jeshi halina madaraka ya kuongoza nchi, ni viongozi wa kiraia na jeshi letu liko chini ya Raia. Kama tuna viongozi wa kiraia ambao tumewachagua na ambao wanavuruga tumaini letu ni sanduku la kura 2010! Jeshi lazima litii mamlaka ya Kiraia na hakuna mahali popote ambapo wanapewa madaraka ya kuchukua madaraka ya kiraia au hata kuangalia halisia. Wanajukumu ambalo liko very clear na nje ya hapo ni kwenda nje ya wajibu wao.
Hata hivyo siko naive kiasi cha kutoelewa ulazima wa Jeshi kuingilia kati utawala wa kiraia. Nina amini kuna mazingira ya nadra sana na ya lazima sana ambapo Jeshi la Wananchi linapotakiwa kuingilia utawala wa kisiasa. Na mazingira hayo kwa sasa Tanzania hayapo.
a. Wakati mtawala wa Kiraia anapohabaribu mchakato na matokeo ya kura na hivyo kulazimisha kuendelea kukaa madarakani. Jeshi linawajibika kuirudisha nchi kwa utawala halali wa kiraia. Mfano, Comoro.
b. Utawala wa kiraia unapoanza kuandika na kutekeleza sheria za kibaguzi ambazo zinawafanya wananchi au baadhi ya wananchi kuwa wakimbizi au kukosa haki za msingi ambazo ni za binadamu (kwa mujibu wa Azimio la UM) au zilizoko katika Katiba. Utawala wa kiraia unapoanza kufanya hivyo na hauko tayari kubadili mwelekeo Jeshi lina haki ya kurudi na kuirudisha Katiba mikononi mwa wananchi.
c. Wakati mtawala/utawala wa kiraia unapoanza kampeni ya mauaji, mateso na unyama dhidi ya Raia kwa kutumia vyombo mbalimbali, basi Jeshi lina wajibu wa kuingilia kati na kumsimamisha mtawala huyo.
Hata hivyo, siamini kuwa jeshi lina haki ya kuingilia utawala wa kiraia ati kwa sababu:
a. Sera za chama tawala ni mbovu au utendaji wa serikali ni mbaya. As long as ubovu/ubaya huo unatokana na usimamizi mbaya wa majukumu, uzembe, n.k basi mchakato wa kawaida wa nidhamu na sheria unatakiwa kufuatwa na kama wananchi wameichoka serikali hiyo wanapewa muda wa kuiondoa madarakani kwa kutumia uamuzi wao wenyewe yaani kura.
b. Wananchi wanapopewa nafasi ya kupiga kura na wao katika uchaguzi huru wanaamua kurudisha serikali ile ile mbovu madarakani, wasitarajie jeshi kuwaokoa.
c. Kama kuna kitu ambacho wananchi hawakipendi dhidi ya viongozi wao au serikali yao ni wajibu wao kuelimishana, kufanya kampeni dhidi ya uongozi/kiongozi huyo na kwa hakika kutafuta chaguo jingine kwa njia za kidemokrasia.
You can call this "Mwanakijiji's Principle".