Mkalukungone Mwamba
JF-Expert Member
- Aug 29, 2022
- 3,141
- 7,205
Rais wa Madagascar, Andry Rajoelina, ameondolewa madarakani kupitia kura ya bunge iliyopitishwa kwa kishindo.
Katika kura hizo, wabunge 130 waliunga mkono hoja ya kumng’atua, huku kura moja ikiwa tupu.
Hatua hii imejiri saa chache baada ya Rajoelina kulivunja bunge na kukimbia nchi kufuatia maandamano ya vijana wanaolalamikia ukosefu wa maji, umeme, na tuhuma za ufisadi.
Soma Pia: Rais wa Madagascar avunja Bunge baada ya kukimbia nchi, Upinzani wadai si halali kisheria
Hata hivyo, ikulu imepinga hatua hiyo ikidai ni kinyume cha katiba, huku hali ya kisiasa ikizidi kuwa tete.
Kikosi maalum cha jeshi, Capsat, kimetangaza kuchukua mamlaka na kusitisha katiba, kikiahidi kuunda serikali ya mpito ya kiraia.
Mahakama ya Katiba inatarajiwa kutoa uamuzi kuhusu uhalali wa hatua hiyo katika siku chache zijazo.