Rais wa Msumbiji awafuta kazi Wakuu wa Majeshi

Rais wa Msumbiji awafuta kazi Wakuu wa Majeshi

Analogia Malenga

JF-Expert Member
Joined
Feb 24, 2012
Posts
5,108
Reaction score
10,191
Rais wa Msumbiji Filipe Nyusi amewafuta kazi wakuu majeshi wa ardhini na angani wakati nchi inapokabiliana na wanamgambo wa Islamic States kaskazini mwa nchi hiyo na uasi wa wanamgambo wanaohusishwa na chama kikuu cha upinzani.

Katika taarifa iliyotolewa usiku Alhamisi rais hakutoa sababu ya kumfuta kazi Ezequiel Isac Muianga, mkuu wa jeshi la ardhini, na Messias André Niposso, mkuu wa jeshi la anga. Rais pia amemfuta kazi kamanda na naibu kamanda wa chuo cha mafunzo ya kijeshi cha Marechal Samora Macheya.

Naibu kamanda wa Taasisi ya mafunzo ya juu ya masuala ya ulinzi pia alifutwa kazi.

Msumbuji imekuwa ikipambana na uasi katika mkoa wenye utajiri wa madini wa Cabo Delgado tangu Oktoba 2017.
Watu nusu milioni wamefurushwa makwao mwaka uliopita pekee.

Kundi la al-Ansar al-Sunna, ambalo linajulikana na wenyeji kama al-Shabab, limehusika na makumi ya mashambulio ya kigaidi ambayo yanakaidiriwa kuuwa mamia ya watu.

Shirika la kutete haki la Amnesty International mwezi huu lilichapisha ripoti inayolaumu majeshi ya Msumbiji wajenzi wa majeshi wa kibinafsi na waasi wanaohudumu katika mkoa wa Cabo Delgado kwa kutekeleza uhalifu wa kivita.

BBC Swahili
 
Attachments

  • 1615552524697.gif
    1615552524697.gif
    42 bytes · Views: 2
Magaidi yanachagua maeneo yenye mafuta,gesi na madini...
 
Hii sio salili nzuri kwetu maana hawa waasi wapo mpakani na kwetu pia walishafanya mashambulizi kadhaa maeneo ya Mtwara....wakizidiwa kwao watahamia kwetu
 
Hii sio salili nzuri kwetu maana hawa waasi wapo mpakani na kwetu pia walishafanya mashambulizi kadhaa maeneo ya Mtwara....wakizidiwa kwao watahamia kwetu
Walishahamia ila kilichowakuta siri yao.!
 
Walishahamia ila kilichowakuta siri yao.!
Hawa watu sio wa kujitapa kua umewashinda haya jamaa wana ari kubwa sana si rahisi kukubali kushindwa.

Kitu ikishahusisha imani/dini hua haimalizwi kirahisi
 
Hawa watu sio wa kujitapa kua umewashinda haya jamaa wana ari kubwa sana si rahisi kukubali kushindwa.
Kitu ikishahusisha imani/dini hua haimalizwi kirahisi
Tumesha washughulikia kunywa juice kwa amani.
 
Dogo Nyusi keshauelewa mchezo kuwa anazungukwa,haiwezekani vitoto vyenye mapanga na sime viteke eneo lenye mali za matrion ya $$$$$$$
Marekani imetangaza kumuwekea vikwazo mtanzania boss wa vita ya cape delgado
 
Hawa watu sio wa kujitapa kua umewashinda haya jamaa wana ari kubwa sana si rahisi kukubali kushindwa.

Kitu ikishahusisha imani/dini hua haimalizwi kirahisi
Hawa wamejificha kwenye kivuli cha iman/ dini ili wapate uungwaji mkono wa upande wa iman
 
Back
Top Bottom