ukwaju_wa_ kitambo
Senior Member
- Sep 15, 2024
- 150
- 173
Hamad Ally a.k.a madee msanii wa Bongo fleva , moja kati ya wasanii wa Bongo fleva waliokuwa wanaunda kundi la Muziki linaitwa " Tip top connection" , kundi la muziki lililokuwa linaundwa na wasanii kama Vile...MB Dog, Z-Anto, Keisha,
Pingu, Spark, Dongo Janja ,madee,Cassim Mganga, Tuma man & madee.
Chini ya Usimamizi wa meneja & mwanzilishi wa kundi hilo marehem " Abdul shabani Tale Tale" jina maarufu " Abdu Bonge" .. ambae alitangulia mbele za haki mwaka 2015.
Na kundi hilo kubaki chini ya mdogo wake na "Abdu Bonge" anaitwa "Hamisi Shaban Taletale jina maarufu " Babu Tale ". Ambae ni meneja wa Tip top connection..
Tip Top Connection ni moja kati ya makundi yaliyopitia misuko suko ya wasanii wake kutoka wengi tena kwa kipindi kimoja,kama utavuta kumbukumbu vizuri mwishoni mwa mwaka 2009 haukuwa mwaka mzuri kwao maana ilipoteza zaidi ya nusu ya wasanii wake waliondoka katika kundi hilo. Wasanii waliotoka Tip Top kipindi kimoja ni pamoja na Keisha,Z anto,Spack,Pingu,Mb Dogg ..
Raisi wa manzese Hamad Ally a.k.a madee alifanikiwa kutoa Album iliyojulikana kwa jina la "Kazi yake Mola" miaka ya 2000.
Album ya madee "kazi yake mola" ikiwa chini ya Usimamizi na usambazaji wa kazi za wasanii " King Brothers stores" pamoja n G project .
Album hii ilikuwa ina nyimbo hizi kama ifuatavyo:.
Side A.
1. Kazi yake mola ( madee ft mandojo & domokaya.
2. Pete ( madee ft doctor k.)
3. Msanii ( madee ft t.i.d)
4. Chini ya jua ( mdee)
5. Nakata Roho ( instrumental)
Side B.
1. Safari sio kifo ( madee)
2. Nakata Roho ( madee)
3. Mpenzi sikia ( madee ft shalow)
4. Safari sio kifo Rmx ( madee ft Albert mangwea & Dully Sykes)
5. Msanii ( madee ft t.i.d)
Raisi wa manzese madee Unapowazungumzia wasanii ambao ni vijana ambao wametumia vizuri vipaji vyao kujiweka sawa kimuziki na kimaisha, huyu hawezi kukosa katika orodha yako. Kwanza kile kitendo cha kudumu katika top ten kwa muda aliokaa, ni jambo la kujivunia kabisa, kwa sababu wanamuziki wengi walioibuka pamoja naye, wamekwama.
Moja kati ya vitu vikubwa ambavyo aliwahi kuvifanya Madee, ni kumleta Dogo Janja ‘Janjaro’ jukwaani akiwa bado mdogo kabisa. Ni wasanii wachache wenye vipaji pia vya kugundua uwezo wa wengine katika kufanya kazi hiyo, kwani licha ya kuwa yeye ni mkazi wa Dar es Salaam, aliweza kuuona uwezo wa Janjaro alipokwenda Arusha, licha ya jiji hilo kuwa na wasanii wengi katika historia ya Bongo Fleva.
Ameshafanya nyimbo nyingi zilizofanya vizuri ndani na nje. Lakini hata hivyo, baadhi ya vibao vilivyovuma sana ni pamoja na kile cha Nani Kamwaga Pombe Yangu, ambacho licha ya kuwa ni kimekaa kikatuni, lakini kinatoa ujumbe na kuchezeka.
#funguka
Je? Ni nyimbo ipi? Bora kwa upande wako kutoka kwa msanii huyu hamad Ally a.k.a madee.
Kwa upande wangu hii top 3 bora kutoka kwa madee Raisi wa manzese.
1. Yote maisha
2. Kazi yake mola
3. Historia
Ukwaju wa kitambo
0767 542 202