Rais wa Romania, Klaus-Werner Iohannis kufanya ziara ya Kiserikali Nchini Tanzania

hizi nchi kwetu ni za muhimu sana. nakumbuka zamani nchi kama Uturuki, walikuwa hawategemewi kama watakuwa kiunganishi kikiubwa sana cha kibiashara na Tanzania, lakini sasaivi anachuana na China kwenye soko la bidhaa.
 
HONGERA DR SAMIA, MALIKIA WA MAZINGIRA,
DUNIA INAKUTAFUTA, TANZANIA [emoji1241] TUMEKUPATA.
[emoji91][emoji91][emoji91][emoji91][emoji122][emoji122][emoji122][emoji122][emoji120][emoji120]
 

View: https://www.instagram.com/p/CzqRhCoidTB/?igshid=MTc4MmM1YmI2Ng==
 
Rais wa Jamhuri ya Romania, Mheshimiwa Klaus Iohannis, atafanya Ziara ya Kitaifa nchini kuanzia tarehe 16 hadi 19 Novemba 2023 kwa mwaliko wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan.

Lengo la ziara hiyo ni kukuza na kuimarisha uhusiano wa kidiplomasia kati ya Tanzania na Romania pamoja na kuibua maeneo mapya ya ushirikiano katika sekta mbalimbali kama Uwekezaji, Elimu, Utalii, Afya na Utamaduni.

Uhusiano wa Kibiashara na Uwekezaji Tanzania na Romania zimeendelea kushirikiana katika sekta ya biashara na uwekezaji ambapo bidhaa kuu za Tanzania zinazouzwa Romania ni minofu ya samaki aina ya sangara, chai, tumbaku na parachichi.

Tanzania inanunua kutoka Romania bidhaa za mashine za umeme, vifaa vya matrekta, magari na vifaa vya matibabu. Kupitia ziara hii Tanzania na Roamania zimedhamiria kuinua na kuimarisha kiwango cha biashara kati ya nchi hizi mbili ambacho licha ya Tanzania kuuza zaidi bidhaa zake nchini Romania, kiwango cha biashara kati ya mataifa haya mawili bado ni kidogo na kimeshuka katika miaka ya hivi karibuni ikilinganishwa na fursa za
kibiashara zilizopo.

Mathalani mwaka 2021 Tanzania iliuza Romania bidhaa zenye thamani ya Dola za Marekani Milioni 7.9 ikilinganishwa na mwaka 2022 ambapo iliuza bidhaa zenye thamani ya Dola za Marekani Milioni 4.06. Kadhalika, Romania ilinunua bidhaa zenye thamani ya Dola za Marekani Milioni 11.6 ikilinganishwa na mwaka 2022 ambapo ilinunua bidhaa zenye thamani ya Dola za Marekani Milioni 2.4. Kwa upande wa uwekezaji, Romania imewekeza nchini kwenye miradi ya usafirishaji, viwanda na utalii yenye thamani ya Dola za Marekani milioni 6.04 na kuzalisha ajira 89. Romania pia imewekeza Zanzibar miradi mitatu yenye thamani ya Dola za Marekani Milioni 7.5 kwa mwaka 2023 na kuzalisha ajira 64.

Vilevile ziara hii ni fursa kwa Tanzania kuimarisha soko lake la utalii nchini Romania ambapo kwa sasa takwimu zinaonesha kuwa idadi ya watalii kutoka nchini humo imeongezeka kutoka 6,418 mwaka 2018 na kufikia 12,148 mwaka 2022.​
 
Aangalie asije akapishana na Mwenyeji wake , kwani kisharudi ?
 
Rumania Ulaya ni taifa maskini ni kwa nini utafute mtu maskini awe rafiki yako usitatute tajiri kama China au Marekani? NASEMA hivi ukienda porini tafuta Simba awe rafiki yako na sii swala!
 

View: https://twitter.com/mamanafanikisha/status/1725068409585504630?t=ZWZar10dXUhkF6ylB3sASQ&s=19
 

View: https://twitter.com/mamayukokazini/status/1725491368372387948?t=F_xKzaftFFBTXo6ryF-Mzg&s=19
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…