Rais wa Ivory Coast amteua kaka yake kuwa Naibu Waziri Mkuu

Rais wa Ivory Coast amteua kaka yake kuwa Naibu Waziri Mkuu

Richer

JF-Expert Member
Joined
Jun 9, 2025
Posts
2,318
Reaction score
4,079
Rais wa Ivory Coast, Alassane Ouattara, ametangaza mabadiliko ya Baraza la Mawaziri, hatua inayoashiria mwendelezo wa uongozi baada ya ushindi wake mkubwa katika uchaguzi uliofanyika Oktoba 2025. Mabadiliko makubwa zaidi ni uteuzi wa ndugu yake, Waziri wa Ulinzi Tene Birahima Ouattara, kuwa Naibu Waziri Mkuu, wadhifa mpya ambao atauhudumu sambamba na nafasi yake ya ulinzi.

Mabadiliko hayo yanakuja miezi mitatu baada ya Ouattara kuchaguliwa tena kwa muhula wa nne kwa karibu asilimia 90 ya kura, na kufuatia uchaguzi wa Bunge wa Desemba 2025, ambapo chama chake tawala cha RHDP kilipata takribani asilimia 80 ya viti vya ubunge.

Kupandishwa kwa Tene Birahima Ouattara kunamweka ndugu mdogo wa rais juu zaidi katika ngazi ya uongozi wa serikali, na kuongeza ushawishi wake huku wizara muhimu zikiendelea kama zilivyo. Kwa mujibu wa Ikulu, hatua hiyo inaakisi nia ya serikali kuendeleza utawala thabiti kwa kuzingatia dhamira waliyopewa na wananchi kupitia sanduku la kura.

Waziri Mkuu wa zamani, Patrick Achi, ameteuliwa kuwa Spika wa Bunge, wakati Makamu wa Rais Tiemoko Meyliet Kone, mwenye umri wa miaka 84, ameendelea kubaki katika nafasi yake.

Rais Ouattara, mwenye umri wa miaka 84 na aliyewahi kuwa Naibu Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Fedha la Kimataifa (IMF), ameiongoza Ivory Coast tangu mwaka 2011. Amesema dhamira yake ni kuweka mazingira mazuri kwa kizazi kipya cha viongozi wa kisiasa.

1769403368004.png


1769403214210.png

============

Ivory Coast President Alassane Ouattara reshuffled his cabinet on Friday, maintaining most senior ministers while appointing his brother, Defence Minister Tene Birahima Ouattara, to the newly created role of vice prime minister, which he will hold alongside his defence portfolio.

The move elevates the younger Ouattara within the government hierarchy, while most key portfolios remained unchanged, signaling continuity rather than a comprehensive overhaul.

The reshuffle follows Ouattara's re-election in October and his party's victory in December's legislative elections, securing a parliamentary majority.

Ouattara, 84, a former deputy managing director of the International Monetary Fund, has led the country since 2011 and has said that he intends to prepare the ground for a new generation of political leaders during his tenure.

Source: Reuters & African news
 
"The gravest mistake that will never be pardoned is to allow the black man to rule."
🖕The former South African president during the apartheid era the late P.W. Botha.
 
Kam vipi turudi kwenye utemi, wanagwa wanakuwa ni wanafamilia wa karibu.
 
Back
Top Bottom