Rais wa Senegal, Bassirou Faye: Ufaransa ifunge kambi zake za kijeshi nchini Senegal. Hii ni nchi huru; hatukubaliani na uwepo wa kambi hizo

Rais wa Senegal, Bassirou Faye: Ufaransa ifunge kambi zake za kijeshi nchini Senegal. Hii ni nchi huru; hatukubaliani na uwepo wa kambi hizo

Sorry nilidhani unaniuliza France wamepata faida gani?...Djibouti inapata Dola millioni 30 kila mwaka halafu local economy pia inafaidika kuwepo na maelfu ya Askari na familia zao ambao hununua kwenye Market zao Maduka yao nk.

Askari wakilipwa mishahara Bar Nightclubs za Waisilamu wa Djibouti hupata maelfu ya Wateja.
Wananchi wa Djibouti Hali zao unazijua
 
Nchi ya Chad imetangaza kuvunja makubaliano ya ushirikiano wa kijeshi kati yake na Ufaransa.

Hatua hiyo imetangazwa na waziri wa mambo ya nje wa Chad Abderaman Koulamallah mnamo tarehe 28 Novemba 2024 kupitia kurasa zake za mitandao ya kijamii ikiwa ni siku moja baada ya ziara ya waziri wa mambo ya nje wa Ufaransa Jean-Noel Barrot nchini Chad.

Kutokana na kuvunjwa kwa makubaliano hayo, wanajeshi wa Ufaransa takribani elfu moja walioko Chad sasa watalazimika kuondoka nchini humo ingawa tarehe rasmi ya kuondoka kwao haijatangazwa.

Hatua hii ni pigo kubwa kwa Ufaransa na ushindi kubwa kwa uhuru wa Afrika baada ya nchi za Niger, Mali na Burkina Faso zinazounda umoja wa nchi za Sahel ( AES) kuwafukuza wanajeshi wa Ufaransa kutoka kwenye nchi zao.

Itakumbukwa kwamba Chad iliwafukuza kutoka nchini mwake wanajeshi wa Marekani mnamo mwezi Mei 2024 ingawa Serikali ya Marekani ilitoa taarifa kwamba inafanya mazungumzo na serikali ya Chad Ili wanajeshi wa Marekani waweze kurudi nchini humo.

Vyanzo/ Sources :
France 24
Reuters
 
Hapo ni kutawaliwa afu unapozwa kwa barafu, walifanya vizuri sana JWTZ kukufukuza wewe mapema, huna akili kabisa. Unauza nchi kwa Dollar eti million 30 kwa mwaka.
Kapitie mikataba ya migodi , bandari na miradi ya barabara na umeme , utaelewa nan ameuzwa Djibouti au Ww Mdanganyika
 

Rais wa Senegal, Bassirou Diomaye Faye, amesema kuwa Ufaransa inapaswa kufunga kambi zake za kijeshi nchini humo, wakati taifa hilo linajiandaa kuadhimisha kumbukumbu ya miaka 80 ya mauaji ya kikatili yaliyofanywa wakati wa ukoloni.

Rais wa Ufaransa, Emmanuel Macron, amekiri kuwa vikosi vya Ufaransa vilihusika na "mauaji" ya wanajeshi wa Senegal mnamo 1944. Akizungumza na shirika la habari la AFP, Faye alisema hatua hiyo ni ya kupongezwa, lakini uwepo wa kambi za kijeshi za Ufaransa nchini Senegal hauendani na mamlaka ya kitaifa.

"Senegal ni nchi huru, ni taifa lenye mamlaka yake, na mamlaka ya kitaifa haikubaliani na uwepo wa kambi za kijeshi ndani ya nchi huru," alisema Faye katika mahojiano yaliyofanyika kwenye ikulu ya rais.

Kuondoa Vikosi vya Ufaransa​

Faye, ambaye alichaguliwa kuwa rais Machi mwaka huu, aliahidi kuimarisha mamlaka ya Senegal na kuondoa utegemezi kwa mataifa ya kigeni. Hata hivyo, alisisitiza kuwa hatua hiyo haina maana ya kuvunja uhusiano na Ufaransa.

Nchi nyingine kadhaa zinazozungumza Kifaransa barani Afrika, zikiwemo Mali, Burkina Faso, na Niger, ambako wanajeshi wamechukua madaraka, zimefukuza vikosi vya Ufaransa na kutafuta washirika mbadala wa usalama.

