Rais Andry Rajoelina anayekabiliwa na upinzani mkali nchini Madagascar ametangaza kulivunja Bunge la Taifa mara moja
Hatua hiyo imekuja muda mfupi baada ya upinzani kutangaza kuwa utaanzisha mchakato wa kumng’oa madarakani kwa madai ya “kuacha wadhifa wake na kukimbia wajibu wake wa kazi”
Awali, kupitia matangazo ya moja kwa moja kwenye Mtandao wa Facebook, Rajoelina alisema amelazimika kukimbilia katika eneo salama baada ya jaribio la kumuua, kufuatia wiki kadhaa za maandamano makubwa yaliyokuwa yakimtaka ajiuzulu
Hata hivyo, hakuthibitisha ripoti zilizoenea kwamba alitoroka nchini humo kwa ndege ya kijeshi ya Ufaransa Wakati huo huo, kikosi chenye nguvu cha jeshi kimetangaza kuunga mkono waandamanaji wanaomtaka Rais Rajoelina aachie madaraka. Jumapili iliyopita, rais huyo alidai kulikuwa na jaribio la kumpindua kinyume cha sheria
Lakini sasa hali imezidi kuwa tata baada ya kiongozi wa upinzani bungeni, Siteny Randrianasoloniaiko, kusema kuwa tamko la rais la kulivunja bunge si halali kisheria. Akizungumza na shirika la habari la Reuters, Siteny alisema: “Agizo hili halina uhalali wa kisheria Spika wa Bunge la Taifa hakupewa taarifa wala kushauriwa kabla ya uamuzi huo kufanyika.”
Hatua hii imezua sintofahamu zaidi kuhusu mustakabali wa kisiasa wa Madagascar, taifa ambalo limekuwa likikumbwa na maandamano, mivutano ya kisiasa, na shinikizo la ndani na nje kumtaka Rajoelina kuachia madaraka
------------------
Upinzani Wapanga Kumuondoa Rais Rajoelina Madarakani kwa Kosa la 'kukimbia wajibu wa kazi
Chanzo kutoka chama kikuu cha upinzani nchini Madagascar, Tiako i Madagasikara (TIM), kimedokeza kuwa chama hicho kinapanga kuanzisha mchakato wa kumng’oa madarakani Rais Andry Rajoelina, kikimtuhumu kwa kosa la “kuacha wajibu wa kazi
Kwa mujibu wa chanzo hicho, chama cha TIM kinaamini kuwa Rajoelina alisafirishwa nje ya nchi kwa ndege ya kijeshi ya Ufaransa, taarifa ambazo kwa mara ya kwanza ziliripotiwa na shirika la utangazaji la Kifaransa, RFI
TIM, kinachoongozwa na rais wa zamani Marc Ravalomanana, ndiye aliyepinduliwa kupitia mapinduzi ya wananchi mwaka 2009, hatua iliyomuwezesha Rajoelina kuchukua madaraka kwa mara ya kwanza
Hatua ya kupanga hoja ya kumng’oa madarakani Rajoelina imekuja wakati taifa hilo la kisiwa linaendelea kukabiliwa na mivutano ya kisiasa na kijeshi, kufuatia maandamano yanayoongozwa na vijana na wanajeshi wanaomtaka rais huyo ajiuzulu rasmi au kurejea nchini kutoa maelezo ya wazi kuhusu hali yake.
-----------------
Taarifa za Rais wa Madagascar kuondoka nchini kimya kimya Kufuatia Maandamano yanayoendelea yakimshinikiza kujiuzulu
Shirika la Habari la BBC linaendelea kufuatilia Taarifa za kuondoka nchini kwa Rais wa Madagascar, Andry Rajoelina, suala lililoibua maswali mengi baada ya Waziri wa Usalama wa Umma, Mandimbin'ny Aina Randriambelo kusema kuwa hakujulikani alipo kwa sasa akizungumza na shirika la habari la ReutersRajoelina hajaonekana hadharani tangu wiki iliyopita ingawa taarifa za awali zilidai kuwa anatarajiwa kuilihutubia taifa Jumatatu hii Oktoba 13, 2025
Kutoweka kwake kunakuja wakati ambapo anakabiliwa na shinikizo kubwa la kisiasa, kufuatia wanajeshi wa kikosi cha CAPSAT kujiunga na waandamanaji wanaomtaka ajiuzulu. Hatua hiyo imeonekana kama pigo kubwa kwa juhudi zake za kushikilia madaraka
Kuna taarifa zinazokinzana kuhusu mahali alipo kiongozi huyo. Shirika la utangazaji la Ufaransa, RFI limeeleza kuwa Rais Rajoelina alisafirishwa nje ya nchi Jumapili kwa kutumia ndege ya kijeshi ya Ufaransa
Kwa mujibu wa RFI, helikopta ilimpeleka kwanza kwenye Kisiwa cha Sainte-Marie kilicho katika pwani ya mashariki ya Madagascar, ambako alikwea ndege hiyo ya kijeshi.
