Roving Journalist
JF Roving Journalist
- Apr 18, 2017
- 3,984
- 13,760
Baada ya kuwasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere, Nyusi alipokelewa na viongozi mbalimbali wa Serikali, wakiongozwa na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. January Makamba, Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Mhe. Albert Chalamila, na Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara, Mhe. Exaud Kigahe.
Akizungumza na vyombo vya habari muda mfupi kabla ya kuwasili kwa Rais Nyusi, Waziri Makamba amesema ziara hiyo inalenga kuimarisha uhusiano wa kidiplomasia na wa kihistoria kati ya nchi hizo mbili, hasa katika sekta za biashara, uwekezaji, na usalama.