Kwa mujibu wa vyanzo viwili vya serikali ya Ufaransa vilivyozungumza na AFP mwaka huu, Ufaransa inapanga kupunguza uwepo wake wa kijeshi barani Afrika. Idadi ya wanajeshi nchini Senegal na Gabon itapunguzwa kutoka 350 hadi 100, nchini Chad kutoka 1,000 hadi 300, na Côte d’Ivoire kutoka 600 hadi 100.

"Ufaransa inabaki kuwa mshirika muhimu kwa Senegal katika uwekezaji, uwepo wa kampuni za Kifaransa, na hata raia wa Kifaransa walioko Senegal," alisema Faye.

Macron Akiri Mauaji​

Rais wa Senegal alisema amepokea barua kutoka kwa Macron inayokiri kuwa Ufaransa inahusika na mauaji ya kambi ya Thiaroye yaliyotokea Desemba 1, 1944. Tukio hilo limekuwa chanzo cha mvutano kati ya Paris na Dakar kwa miaka mingi.

Mnamo Novemba 1944, takriban wanajeshi 1,600 wa Kiafrika waliokuwa wametumikia Ufaransa na kushikiliwa mateka na Ujerumani walirejeshwa Dakar. Baada ya kuwasili katika kambi ya Thiaroye nje ya Dakar, walilalamika kuhusu kucheleweshwa kwa malipo yao, na baadhi wakakataa kurudi makwao bila kulipwa haki zao.

Vikosi vya Ufaransa vilifyatua risasi kwa waandamanaji, na kuua angalau watu 35, ingawa wanahistoria wanasema idadi inaweza kuwa kubwa zaidi.

Kudai Msamaha​

"Nimepokea barua kutoka kwa Rais Emmanuel Macron akiweka wazi kuwa yale yalikuwa ni mauaji, bila utata wowote," alisema Faye.

Faye aliipongeza hatua hiyo ya Rais wa Ufaransa, ambaye pia ameomba radhi kwa kushindwa kuhudhuria maadhimisho ya miaka 80 ya tukio hilo.

Alisema anafikiria kudai msamaha rasmi kutoka Ufaransa.

"Kukiri kuwa mauaji yalifanyika kunapaswa kuleta matokeo ya kulipa fidia. Tunaamini kwamba hilo ni jambo linalopaswa kufuatia hatua hii."
Wakati huo majirani zetu Kenya wanajivunia uwepo base za marekani na British
 
Yemen hata US kapiga magoti umfanananishe na Djibouti, we kweli wa Mirembe. Djibouti wakumfananisha na Israel.
Hivi umeuona umasikini uliopo Yemen?!

Hivi mnafikiri US akiamua kuingia Yemen na kuwaondoa hao Wahouthi atashindwa?!
 
Kapitie mikataba ya migodi , bandari na miradi ya barabara na umeme , utaelewa nan ameuzwa Djibouti au Ww Mdanganyika
Wewe nenda US kangalie bandari nani anaziendesha hi ya Tanzania nini wewe. Barabara kila nchi inapigwa pesa sio Tanzania tu, Umeme vile vile mambo ya migodi wewe view yako sio sawa na view ya serekali.
 
Wewe nenda US kangalie bandari nani anaziendesha hi ya Tanzania nini wewe. Barabara kila nchi inapigwa pesa sio Tanzania tu, Umeme vile vile mambo ya migodi wewe view yako sio sawa na view ya serekali.
Lete mikataba ya uwekezaj ya USA na Hii ya kwenu tuisome na utuambie kama inafanana
 
Ufaransa kakaliwa kooni kila pembe wanamkataa safi sanaaa watu Wanaanza kujitambua
Utawala wa ndugu Macron umekumbwa na balaa gani, mbona anapoteza makoloni yake tofauti na watangulizi wake Kina De Gaulle, Chiraq etc
 
Wanajivunia wanajeshi wa kigeni kubaka wanawake wa Kenya, kuwaua raia na kuharibu ardhi yao kwa mazoezi ya kijeshi?? Kuna documentary YouTube inahusu masaibu wanayokutana nayo wakenya kutokana na hizo bases za kigeni. Ungejua hata usingesema wanajivunia . Yaani kama waingereza wanaua raia na hakuna kitu serikali ya Kenya inafanya
Wakati huo majirani zetu Kenya wanajivunia uwepo base za marekani na British
 
Back
Top Bottom