Rais wa Marekani humuapisha mkuu wa majeshi ya Marekani tu!

Yoda

JF-Expert Member
Joined
Jul 22, 2018
Posts
64,960
Reaction score
111,265
Tofauti na marais wengi duniani ambao huwaapisha kiapo cha utumishi maafisa na watumishi lukuki wa serikali na mihimili mingine ya nchi, rais wa Marekani kiutamaduni yeye huwa anamuapisha mkuu wa majeshi ya Marekani/mwenyekiti wa kamandi za jeshi la Marekani tu.

Mawaziri na watumishi katika vyeo vingine vikubwa huwapishwa na makamu wa rais, jaji mkuu na majaji wengine wote wanapishana wenyewe na wanajeshi pia huwa wanaapishana wenyewe kwa wadogo kuapa kwa wenye vyeo vya juu yao.

Katika kiapo chao pia huwa hakuna kipengele cha kutokutoa siri ila siri za usalama wa taifa huwa zinatunzwa sana!
 
Utaratibu wao umekaa vyema sana. Marekani wanakula kiapo cha maadili na utii wa Katiba na kwa nchi, wakati nchi nyingine wanakula viapo vya utii kwa marais.

"I, Yoda do solemnly swear that I will support and defend the Constitution of the United States against all enemies, foreign and domestic; that I will bear true faith and allegiance to the same; that I take this obligation freely, without any mental reservation or purpose of evasion; and that I will well and faithfully discharge the duties of the office on which I am about to enter. So help me God."

Kwa kiapo hicho utaapishwa na msimam8zivwa viapo au supervisor wako au mwingine yeyote, siyo rais. Wengine endeleeni na utii kwa marais
 
Pia huko wanaume wanaolewa, unasemaje kaka zako tupokee mahali kwa ajili Yako?!!!
 
Hebu weka chanzo au vyanzo vya hayo madai yako kwamba Rais wa Marekani humwapisha tu mkuu wa majeshi ya Marekani….
 
Hebu weka chanzo au vyanzo vya hayo madai yako kwamba Rais wa Marekani humwapisha tu mkuu wa majeshi ya Marekani….
Oh, majirani tafuteni shuka tuje kimstiri mtu mzima mwenzetu Huku........anaenda kuumbuka🤣🤣🤣🤣🤣
 
Habari kwamba Rais wa Marekani humwapisha tu chairman of the joint chiefs of staff chanzo chake ni nini/ kipi?
 
Hiyo ni Marekani, so what?
 
Reactions: Lax
Nani anawachagua hao watu?
 
Habari kwamba Rais wa Marekani humwapisha tu chairman of the joint chiefs of staff chanzo chake ni nini/ kipi?
1. The U.S. Constitution (Article II, Section 1, Clause 8).

2. Federal law (5 U.S.C. § 3331).

3. The Constitution (Article II, Section 2, Clause 2)

Hizo zote zinaelezea kuhusiana na viapo, lakini pia hazimu assign rais kuapisha the apointed federal officials.

Nimepongeza utaratibu huo, based on historical records ambazo hata kwa records ambazo ninazokumbuka, najua hata Chairman of the joint Chief of Staff huwa anaapishwa na Secretary of defense, not the president.

Ukiangalia vyema my reoly utaona nilichoelezea na nilichokilenga...UTARATIBU.
 
Hahahaa!

Vizuri umekubali kuwa Secretary of Defense ndo mwenye mamlaka ya kisheria ya kumwapisha Chairman of the Joint Chiefs of Staff na siyo rais, kama vile ambavyo mwanzisha mada alivyodai.

Watu ni waongo sana.

Jamaa kajitungia tu mambo kichwani mwake na kuja kupotosha hapa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…