ward41
JF-Expert Member
- Apr 3, 2022
- 749
- 2,533
Kuna uzushi mwingi wa vijiweni kwamba raisi wa MAREKANI anapatikana na deep state na kwamba kuna kikundi kidogo cha watu sirini wanamteua raisi. Hii sio kweli.
Raisi wa MAREKANI anapatikana kwa kura za Wananchi. Ndiyo maana wagombea wanafanya campaign ili wapigiwe kura
Utofauti na huku kwetu ni kwamba raisi wa MAREKANI anapatikana kwa njia ya points (electoral votes).
Jimbo husika linapewa points (electoral votes) na mgombea atakaeshinda kura za Jimbo husika anapewa tu point zote za jimbo husika. Na majimbo yana point tofauti Tofauti. Majimbo yenye idadi kubwa ya watu yana point nyingi na idadi ndogo yamepewa point chache.
Kuna mfanano Fulani na mpira wa mguu ( soccer) . Team inaweza shinda magoli mengi lakini point ni 3. Na team ikashinda goli moja bado point zikawa zilezile 3.
Sasa kwenye mpira team inaweza pia ikachukuwa Ubingwa labda wa ligi kwa magoli machache ikiwa ili maintain ushindi kwa kila mechi japo mwembamba. Team vilevile inaweza ikapoteza Ubingwa licha ya kuwa na magoli mengi kwenye ligi iwapo haikumantain ushindi kwa kila mechi licha ya kufunga magoli mengi kwenye mechi zake za ushindi
Kwa mfano, team A imecheza mechi 10 na zote imeshinda kwa magoli jumla 13, point 30
Team B imecheza mechi 10, imeshinda mechi 7 na kufungwa mechi tatu lakini mechi zake za ushindi ilikuwa inafunga 4, 3, 5, 4 hatimaye kupata magoli mengi na point chache. Team B licha ya kuwa na magoli mengi imepoteza Ubingwa kwa sababu mshindi anapatikana kwa point.
Uchaguzi wa MAREKANI umefanana Sana na huo mfano.
Mgombea anaweza kupata kura majimbo yenye idadi kubwa ya wapiga kura, lakini yakawa majimbo machache, Uwezekano wa kukosa uraisi unakuwa mkubwa. Inatakiwa kwenye majimbo 50 (50 states) U maintain ushindi kwenye majimbo mengi bila kusahau majimbo yenye point nyingi kama Ohio, California, Texas nk. Ukiweza hilo unazoa point nyingi (electoral votes) hatimaye kuibuka mshindi.
Mwaka 2016, Hillary Clinton alipata kura nyingi za Wananchi kwa sababu Alishinda tu majimbo yaliyo machache yenye idadi kubwa ya wapiga kura bila kuzingatia kupata ushindi wa majimbo mengi. Ni sawa na team imecheza mechi 10, ushindi mechi 7, kufungwa 3 lakini ushindi wako ulikuwa na magoli mengi. Ilikuwa unafunga 5, 4, 3, nk.
Mwingine ameshinda mechi zote lakini kwa goli moja, mbili wastani. Kwa sababu ana mechi nyingi za ushindi, atakuwa bingwa.
Kwa hiyo kuna Mambo mengi ya kuzingatia ili mgombea ashinde uchaguzi wa uraisi MAREKANI