Rais wa Marekani, Joe Biden ajikwaa na kuanguka katika hafla ya Colorado

Rais wa Marekani, Joe Biden ajikwaa na kuanguka katika hafla ya Colorado

Na asirudie kabisa kutulazimisha mambo yake, hiyo ni intro akirudia tena.....siku akianguka haamki😁
 
Marais wengi tu wanapata hekaheka kama hizo ila haziwezi kutangazwa sembuse hata kupigwa picha kwa sababu ya asili ya tawala zenyewe maanake ni za kiimla vibaya.

Hii tunaonyeshwa kwa sababu ya asili ya nchi husika lkn kwa nchi zingine kama Russia, China, Iran, North Korea, Cuba, Syria, Belarus na nchi karibu zote za kiafrika, huwezi kuona kitu kama hicho kwa sababu watawala wanaonekana kama miungu watu.
 
Acha bhna huyu salva si ndio rais wa sudan kusini
Mugabe issue yake tofauti na Rais wa South Sudan Salva
Alijikojolea akiwa amesimama wakati wimbo wa Taifa unaimbwa.

Hivi hukuona hiyo Mkuu
Mbona ilikuwa aibu ya mwaka na mkojo unatiririka mpaka chini huku akiangalia kwa mshangao masikini

Nilimhurumia ingawa kama ni ugonjwa ilibidi awe na mfuko wa kuhifadhi mkojo
 
Rais wa Marekani Joe Biden amejikwaa na kuanguka alipokuwa akikabidhi cheti cha diploma katika sherehe ya kuhitimu kwa Chuo cha Jeshi la Wanahewa la Marekani huko Colorado.

Biden, ambaye ndiye Rais mkongwe zaidi wa taifa hilo anayehudumu akiwa na umri wa miaka 80, alisaidiwa kusimama na alionekana kuwa hajadhurika.

Rais alikuwa amesimama kwa takriban saa moja na nusu kupeana mikono na kila mmoja wa wanafunzi 921 waliohitimu.

Awali, Mkurugenzi wa mawasiliano wa Ikulu ya White House alisema kuwa "yuko sawa".

Kulikuwa na mfuko wa mchanga kwenye jukwaa alipokuwa akipeana mikono," Ben LaBolt aliandika kwenye Twitter baada ya kuanguka siku ya Alhamisi.

"Nilipata mchanga," Rais huyo aliyetabasamu alitania waandishi wa habari alipokuwa akirejea Ikulu jioni hiyo. Ripoti ya waandishi wa habari wa Ikulu ya White House hapo awali ilisema Bw Biden alijikwaa kwenye mfuko mweusi wa mchanga alipokuwa akipanda jukwaani.

Picha za tukio hilo zinaonyesha Bw Biden akionekana kuelekeza moja ya mifuko miwili ya mchanga iliyotumiwa kuinua kifaa chake cha teleprompta huku akisaidiwa na afisa wa Jeshi la Wanahewa na washiriki wawili wa huduma yake ya siri.

Alionekana akirudi kwenye kiti chake bila kusaidiwa na baadaye akikimbia kurudi kwenye msafara wake sherehe ilipokamilika muda mfupi baada ya ajali hiyo.

View attachment 2643152

Mwandishi huyo aliongeza kuwa Rais hakujibu maswali aliporejea kwenye ndege yake. Katibu wa waandishi wa habari wa Ikulu ya White House, Karine Jean-Pierre alisema Bw Biden alikuwa akijihisi "mwenye afya kabisa" na alipanda ndege hiyo akiwa na "tabasamu kubwa".

Wakosoaji wamesema Bw Biden ni mzee sana kuwania muhula wa pili kama Rais.

Kura za hivi majuzi zinaonyesha kuwa wapiga kura wengi wa Marekani wana wasiwasi kuhusu umri wake mkubwa. Atakuwa na umri wa miaka 82 mwanzoni mwa muhula wa pili ikiwa atashinda.

Kuanguka huku, pamoja na kujikwaa hapo awali kutoka kwa baiskeli yake na njiani akipanda ngazi za Air Force One, kunaweza kuongeza wasiwasi huo.

Rais wa zamani wa Marekani Donald Trump, mtangulizi wa chama cha Republican atachuana na Bw Biden katika uchaguzi wa Ikulu ya Marekani 2024, na alizungumza juu ya kisa hicho kutoka kwa hafla ya kampeni huko Iowa, akisema "mambo yote ni balaa tupu".
Mara ya pili hii alishaangukaga na baiskeli anaiga hili jitu👇🏻👇🏻👇🏻
 

Attachments

  • Screenshot_20230602-172028_Google.jpg
    Screenshot_20230602-172028_Google.jpg
    265 KB · Views: 2
  • Screenshot_20230602-171934_Google.jpg
    Screenshot_20230602-171934_Google.jpg
    138.4 KB · Views: 3
[emoji1] Mugabe alipoanguka aliwafukuza kazi walinzi wote

Salva Kiir nae alipojikojolea mpaka waandishi wa Habari walikula shaba
Walipigwa risasi hao waandishi?

Na alijikojolea kwa sababu ya ugonjwa wa tezi dume au umri mkubwa?
 
Apumzike tu,asije siku kujamba au kujisaidia hadharani.
Umri haudanganyi.
 
Mugabe issue yake tofauti na Rais wa South Sudan Salva
Alijikojolea akiwa amesimama wakati wimbo wa Taifa unaimbwa.

Hivi hukuona hiyo Mkuu
Mbona ilikuwa aibu ya mwaka na mkojo unatiririka mpaka chini huku akiangalia kwa mshangao masikini

Nilimhurumia ingawa kama ni ugonjwa ilibidi awe na mfuko wa kuhifadhi mkojo
Nakumbuka sasa ndio nimeshangaa uliposema kuwa kumbe aliwapiga shaba wale waandishi wa habari aisee..
 
Nakumbuka sasa ndio nimeshangaa uliposema kuwa kumbe aliwapiga shaba wale waandishi wa habari aisee..
Haswa, bora umekumbuka tukio
Wale wote waliorekodi live wengi wao waliuwawa nasikia na wengine wako jela

Eti kwanini warekodi Rais anajikojolea na kuachia live kwenye TV?
Africa tuna shida sana Mkuu
Hapo Biden kaanguka mbona hawakumdaka mpaka chini ndio wamemnyanyua
 
Huyu Mzee apumzike tu nahisi muula wa pili hatorudi
 
Haswa, bora umekumbuka tukio
Wale wote waliorekodi live wengi wao waliuwawa nasikia na wengine wako jela

Eti kwanini warekodi Rais anajikojolea na kuachia live kwenye TV?
Africa tuna shida sana Mkuu
Hapo Biden kaanguka mbona hawakumdaka mpaka chini ndio wamemnyanyua
Daaah kumbe yule mzee nae mshenzi
 
Kuna mwamba ana tabasam Raisi kupiga mweleka ingekua bongo kazi anayo
 
Back
Top Bottom