Rais wa Namibia Atembelea Majirani zake wa Zamani Magomeni

Mawele

Platinum Member
Joined
Jul 25, 2023
Posts
1,161
Reaction score
4,251
Rais wa Namibia Atembelea Majirani zake wa Zamani Magomeni

Rais wa Jamhuri ya Namibia, Mhe. Dkt. Netumbo Nandi-Ndaitwah, ametemebelea eneo la magomeni katika nyumba aliyowahi kuishi wakati wa harakati za ukombozi wa Namibia kupitia chama cha SWAPO.

Katika ziara hiyo ya kipekee iliyochanganya hisia za kumbukumbu na mshikamano wa kihistoria kati ya Tanzania na Namibia, Rais Nandi-Ndaitwah alipokelewa kwa furaha na majirani zake hao wa Magomeni, akiwemo mama Salehe na mtoto wa mama Salama ambao walimfahamu tangu alipokuwa akiishi eneo hilo akiwa mwakilishi wa harakati za ukombozi.

Akizungumza na wakazi hao, Rais huyo alitoa shukurani zake kwa Serikali na wananchi wa Tanzania kwa mchango wao mkubwa katika harakati za ukombozi wa Namibia, akisisitiza kuwa historia hiyo imejenga uhusiano imara na wa kudumu kati ya mataifa hayo mawili.

“Magomeni ni sehemu ya maisha yangu na historia ya taifa langu. Tanzania ilitupa hifadhi, upendo na nafasi ya kupigania uhuru wetu. Huu ni ushahidi wa urafiki wa kweli na mshikamano wa Afrika,” alisisitiza.

Baada ya mazungumzo hayo, Rais Nandi-Ndaitwah alitembea nyumba aliyowahi kuishi, akapata fursa ya kukumbuka maisha ya miaka hiyo ya mapambano, huku majirani hao wakishiriki kumbukumbu na furaha ya kukutana tena na kiongozi huyo akiwa amefika kuwasilimu katika nafasi yake mpya ya Urais.

Screenshot 2026-06-22 at 13-47-18 Instagram.png

Pia soma: Rais wa Namibia kufanya ziara ya kitaifa nchini 19 - 22 Juni, 2026
 
Ukienda kumtembelea mgonjwa hospitalini na kubaki kumtazama kama tv, bila kumpelekea matunda utaonekanaje?
Kwani lazima umupelekee matunda? Unaweza kumpelekea vitu vingine vinavyomfaa.
 
Chukulia ata hivyo vinavyomfaa hakupelekewa zaidi ya kwenda kutazamwa tu kwa macho, hapo utasemaje?
 
Rais wa Namibia Atembelea Majirani zake wa Zamani Magomeni

Rais wa Jamhuri ya Namibia, Mhe. Dkt. Netumbo Nandi-Ndaitwah, ametemebelea eneo la magomeni katika nyumba aliyowahi kuishi wakati wa harakati za ukombozi wa Namibia kupitia chama cha SWAPO.

Katika ziara hiyo ya kipekee iliyochanganya hisia za kumbukumbu na mshikamano wa kihistoria kati ya Tanzania na Namibia, Rais Nandi-Ndaitwah alipokelewa kwa furaha na majirani zake hao wa Magomeni, akiwemo mama Salehe na mtoto wa mama Salama ambao walimfahamu tangu alipokuwa akiishi eneo hilo akiwa mwakilishi wa harakati za ukombozi.

Akizungumza na wakazi hao, Rais huyo alitoa shukurani zake kwa Serikali na wananchi wa Tanzania kwa mchango wao mkubwa katika harakati za ukombozi wa Namibia, akisisitiza kuwa historia hiyo imejenga uhusiano imara na wa kudumu kati ya mataifa hayo mawili.

“Magomeni ni sehemu ya maisha yangu na historia ya taifa langu. Tanzania ilitupa hifadhi, upendo na nafasi ya kupig.
 
Back
Top Bottom