Kinyungu
JF-Expert Member
- Apr 6, 2008
- 19,484
- 38,416
Leo Rais Biden wa USA ameanguka jukwaani wakati akisalimiana na Wahitimu wa chuo cha kijeshi cha Anga huko Colorado, chanzo cha kuanguka hakijulikani kama amejikwaa au ni umri mkubwa kiasi kwamba anapoteza balance. Mara baada ya kuanguka maafisa wa usalama wamemsaidia kuinuka fasta na kumpeleka sehemu ya kukaa. Jionee mwenyewe jinsi alivyoanguka
My take: Biden amezeeka sana asigombee tena urais Mwakani. Atafia jukwaani huyu
=========
Bwana Biden, ambaye ni Rais mwenye umri mkubwa zaidi nchini akiwa na miaka 80, alisaidiwa kuinuka na kuonekana kuwa salama baada ya kuanguka alipokuwa akirejea kwenye kukaa baada ya kuhutubia kwenye Mahafali ya Chuo cha Kijeshi cha Anga huko Colorado (US Air Force Graduation Ceremony).
Alionekana akirudi kiti chake bila msaada na baadaye akakimbia kurudi kwenye msafara wake wa magari baada ya sherehe kumalizika muda mfupi baada ya tukio hilo.
Ripoti ya kikundi cha waandishi wa habari wa Ikulu ya White House ilisema awali kwamba Bwana Biden alijikwaa kwenye mifuko miwili nyeusi ya mchanga alipokuwa akitoka jukwaani. Mwandishi wa kikundi hicho aliongeza kuwa Rais hakujibu maswali aliporejea kwenye ndege yake.
Msemaji wa vyombo vya habari vya Ikulu ya White House, Karine Jean-Pierre, alisema Bwana Biden alikuwa "Vizuri kabisa" na alipanda ndege huku akionyesha "Tabasamu kubwa".
"Nilitegwa na mchanga," alidokeza Biden akiwa na tabasamu kwa waandishi wa habari alipofika nyumbani katika Ikulu ya White House siku hiyo jioni.
Mkurugenzi wa mawasiliano wa Ikulu ya White House alisema awali "Rais yuko sawa".
Wakosoaji wamesema kwamba Bwana Biden ni mzee sana kuwania muhula wa pili kama Rais.
Uchunguzi wa hivi karibuni unaonyesha kuwa wapiga kura wengi nchini Marekani wanahofia umri wake mkubwa. Atakuwa na umri wa miaka 82 mwanzoni mwa muhula wake wa pili ikiwa atashinda.
Kujikwaa huko, pamoja na misukosuko ya awali kama kuporomoka kutoka kwenye baiskeli yake na kupanda ngazi za Air Force One, inaweza kuongeza wasiwasi huo.
BBC