Kenya vyama ni vya watu mahsusi hivyo ata hakuna haja ya ugombezi rasmi.
Mathalani, kwa chama cha ODM, kiongozi wa chama ndiye anayekuwa mgombea urais moja kwa moja, Raila Odinga.
Wiper, kiongozi wa chama, Kalonzo Musyoka ndiye mgombea moja kwa moja, hakuna mtu anayeweza kugombea nae.
UDF, kiongozi wa chama Musalia Mudavadi ndiye mgombea urais rasmi wa urais
TNA kilikuwa cha Uhuru na URP kilikuwa cha Rutto.Na kuelekea 2017 hivi viwili vimeungana hivyo kutakuwa na Jubilee Alliance ambayo mgombea wa 2017 ni Uhuru Kenyatta na mgombea wa 2022 ni Rutto.
Hivyo demokrasia ya uchaguzi ndani ya vyama kwa Kenya haipo.Kinachotokea ni kuwa hivi vyama vinaweza kuungana kutoa mgombea mmoja, ambapo vinara wa vyama hivyo wanakubaliana nani kati yao awe mgombea urais.
Mwaka 2013 Raila na Kalonzo waligombea pamoja sawa na Kenyatta na Rutto walivyokubaliana.Wanacha wa vyama hawana sauti juu ya hayo.
Hii inafanyika pia kwa sababu kura za maeneo mbalimbali ya Kenya zinamtegemea mtu mmoja, ukitaka kura za mkoa wa zamani wa Nyanza kwa wajaluo lazima uwe na Raila maana wajaluo wanampigia kura mtu atakayesema Raila wampigie.
Rift Valley kwa chaguzi mbili zilizopita wameonyesha wanampigia kura mtu ambaye Rutto anasema wampigie, kama wakamba wanavyomsikiliza Kalonzo Musyoka na wakikukuyu kwa mkikuyu mwenzao(kwa sasa Uhuru Kenyatta).
Kwenye uchaguzi uliopita wapoga kura wa eneo la Wakikuyu kwa Uhuru na eneo la Rutto la Rift Valley walikuwa wanafika asilimia 45% ya wapiga kura wote, hivyo kuwahakikishia ushindi ata kabla ya uchaguzi.