#COVID19 Rais wa Msumbiji Filipe Nyusi na mke wake Isaura Nyusi wamekutwa na virusi vya corona

#COVID19 Rais wa Msumbiji Filipe Nyusi na mke wake Isaura Nyusi wamekutwa na virusi vya corona

Analogia Malenga

JF-Expert Member
Joined
Feb 24, 2012
Posts
5,108
Reaction score
10,191
1641301555033.png

Rais wa Msumbiji Filipe Nyusi na mke wake Isaura Nyusi wamekutwa na virusi vya corona na wamejitenga kwa sasa.

Kwa mujibu wa taarifa kutoka ofisi ya rais Bw. Nyusi na mke wake wameamua kujitenga kwa kuzingatia muongozo wa afya baada ya kupatikana na virusi , ijapokuwa hawakuonesha dalili zozote.

Taarifa hiyo ilisema waliamua kufanya vipimo baada ya "shughuli walizokuwa nazo siku chache zilizopita ".

Kumekuwa na ongezeko la virusi vya corona katika siku za hivi karibuni nchini Msumbiji.

Nchi hiyo imethibitisha kuwa na watu 193,000 wanaougua Covid-19, huku vifo 2,031 vikirekodiwa.

BBC Swahili
 
Ugonjwa hatarishi unaojulikana baada ya mtu kupimwa... kabla ya hapo walikuwa wanadunda tu. Hizo fix ili watu waogope wakafakamie chanjo
 
Back
Top Bottom