Rais wa Senegal, Bassirou Faye: Ufaransa ifunge kambi zake za kijeshi nchini Senegal. Hii ni nchi huru; hatukubaliani na uwepo wa kambi hizo

Wanajivunia wanajeshi wa kigeni kubaka wanawake wa Kenya, kuwaua raia na kuharibu ardhi yao kwa mazoezi ya kijeshi?? Kuna documentary YouTube inahusu masaibu wanayokutana nayo wakenya kutokana na hizo bases za kigeni. Ungejua hata usingesema wanajivunia . Yaani kama waingereza wanaua raia na hakuna kitu serikali ya Kenya inafanya
Kila siku wanatamba
 
Utawala wa ndugu Macron umekumbwa na balaa gani, mbona anapoteza makoloni yake tofauti na watangulizi wake Kina De Gaulle, Chiraq etc
Mapinduzi ya Sahel yameamsha wengi. Pia internet na social media sasahivi hudanganyi mtu. Taarifa zote tunazo. Pia tunakumbuka Ufaransa ilivyochangia pakubwa yaliyotokea Libya mwaka 2011. Na pia inasemekana kuna mkono wa Bwana Putin ingawa hilo siwezi kuthibitisha
Kila lenye mwanzo halikosi kuwa na mwisho
 
Hivi umeuona umasikini uliopo Yemen?!

Hivi mnafikiri US akiamua kuingia Yemen na kuwaondoa hao Wahouthi atashindwa?!
Unadhani hatamani kuwaondoa eeenh Yale mabomu waliokua wanawapiga Wahouthi tokea mwaka 2014 mpaka 2021 unadhani walikua anania nao gani
 
Utawala wa ndugu Macron umekumbwa na balaa gani, mbona anapoteza makoloni yake tofauti na watangulizi wake Kina De Gaulle, Chiraq etc
Kwakweli sijajua macron anakumbwa nanini ila nakumbuka kuna day nilisikiliza uchambuzi DW pale kuna jamaa kama sijakosea anaitwa Ahmed Salim mwamba alielezea tu kwamba Watawala vijana wamechoshwa na sera za ufaransa ufaransa wana sera moja Ile ya pesa sijui jamaa aliichambua vyema nimeisahau tu hakuna mkoloni mzuri ila mkoloni mfaransa hafai hafai hafai na hapo west Africa anaondoka jumla ni suala la muda tu kwa sasa anaendelea kumzibia awepo hapo ni Nigeria 🇳🇬 kama Senegal 🇸🇳 atafanya kweli basi na Nigeria anafuata na akisepeshwa na Nigeria kwisha habari zake yaani
 
Kuna mikataba ya uhuru ambayo nchi zilizokuwa makoloni ya Ufaransa zililazimishwa kusaini Ili zipate uhuru. Zote zilisaini isipokuwa Guinea, Morocco na Algeria. Na pia hao ambao hawakusaini haikuwa rahisi walipoteza mamilioni ya raia Ili wapate uhuru bila kusaini hiyo mikataba. Ukiisoma utamwaga machozi. Ufaransa anachokifanya ni zaidi ya unyonyaji. Hamna lugha ya kuelezea. Acha wamfukuze tu. WAMECHOKA
 
Unadhani hatamani kuwaondoa eeenh Yale mabomu waliokua wanawapiga Wahouthi tokea mwaka 2014 mpaka 2021 unadhani walikua anania nao gani
US ni Superpower ikiamua kuwachakaza hao Houthi anaweza.
 
Kuna mikataba ya uhuru ambayo nchi zilizokuwa makoloni ya Ufaransa zililazimishwa kusaini Ili zipate uhuru. Zote zilisaini isipokuwa Guinea, Morocco na Algeria. Na pia hao ambao hawakusaini haikuwa rahisi walipoteza mamilioni ya raia Ili wapate uhuru bila kusaini hiyo mikataba. Ukiisoma utamwaga machozi. Ufaransa anachokifanya ni zaidi ya unyonyaji. Hamna lugha ya kuelezea. Acha wamfukuze tu. WAMECHOKA
Asee wafaransa washenzi sana kwakweli
 
Rais wa Senegal, Bassirou Diomaye Faye, amesema kuwa Ufaransa inapaswa kufunga kambi zake za kijeshi nchini humo, wakati taifa hilo linajiandaa kuadhimisha kumbukumbu ya miaka 80 ya mauaji ya kikatili yaliyofanywa wakati wa ukoloni.

