Rais wa Senegal, Bassirou Diomaye Faye, amemteua Ahmadou Al Aminou Lo kuwa Waziri Mkuu mpya wa nchi hiyo.
Ahmadou Lo, ambaye aliwahi kuwa kiongozi mkuu katika Benki Kuu ya Mataifa ya Afrika Magharibi (BCEAO), ni mtaalamu aliyebobea katika masuala ya uchumi na fedha.
Ofisi ya Rais imesisitiza kuwa uteuzi huu unalenga kuongeza ufanisi katika uongozi na kuharakisha mabadiliko yanayoendelea ili kuwaletea tija wananchi wa Senegal, hasa katika kipindi hiki ambacho nchi hiyo inakabiliwa na changamoto kubwa za kiuchumi na kitaasisi.
Uteuzi huu umekuja baada ya Rais Faye kumfuta kazi mshirika wake wa karibu, Ousmane Sonko, siku ya Mei 22, 2026, ambaye alikuwa ameshikilia nafasi hiyo tangu mwezi Aprili 2024.
Soma pia Spika wa Bunge Senegal ajiuzulu, aeleza ni kwa Maslahi mapana ya Taifa
Source: TRT AFRIKA