Rais wa Senegal, Bassirou Faye: Ufaransa ifunge kambi zake za kijeshi nchini Senegal. Hii ni nchi huru; hatukubaliani na uwepo wa kambi hizo

Wananchi wa Djibouti Hali zao unazijua
 
Nchi ya Chad imetangaza kuvunja makubaliano ya ushirikiano wa kijeshi kati yake na Ufaransa.

Hatua hiyo imetangazwa na waziri wa mambo ya nje wa Chad Abderaman Koulamallah mnamo tarehe 28 Novemba 2024 kupitia kurasa zake za mitandao ya kijamii ikiwa ni siku moja baada ya ziara ya waziri wa mambo ya nje wa Ufaransa Jean-Noel Barrot nchini Chad.

Kutokana na kuvunjwa kwa makubaliano hayo, wanajeshi wa Ufaransa takribani elfu moja walioko Chad sasa watalazimika kuondoka nchini humo ingawa tarehe rasmi ya kuondoka kwao haijatangazwa.

Hatua hii ni pigo kubwa kwa Ufaransa na ushindi kubwa kwa uhuru wa Afrika baada ya nchi za Niger, Mali na Burkina Faso zinazounda umoja wa nchi za Sahel ( AES) kuwafukuza wanajeshi wa Ufaransa kutoka kwenye nchi zao.

Itakumbukwa kwamba Chad iliwafukuza kutoka nchini mwake wanajeshi wa Marekani mnamo mwezi Mei 2024 ingawa Serikali ya Marekani ilitoa taarifa kwamba inafanya mazungumzo na serikali ya Chad Ili wanajeshi wa Marekani waweze kurudi nchini humo.

Vyanzo/ Sources :
France 24
Reuters
 
Hapo ni kutawaliwa afu unapozwa kwa barafu, walifanya vizuri sana JWTZ kukufukuza wewe mapema, huna akili kabisa. Unauza nchi kwa Dollar eti million 30 kwa mwaka.
Kapitie mikataba ya migodi , bandari na miradi ya barabara na umeme , utaelewa nan ameuzwa Djibouti au Ww Mdanganyika
 
Wakati huo majirani zetu Kenya wanajivunia uwepo base za marekani na British
 
Yemen hata US kapiga magoti umfanananishe na Djibouti, we kweli wa Mirembe. Djibouti wakumfananisha na Israel.
Hivi umeuona umasikini uliopo Yemen?!

Hivi mnafikiri US akiamua kuingia Yemen na kuwaondoa hao Wahouthi atashindwa?!
 
Kapitie mikataba ya migodi , bandari na miradi ya barabara na umeme , utaelewa nan ameuzwa Djibouti au Ww Mdanganyika
Wewe nenda US kangalie bandari nani anaziendesha hi ya Tanzania nini wewe. Barabara kila nchi inapigwa pesa sio Tanzania tu, Umeme vile vile mambo ya migodi wewe view yako sio sawa na view ya serekali.
 
Wewe nenda US kangalie bandari nani anaziendesha hi ya Tanzania nini wewe. Barabara kila nchi inapigwa pesa sio Tanzania tu, Umeme vile vile mambo ya migodi wewe view yako sio sawa na view ya serekali.
Lete mikataba ya uwekezaj ya USA na Hii ya kwenu tuisome na utuambie kama inafanana
 
Ufaransa kakaliwa kooni kila pembe wanamkataa safi sanaaa watu Wanaanza kujitambua
Utawala wa ndugu Macron umekumbwa na balaa gani, mbona anapoteza makoloni yake tofauti na watangulizi wake Kina De Gaulle, Chiraq etc
 
Wanajivunia wanajeshi wa kigeni kubaka wanawake wa Kenya, kuwaua raia na kuharibu ardhi yao kwa mazoezi ya kijeshi?? Kuna documentary YouTube inahusu masaibu wanayokutana nayo wakenya kutokana na hizo bases za kigeni. Ungejua hata usingesema wanajivunia . Yaani kama waingereza wanaua raia na hakuna kitu serikali ya Kenya inafanya
Wakati huo majirani zetu Kenya wanajivunia uwepo base za marekani na British
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…