Rais wa Ufaransa, Emmanuel Macron, amekiri kuwa vikosi vya Ufaransa vilihusika na "mauaji" ya wanajeshi wa Senegal mnamo 1944. Akizungumza na shirika la habari la AFP, Faye alisema hatua hiyo ni ya kupongezwa, lakini uwepo wa kambi za kijeshi za Ufaransa nchini Senegal hauendani na mamlaka ya kitaifa.

"Senegal ni nchi huru, ni taifa lenye mamlaka yake, na mamlaka ya kitaifa haikubaliani na uwepo wa kambi za kijeshi ndani ya nchi huru," alisema Faye katika mahojiano yaliyofanyika kwenye ikulu ya rais.

Kuondoa Vikosi vya Ufaransa​

Faye, ambaye alichaguliwa kuwa rais Machi mwaka huu, aliahidi kuimarisha mamlaka ya Senegal na kuondoa utegemezi kwa mataifa ya kigeni. Hata hivyo, alisisitiza kuwa hatua hiyo haina maana ya kuvunja uhusiano na Ufaransa.

Nchi nyingine kadhaa zinazozungumza Kifaransa barani Afrika, zikiwemo Mali, Burkina Faso, na Niger, ambako wanajeshi wamechukua madaraka, zimefukuza vikosi vya Ufaransa na kutafuta washirika mbadala wa usalama.

Kwa mujibu wa vyanzo viwili vya serikali ya Ufaransa vilivyozungumza na AFP mwaka huu, Ufaransa inapanga kupunguza uwepo wake wa kijeshi barani Afrika. Idadi ya wanajeshi nchini Senegal na Gabon itapunguzwa kutoka 350 hadi 100, nchini Chad kutoka 1,000 hadi 300, na Côte d’Ivoire kutoka 600 hadi 100.

"Ufaransa inabaki kuwa mshirika muhimu kwa Senegal katika uwekezaji, uwepo wa kampuni za Kifaransa, na hata raia wa Kifaransa walioko Senegal," alisema Faye.

Macron Akiri Mauaji​

Rais wa Senegal alisema amepokea barua kutoka kwa Macron inayokiri kuwa Ufaransa inahusika na mauaji ya kambi ya Thiaroye yaliyotokea Desemba 1, 1944. Tukio hilo limekuwa chanzo cha mvutano kati ya Paris na Dakar kwa miaka mingi.

Mnamo Novemba 1944, takriban wanajeshi 1,600 wa Kiafrika waliokuwa wametumikia Ufaransa na kushikiliwa mateka na Ujerumani walirejeshwa Dakar. Baada ya kuwasili katika kambi ya Thiaroye nje ya Dakar, walilalamika kuhusu kucheleweshwa kwa malipo yao, na baadhi wakakataa kurudi makwao bila kulipwa haki zao.

Vikosi vya Ufaransa vilifyatua risasi kwa waandamanaji, na kuua angalau watu 35, ingawa wanahistoria wanasema idadi inaweza kuwa kubwa zaidi.

Kudai Msamaha​

"Nimepokea barua kutoka kwa Rais Emmanuel Macron akiweka wazi kuwa yale yalikuwa ni mauaji, bila utata wowote," alisema Faye.

Faye aliipongeza hatua hiyo ya Rais wa Ufaransa, ambaye pia ameomba radhi kwa kushindwa kuhudhuria maadhimisho ya miaka 80 ya tukio hilo.

Alisema anafikiria kudai msamaha rasmi kutoka Ufaransa.

"Kukiri kuwa mauaji yalifanyika kunapaswa kuleta matokeo ya kulipa fidia. Tunaamini kwamba hilo ni jambo linalopaswa kufuatia hatua hii."
.mrusii balaaa huyooo anaingiza timu
 
Attachments

  • 89C5054F-64C0-4369-A9C8-D85CE41105AA.jpeg
    89C5054F-64C0-4369-A9C8-D85CE41105AA.jpeg
    63.1 KB · Views: 1
Ufaransa kakaliwa kooni kila pembe wanamkataa safi sanaaa watu Wanaanza kujitambua
Kituo kinachofuata ni Mauritania na Chad +Gambia
Mfaransa ni mshenzi sana yaani huyu ndio mkoloni mpuuzi ambaye bado naendelea kukumbatia makoloni yake kama mali yake , yaani hiyo west Africa ,Central na North aliimegea kipande kikubwa na bado anaendelea kukikumbatia mpaka leo
Mpuuzi sana
Wafurushwe huko kama walivyotimuliwa mali ,bukina , Niger
 
Back
Top Bottom