Katika kumfafanua waziri mkuu huyo, Hezrog amesema Netanyahu ameweza kuhimili misukosuko mingi katika kipindi chake cha kisiasa cha miaka 30 lakini safari hii itabidi aondoke kutokana na uzembe mkubwa wa kiusalama uliotokea mwaka huu.
Katika historia yake hiyo amepewa majina mengi kutokana na kuponea kwake chupu chupu kuondoshwa madarakani. Ameitwa king bibi kwa kukaa kwake madarakani kwa muda mrefu. Vile vile ameitwa mwanasiasa mchawi kwa kuweza kupata ushindi wakati dalili zote zikionesha kushindwa.
Hivi karibuni alipewa jina la amani (security). Jina hilo amesema sasa limechanwa chanwa baada ya Hamas kupenya ngome na kuuwa waisrael wengi kuliko kipindi cha kiongozi yeyote nchi hiyo.
Yom Kipur na vita vingine viliuwa watu lakini ilikuwa ni vita vilivyojulikana viko karibu kutokea kutokana na kusoma harakati za adui. Hili shambulio la Hamas halijapata kutokea na wala kufikirika.