Baadhi ya vyanzo vinanukuliwa na RFI vikidai kuwa Rajoelina huenda aliendelea na safari kuelekea Dubai katika Falme za Kiarabu, kupitia nchi ya Mauritius
RFI imeongeza kuwa Rais wa Ufaransa, Emmanuel Macron, ndiye aliyeruhusu operesheni ya kumhamisha Rajoelina kwa usalama
Hata hivyo, serikali ya Ufaransa imesisitiza kuwa haitaingilia kijeshi katika mzozo wa kisiasa unaoendelea Madagascar, ikisisitiza kuwa hatua yoyote iliyochukuliwa ni ya kibinadamu na inalenga kulinda maisha ya watu
Wakati huu, wananchi wa Madagascar wanasubiri kwa hamu hotuba ambayo Rajoelina alitarajiwa kutoa Jumatatu, huku taifa likiwa katika hali ya sintofahamu kuhusu uongozi na mustakabali wa kisiasa wa nchi hiyo
Kiongozi wa upinzani nchini Madagascar, Siteny Randrianasoloniaiko, ameiambia shirika la habari la Reuters kwamba Rais Andry Rajoelina ameondoka nchini, ingawa haijulikani alikoelekea
“Rais ameondoka nchini. Tulizungumza na watumishi wa ikulu na wamethibitisha kuwa aliondoka Jumapili,”* alisema Randrianasoloniaiko, akinukuliwa na Reuters
========
President's decree to dissolve parliament not valid, opposition says
The leader of the opposition in parliament has said President Andry Rajoelina's decree to dissolve the national assembly - the lower house of parliament - is "not legally valid", Reuters news agency is reporting.
"This decree is not legally valid... the president of the national assembly says he was not consulted," Siteny Randrianasoloniaiko is quoted as saying
Madagascar's embattled president dissolves national assembly
Moments ago, Madagascar's embattled President Andry Rajoelina said he has dissolved the national assembly - the lower house of parliament - with immediate effect.
This came after the opposition said it would start impeachment proceedings against him in parliament for "abandonment of post".
Rajoelina had earlier said in a live broadcast to the nation on Facebook that he was forced to shelter in a "safe place" after an attempt on his life, following weeks of protests calling for him to quit.
He did not confirm reports that he had fled Madagascar on a French military aircraft.
A powerful military unit has thrown its weight behind protesters demanding his resignation.
On Sunday, Rajoelina said there was an attempt to seize power illegally.
--------------
Move to impeach president for 'abandonment of post'
A source in the biggest opposition party in Madagascar has told me they are planning to impeach President Andry Rajoelina for "abandonment of post."
The source from TIM party said they believe he has been flown out of the country in a French aircraft - something that French public broadcaster RFI first reported.
TIM is led by ex-President Marc Ravalomana, who was ousted in a popular uprising in 2009, leading to Rajoelina taking power
Opposition says president has fled country - Reuters
An opposition leader has told the Reuters news agency that President Andry Rajoelina has left Madagascar, but that his final destination is not known."The president left the country, we called the staff of the presidency and they confirmed that he left the country" on Sunday, Siteny Randrianasoloniaiko is quoted as saying.
It follows reports by the French-language broadcaster RFI that Rajoelina had been airlifted from Madagascar on Sunday in a French military plane
------------
Rajoelina may have headed to Dubai - report
French broadcaster RFI is also reporting that on Sunday, a helicopter took the Malagasy president to Sainte-Marie Island, on Madagascar's east coast, and from there, he boarded a French military aircraft
President Rajoelina may have then headed for Dubai in the United Arab Emirates via Mauritius, RFI says
The broadcaster adds that, according to sources close to the matter, French President Emmanuel Macron authorised Rajoelina's evacuation
However, the government in Paris has stated that it will not intervene militarily in the situation in Madagascar
--------------
President Rajoelina flown out of the country by France - report
There has been much speculation about President Andry Rajoelina's location - now French broadcaster RFI has reported that the leader was flown out of the country on a French military plane on Sunday.
RFI has not yet said where Rajoelina landed
---------------
President's whereabouts not known - minister
The whereabouts of Madagascar's President Andry Rajoelina are unknown, Public Security Minister Mandimbin'ny Aina Randriambelo has told Reuters news agency
Rajoelina has not been seen in public since last week, but he is due to address the nation later on Monday
He faced a major blow in his attempt to hang to power when a powerful military unit threw its weight behind protesters demanding his resignation
Source: BBC